Mgodo visa
JF-Expert Member
- Nov 1, 2016
- 3,590
- 3,632
Wajuvi yetu Macho..!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani kwa kauli ya uzi huu umeielewaje? Hapo anatamba kuwa atampa maagizo Rais awatumbue baadhi ya wateule wake. Unajua huyu kweli ni zero brain hajaelewa kuwa kauli yake hiyo ni kuutangazia umma kuwa yeye ana uwezo wa kumpa maagizo Rais na Rais akayatekeleza.Huyu dogo ipo siku atampa maagizo (amri) Rais
Ina Lillah waina illah rajiunaKwani kwa kauli ya uzi huu umeielewaje? Hapo anatamba kuwa atampa maagizo Rais awatumbue baadhi ya wateule wake. Unajua huyu kweli ni zero brain hajaelewa kuwa kauli yake hiyo ni kuutangazia umma kuwa yeye ana uwezo wa kumpa maagizo Rais na Rais akayatekeleza.
Mzee tupiamo ka picha kakoNdugu zangu Watanzania,
Hayo ni maneno yaliyotamkwa kwa ujasiri mkubwa sana na Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa ,ambaye pia ndiye kijana jasiri zaidi kuwahi kutokea katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la sahara,lakini pia ambaye Watanzania wengi wanatamani awe Rais Wa Taifa letu baada ya Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan kumaliza Muda wake mwaka 2030.
Ambapo Mheshimiwa makonda akiwa mkoani njombe amesema kuwa baada ya kukamilisha ziara yake atarejesha mrejesho kwa Mheshimiwa Amiri jeshi mkuu na Rais wetu Mh mama Samia kuwa niliko pita huko nimeona huyu na huyu hawatufai kuendelea katika nafasi zao maana wameshindwa kazi na kutimiza majukumu yao na wanaichonganisha serikali yako na wananchi.
Amesema kuwa kwa hiyo ukiona umetenguliwa katika nafasi yako na yeye Mheshimiwa makonda alipita katika eneo lako basi ujuwe ni yeye kapelekea hivyo kutokana na kushindwa kwako kwa kazi akikokubaini.kwa hiyo usimlaumu Rais au makamu au nani.
Akasema pia kuwa ni bora watu wamchukie kwa furaha ya wengi ambao ni wananchi na kwamba kilichopandishwa kwa maombi hakiwezi kushushwa kwa Majungu.
Ndugu zangu Watanzania niliwaonyeni sana humu jukwaani watumishi wa umma na viongozi tangia awali kuwa ziara za Mheshimiwa Makonda zichukulieni kwa uzito mkubwa sana,msilete nyodo wala uzembe ,kwa kuwa zitawazoa na kuwatupa nje huko.
Niliwaambia kwa kuwasisitiza sana kuwa Mheshimiwa Makonda huwa hataki mchezo wala kulea uzembe wala kuvumilia ubabaishaji . Mh Makonda ni kiongozi asiyeogopa wala kuona haya kusema ukweli hata kama utamchukia lakini yeye kwake nyeupe ni nyeupe na kijiko ni kijiko tu.
Kaeni mkao wa kula kuvuna matunda yenu kwa kadri ya kazi zenu mnazofanya na kutekeleza kulingana na majukumu yenu.maana wakatii mwingine chama kinachukiwa kwa sababu tu ya uzembe ya watu wachache wanaokuwa wameshindwa kutimiza vyema majukumu yao waliyopewa na kuaminiwa.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.View attachment 2898762View attachment 2898763View attachment 2898765View attachment 2898768
Watie moyo wapige kazi sio kuwatia moyo kwa kuwapa maneno ya kwenye kanga kama upo nao unyagoni.Nguo ya kuazima haisitiri makalio na cheo ni dhamana. Kwa kusema ayo niwatie moyo wote mtakaotumbuliwa kuwa kuna maisha nje ya vyeo vyenu hamkuzaliwa na ukurugenzi wala ukuu wa wilaya.
Mje huku tulime bamia na nyie muonje utamu wa kuwa Mtanzania.
Sitaki. Unaogopa wakitumbuliwa utakosa cha kuwadanga?Watie moyo wapige kazi sio kuwatia moyo kwa kuwapa maneno ya kwenye kanga kama upo nao unyagoni.
Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
Mpaka wanyooshe maelezo !Paul Makonda ambaye ni Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa amezungumza hayo akiwa Njombe mjini.
"Na sisi tukimaliza hii ziara tunampelekea ripoti Mwenyekiti wa chama Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba tulipita mkoa fulani lakini kule fulani hatufai, na mimi nimesema acha niwe mbaya kwa furaha ya wengi, wala sipati shaka, nilisema jana kitu kilichopandishwa kwa maombi hakishushwi kwa majungu, kwahiyo wale ambao hamfanyi kazi zenu, siku ukiona ya kwamba umekuwa demoted au umetenguliwa na hayo maeneo nilipita mimi usimlaumu Dkt. Samia, usimlaumu Mzee wetu Mpango, usimlaumu Waziri Mkuu ujuwe ni mimi, malengo yetu ni kuhakikisha haki inatawala" -Makonda
Nini maoni yako?
Credit - JamboTv
Unatumia masaburi kufikiri? Jiulize, kwanini Makonda anawaambia atapeleka ripoti kwa Rais ili watumbuliwe kama wanawajibika vizuri kwenye kazi zao?Lengo lako ni lipi wewe!? Unataka wasiwajibike kwenye kazi zao?!.