Pre GE2025 Paul Makonda: Arusha hawakupata barabara kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara!

Pre GE2025 Paul Makonda: Arusha hawakupata barabara kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa hivyo alivunja barabara zilizokuwepo?. Yani wabunge wa miaka 50 wa CCM washindwe halafu lawama kwa Sugu kisa ni upinzani.
Avunje kwani alijenga yeye? Kwanza za zamani zinakuwa zimechakaa inahitajioa Mpya ndio hizo Sugu alishindwa Kwa sababu ali wrong number 😂😂
 
Unapigana na mwenyekiti wa CCM aliyesema makusanyo yanaingia kwenye mifuko ya wajanja?.

Ni hivi ukishakuwa mbunge unahaki sawa kwenye utekelezaji wa maendeleo Kama wabunge wengine. Ndio maana katiba inatambua status ya mbunge na sio chama chake.
Siku zote wajanja Huwa sio wengi na Wala hawaibi makusanyo mengi saaana.

Mwenyekiti anataka waache udokozi,otherwise Sasa tunakusanya 2.5T kutoka 1.5T mwaka 2021.

Rekodi hii haijawahi wekwa ila Bado hazitoshi inatakiwa walau tungekuwa kwenye 3T/M
 
Maamuzi ya kujenga barabara ni ya Serikali, hivyo staki kuamini kuwa Serikali ilizuiwa na majungu kujenga

CCM inaunda Serikali na kuwasimamia Watumishi.
Kinachoshangaza ni wana ccm kuwa wa kulialia kwenye majukwaa. Wakati kuanzia serikali ya kitongoji/mitaa mpaka serikali kuu ni yao nchi nzima. Tukiwaambia mmeishiwa maarifa na uwezo wa kuongoza serikali mnakimbilia kuteka na kupoteza wanaowaeleza ukweli.
 
Avunje kwani alijenga yeye? Kwanza za zamani zinakuwa zimechakaa inahitajioa Mpya ndio hizo Sugu alishindwa Kwa sababu ali wrong number 😂😂

Aiseeh! Uchama umekufunika macho huoni mbele. Yani serikali iliona Bora wananchi wabaki na barabara mbovu kisa mbunge ni Sugu. Aiseeh unafurahisha sana
 
Aiseeh! Uchama umekufunika macho huoni mbele. Yani serikali iliona Bora wananchi wabaki na barabara mbovu kisa mbunge ni Sugu. Aiseeh unafurahisha sana
Uchawa ndio nini? Sasa itajihusisha vipi wakati ilikataliwa? Waliopewa dhamana za Kisasa watekeleze ahadi zao Sasa 😆😆
 
Kinachoshangaza ni wana ccm kuwa wa kulialia kwenye majukwaa. Wakati kuanzia serikali ya kitongoji/mitaa mpaka serikali kuu ni yao nchi nzima. Tukiwaambia mmeishiwa maarifa na uwezo wa kuongoza serikali mnakimbilia kuteka na kupoteza wanaowaeleza ukweli.
Wanalia au wanaikumbusha Serikali wajibu wake ?
 
Sio kujipendekeza Bali lazima uwe kwenye chama husika vinginevyo utapata tabu sana kama sio Kutengwa kabisa
Ndio maana nasema ni siasa za kishamba. Kama kuwa hicho chama cha wazee ndio unapata barabara nzuri, huko vijijini ambako ni ccm kwa lazima mbona ndio umasikini umeshika kasi? Bado mna siasa hizo za kishamba?
 
Ndio maana nasema ni siasa za kishamba. Kama kuwa hicho chama cha wazee ndio unapata barabara nzuri, huko vijijini ambako ni ccm kwa lazima mbona ndio umasikini umeshika kasi? Bado mna siasa hizo za kishamba?
Chama Cha kijnja kiliparalyse maendeleo ya Arusha na kuigeuza kambi ya intarahamwe Kila siku maandamano.

Saizi si unaona imetulia tuliii
 
Mkoa hauna hata stendi yenye hadhi na yeye anaendeleza majungu yake hayo hayo.
 
Mfumo wa Vyama vingi ni kuja na sera mbadala,Kwa hapa Tanzania Wapinzani wamefeli vibaya.

Chama chako kina sera zipi mbadala kwenye Kilimo?

..Chadema walishinda halmashauri halafu Magufuli akapora mapato ya halmashauri na kuyapeleka serikali kuu. Matokeo yake ni halmashauri zilizoongozwa na Chadema kushindwa kutekeleza ilani zao kulingana na sera zao.
 
Wanalia au wanaikumbusha Serikali wajibu wake ?
Wanaolia ni hao hao wenye serikali. Mkiambiwa mna macho lkn hamuoni mna masikio lkn hamsikii mna elimu lkn bado hirizi hamuachi kuzivaa. Nchi imepigwa upofu kutokana na unafiki wa watendaji wakuu wa serikali. Ina maana bila Waziri kufika maeneo fulani kutoa ahadi ya ujenzi wa barabara basi tena?? Serikali haina mipango kupitia mabaraza ya halmashauri??

Nimemsikia Rais akilalamika kwamba kodi zinazolipwa haziendani na mapato halisi ya walipa kodi. Hapo anamkumbusha nani au serikali ipi?? Ana Mamlaka kwa wezi wa kodi lkn wala hilo halijui.

Jiji lote la Ar liko chini ya ccm halafu Mtendaji huyo huyo wa Serikali ya ccm ndiye wakwanza kulalamika. Kama siyo siasa za maji taka ni nn?? Mpandisheni kwenye majukaa ya siasa akapige majungu vizuri.
 
Ujinga huo huo ndio ulitokea Kwa Sugu akiwa Mbeya.Hatutaki tena saizi tunatamba naTulia na SSH 👇👇
Mnazidi kuthibitisha kuwa tuna serikali ya ovyo sana. Yaani serikali haina mipango mikakati ya maendeleo inayobainisha uwekezaji unaohitajika kuimarisha vyanzo vikuu vya mapato ya nchi?

Serikali inasubiri wanasiasa waiombe barabara na miundombinu muhimu inayohitajika kwenye maeneo makuu ya utalii nchini? Serikali hii iliyojenga na kuimarisha KIA na kununua ndege halafu inaacha barabara mbovu na kuzuia maendeleo mengine ikisubiri kwanza maombi ya mbunge kisha kusikiliza "majungu" na mipasho ya kina Makonda ndipo ifanye kazi?

Mnashabikia ujinga uleule wa kusema "msipochagua ccm hatuleti maendeleo"?

Donald Trump hakukosea. Hiyo ni sthl country. Hamna akili.
 
Adui wa maendeleo ya Tanzania ni wajinga wachache kupewa dhamana ya kuongoza nchi hii. Kwa muda mrefu ccm imeogopa sana kuwa na wagombea binafsi,kwa kuwa ina hakika haipendwi na wengi watakimbilia huko wawe huru, kujiondoa na huu ujinga wa kuita caucus ya chama na kutishana na kipitisha vitu vya hovyo. Inafahamika wabunge wengi wa ccm ni mateka wa kimfumo. Inataka kujitolea sana kama alivyofanya Mh. Mpina ambaye anajua kuna gharama atalipwa. Ccm imejaa wanafiki na wanaendelea kuwakusanya kutoka maeneo mengine kama akina Msigwa.
Anachoongea Makonda ni mfano mzuri wa unafiki uliokithiri, kwamba Arusha haijawahi kuwa na wakuu wa mikoa wa maana isipokuwa yeye!! Jitu lenye sifa ya uuaji na mateso kwa wapinzani mpaka kudhalilisha watu wenye fikra huru kama mzee Warioba kisa kutetea viongozi dhaifu wasiohimili hoja kinzani.
Mbona Mkapa na Nyerere hawakuhangaika na Mrema au Mtikila?
 
Wakuu,

Makonda ameendelea kutoa spana huko Arusha baada ya kusema kuwa wakazi wa mkoa wa Arusha kwa muda mrefu kwa sababu walikuwa wanaendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara.

Kauli hii inakuja baada ya Waziri wa TAMISEMI kufanya ziara mkoani hapo leo October 4.2024 na ndipo mkuu huyo wa mkoa alidokeza kuwa kwa sababu Arusha ilikuwa inaendekeza majungu na ushirikina pamoja na siasa uchwara kwa muda mrefu ndio maana barabara zimechelewa kujengwa.

"Na kwa kweli Arusha hawakupata barabara nyingi kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara. Yaani huko ndio walipokuwa wamebobe. Ni wazee wa shoti."

"Yaani unaweza ukawa umeomba kama hapa jambo tumeliomba kwako, tukichelewa anaweza akazunguka mtu uko ukashangaa barabara inaanza tena kubadilishwa badilishwa."

Huu ni muendelezo wa kauli tata na kandamizi kutoka kwa kauli hiyo ya mkuu wa mkoa!

Kwani walikuwa hawalipi kodi? Viongozi waliokuwepo wa Serikali walitekeleza miradi ipi?
 
Back
Top Bottom