Pre GE2025 Paul Makonda: Arusha hawakupata barabara kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara!

Pre GE2025 Paul Makonda: Arusha hawakupata barabara kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hakuna haja ya chama kimoja ila ni Vyama vingi,watakaoshunda ndio wataamua wapi Wapeleke pesa bila kujalisha wamezikusanya wapi maana wengi wape wachache watafanyiwa uungwana ila hawana maamuzi.

Unapochagua Wapinzani na huwezi shika Serikali umejitumbukiza shimoni ukisubiria huruma ya aliyeshika Dola ,ndio kanuni ya Demokrasia 😄😄

Ndio maana nikasema ulitaka kufanya hivyo kwenye maendeleo uwe chama kimoja. Ukiwa vyama vingi peleka maendeleo kote na sio kwa chama chako tu. Ukifanya hivyo unavunja katiba .
 
Wakuu,

Makonda ameendelea kutoa spana huko Arusha baada ya kusema kuwa wakazi wa mkoa wa Arusha kwa muda mrefu kwa sababu walikuwa wanaendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara.

Kauli hii inakuja baada ya Waziri wa TAMISEMI kufanya ziara mkoani hapo leo October 4.2024 na ndipo mkuu huyo wa mkoa alidokeza kuwa kwa sababu Arusha ilikuwa inaendekeza majungu na ushirikina pamoja na siasa uchwara kwa muda mrefu ndio maana barabara zimechelewa kujengwa.

"Na kwa kweli Arusha hawakupata barabara nyingi kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara. Yaani huko ndio walipokuwa wamebobe. Ni wazee wa shoti."

"Yaani unaweza ukawa umeomba kama hapa jambo tumeliomba kwako, tukichelewa anaweza akazunguka mtu uko ukashangaa barabara inaanza tena kubadilishwa badilishwa."

Huu ni muendelezo wa kauli tata na kandamizi kutoka kwa kauli hiyo ya mkuu wa mkoa!

Maamuzi ya kujenga barabara ni ya Serikali, hivyo staki kuamini kuwa Serikali ilizuiwa na majungu kujenga hizo barabara.
 
Tuletee clip inayoonyesha Lema akionyeshe mkakati ya ujenzi wa barabara maenro husika?

Hata hujui mchakato wa barabara inaanzia wapi. Hilo swali ungemuuliza TANROADS, Waziri wa Fedha na Waziri wa Miundo mbinu.
 
Inasikitisha mtu mzima tena mfuasi wa chama kikuuu cha CCM ambaye haujui madhumuni ya mfumo wa Vyama Vingi Tanzania.Na je huu mfumo ulianzishwa na wananchi au Serikali?Mtu kukosa elimu ya Uraia na kujaza upumbavu kichwani hasara kwa kizazi cha leo na kijacho.
Mfumo wa Vyama vingi ni kuja na sera mbadala,Kwa hapa Tanzania Wapinzani wamefeli vibaya.

Chama chako kina sera zipi mbadala kwenye Kilimo?
 
Rome haikujengwa siku moja Mangi,jiji la Arusha limeanza kupiga hatua siku nyingi na hawa wenzetu pia watafika huko.Si umeona Iringa na Songea wako wapi ukilinganisha na miaka kumi iliyopita?
Shinyanga na Geita ni majiji ya utalii!?....Geita ni halmashauri, shinyanga ni town council...ng'ombe na Mchele haihitaji barabara kihivyo🤣🤣
 
Notajie mbunge mmoja wa CCM aliyejenga barabara kwa pesa zake Yani kilomita kuanzia 10. Kutoka kwenye mifuko wake.
Wabunge wanajenga kutoka kwenye Serikali za Vyama Vyao ,Sasa hamna Serikali mnategemea nini? 😆😆
 
Kwenye kampeni Huwa mna nadi nini? Na mnatekeleza nini?

Kama ni serikali,kazi ya Mbunge ni ipi?

Kazi ya mbunge ni kusimamia serikali kuhakikisha matatizo ya wananchi yaliyo Chini ya serikali yanatatuliwa. Kama maji, afya, barabara etc
 
Punguza ukabila.
hujaishi nao hao watu wanamambo ya kijinga sana kuzungukazunguka na kupinga miradi kama mabarambara wanatabia ya kuifuata wakati wa kutanua ili kumwaga lami wananza kuzungukazunguka wewe fikiria mtu anaotesha mgomba mpaka karibu na nguzo ya umeme hovyo sana
 
Kazi ya mbunge ni kusimamia serikali kuhakikisha matatizo ya wananchi yaliyo Chini ya serikali yanatatuliwa. Kama maji, afya, barabara etc
Wapinzani mkubwa wachache mtasimamia vipi uwajibikaji wa Serikali wakati hamna tool hiyo ambayo inawahitaji muwe wengi Ili mpate Nguvu ya maamuzi?

Mfano Serikali ikiwa inajibu tunatafuta hela miaka inaenda mtawafanyaje?

Hiyo ndio hasara ya kuchagua upande usio sahihi ambao hauwezi kuunda Serikali
 
Back
Top Bottom