Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Naamini hujafanya utafiti wa kutosha kwamba waponama la. Kwa hiyo huna haki ya kuhitimisha kuwa hawapo mawaziri wa namna hiyo.
Yeye kasema ni mawaziri wanaume na wanajuana (anawajua na wanamjua)
Subiri muda.
Kama unaweza ukamuamini Makonda jihesabu tu kuwa IQ yako ni ya D 2. Pole sana
 
Yaani aibu tupu. RC anawapa onyo Mawaziri tena kwa vitisho!! Ndiyo maana tunasema CCM na Serikali yake imeishiwa maarifa.

Hebu fikiria wakati Konda Boy anatoa upupu wake ule, Kuna Watendani Wakuu wa Chama na Serikali walimshangilia.
Ukoo wa panya usipodhibitiana
 
Makonda alitaka kurudi kwenye ukuu wa mkoa, akamwomva Hayati, lakini alimkatalia kwa sababu moja kubwa kwamba alikuwa anaongea uwongo kwa viongozi mbalimbali wa chama eti Hayati Rais Magufuli alikuwa amemtuma akagombee ubunge ili amteue kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Hayati Magufuli mpaka akalazimika kutamka hadhari mbele ya vyombo vya habari kuwa wajumbe wasidanganyike, hakuna mtu ambaye yeye Hayati Magufuli alikuwa amemtuma kwenda kugombea ubunge. Aliyasema hayo akimlenga Makonda.

Uwongo, Makonda hajaanza leo, ni hulka yake. Hakuna mtu mwadilifu kabisa wa nafsi anayeweza kufanya kazi na Makonda.
Kwa hilo kisiasa zetu halina ubaya, alitumia fursa za wajinga wajinga wanaojipendekeza hovyo.
 
“If you don’t stand for something, you’ll fall for anything” Bob Marley.

Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kujaribu kufanya maamuzi ya kuwafurahisha watu, siku ukienda kinyume nao ni ugomvi. Hata uwape nini wana sahau mara moja kisa tu umeenda tofauti nao.

Raisi wa Tanzania atishiwi nyau ndani ya CCM wala serikalini ni swala la kuamua tu kuwatia adabu wasumbufu na maisha yataendelea kama kawaida tu.

Binafsi sio shabiki wa huyu mama kabisa Iła for the right reason, inakera zaidi kuona watu aliwaopa kila kitu bado hawaridhiki wanataka kumpangia maamuzi yake afanye kazi na nani.
 
Bashite, mamlaka ya uteuzi itengue uteuzi wake haraka sana, kwenye kiapo wanakiri na kuahidi kutotoa Siri zozote wanazozijua HADHARANI Kwa maslahi ya TAIFA,au labda Kwa idhini ya Rais,Sasa either ana ruhusa ya Rais katika KUTAMKA huo upuuzi wake au kama Hana basi hiyo nafasi haimstahiki kuendelea nayo.
Hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya, kila kitu kimepangwa nakutekelezwa ipasavyo.
 
Na hapo alipo Arusha ataondolewa na sababu itakuwa hawezi kufanya kazi na viongozi wenzake, kiherehere kikizidi ndo huwa kama hivyo, walioko chini yake wengine ni umri wa baba yake lkn anawananga kama watoto wake hata mdogo wako hauwezi kumpereka kama mbuzi, wakuu wa wilaya wataomba kupangiwa kazi nyingine au kuhamishwa, wakuu wa vitengo wataomba kuhama, tusubiri ....
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ikifika Aprili 15, 2024 atawataja kwa majina Watu wakiwemo Mawaziri wanaotoa fedha za kuwalipa Watu ili wamtukane Rais Samia mitandaoni kama hawataacha.

Akizungumza wakati wa Kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, amesema "Kaka zangu mnaotuma na kulipa watu kumchokoza Mama yangu Samia mnanijua na mimi nawajua, wengine ni Mawaziri leo tarehe 12 iwe mwisho"

Aidha Makonda amemwomba Rais Samia kutoa Fedha za ujenzi wa Kilomita 20 za Lami Jijini humo na kueleza kuwa Wananchi wamemtuma amuombe Mama yake na wanampima kama ni Mama yake kweli

=========

Akitoa salaam za mkoa kwenye kongamano la kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine leo hii 11 April 2024, amesema kuna watu, wakiwemo mawaziri wanawatuma watu kumtukana Rais Samia mitandaoni.

Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya Jumatatu tarehe 14 April 2024.

Unaweza kubashiri ni mawaziri gani wanafanya hujuma hizi dhidi ya bosi wao? Au Makonda anatafuta kiki?

Maana hata jiwe alimdanganya kama hivi, ndiyo maana jiwe akawa karibu sana na Makonda. Jiwe alipokuja kugundua kuwa aliingizwa chaka akamtema.

View attachment 2961639

Source:. Kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine

Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine
Samia akicheka na kima atavuna mabua, Bashite ni ngedere aliyeshindikana
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kauli iliyotolewa na Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda ni nzito kwelikweli,imeitetemesha nchi,imeleta sintofahamu kwa wananchi ,imeleta amsha amsha na kila mtu na neno lake.ni kauli ambayo imeacha maswali mengi kila mtu na majibu yake.kila mtu anawaza ni akina nani hao wanaomhujumu Rais wetu na nini dhamira yao.kwanini walipe watu kwa ajili ya kumtukana Mheshimiwa Mitandaoni? Dhumuni lao wanataka nini? Wanataka Rais Samia akichafuka kwa matusi wao wapate nini? Wana malengo gani?

Nini malengo yao baada ya kuwa Rais ametukanwa sana? Wanataka wampindue Rais uchaguzi ujao? Wanataka kumhujumu? Kwanini wamhujumu? Je ikiwa hao watu wataacha kuwalipa kuwalipa hao watu wanomtukana Mheshimiwa Rais mitandaoni,unafikiri ni njia ipi ya pili au mipango gani mingine watafanya kuendelea kumuhujumu Mheshimiwa Rais? Je ndio utakuwa mwisho wa wao kuachana na mipango wao ovu? Je usalama wa Rais upo kiasi gani kwa yeye kuendelea kuwa na kufaya kazi na watu ambao amewaamini lakini wao wameshindwa kuwa waaminifu kwake mpaka kufikia kulipa watu pesa ili Rais atukanwe na kuhujumiwa kupitia mitandao? Je watu hawa ni vipi wanaweza kufanya kazi kwa weledi wakati hawampendi Rais? Ni vipi wanaweza kutunza siri za baraza la mawaziri? Ni vipi wanaweza shindwa kuvujisha siri za vikao?

Kauli hiyo ni muhimu vyombo vyetu vya usalama kuifanyia kazi kauli hiyo na kumshauri Mheshimiwa Rais kufanya maamuzi ya haraka.maana haiwezekani Mh Rais awe na watu ambao hawapo pamoja,hawana mawazo ya pamoja.ni hatari sana.kwa sababu watu hao watatoa na kuvujisha siri zote za baraza la mawaziri,watavujisha nyaraka za serikali,watavujisha mipango na mikakati yote ya serikali,watamhujumu Rais na serikali yake na nchi kwa ujumla.watafaya kazi chini ya viwango ili Rais alaumiwe na kutukanwa zaidi na zaidi.watafanya maamuzi na kutoa kauli zitakazokuwa zinajenga chuki na kuichongaisha serikali na wananchi.watafanya kila linalowezekana ili Rais Samia aendelee kuchukiwa zaidi na zaidi.

Huwezi ukalala na nyoka ndani na ukasema nyoka hatakuwa na madhara kwako kwa sababu tu unalala juu ya kitanda.kwahakika utakuwa unajidangamya. Nyoka mmoja aliye ndani ya nyumba yako ni hatari zaidi kuliko koboka aliye nje pamoja na Kundi la Simba walio nyuma ya nyumba yako.kama kuna nyoka ndani ni bora upambane kumtoa haraka sana ili ndani kuwe na amani na usalama.

Kauli ya Mheshimiwa Makonda siyo ya bahati mbaya na haiwezi kutolewa kwa bahati mbaya wala kisiasa.hivyo naamini anafahamu anachokizungumza na alichozungumza na mawaziri wanaomhujumu Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Rais hawezi kufanya kazi na kuwa pamoja na watu ambao viapo vyao wameshavisigina na kuingia kazini kumhujumu. Ni lazima hatua zichukuliwe haraka ili kujenga imani na kuaminiana ndani ya baraza.hakunaga jambo dogo na la bahati mbaya katika siasa. Ni hatari sana kuendelea kuishi na shetani kwa matarajio kuwa atabadilika na kuwa malaika mkuu.chui hata aloane hawezi kubadilika na kuwa kondoo wala nyoka akijivua gamba habadiliki na kupunguza sumu yake.atabaki kuwa nyoka yule yule mwenye sumu ile ile na tabia zile zile za nyoka.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Jitahidi uwe Chawa wa CCM ila usiwe Chawa wa Makonda

Safari ya siasa inahitaji weredi wa Hali ya huu play smart Lucas

Unapambana Sana ila just be smart
 
Back
Top Bottom