Hahaaa! Wa-Zanzibar aina ya Jecha wala sio kwamba wanaonewa... in fact wanafahamu wanachokifanya na hawana tatizo sana na wanachokifanya hata kama ni kwa shingo upande! Nasema hivyo kwa sababu ma-CCM Zanzibar yanafahamu kwamba, kuendelea kuwapo kwao madarakani kunategemea CCM Bara kwa kiasi kikubwa!
Hao ni CCM-Zanzibar Ruling Class!!
Sasa hawa CCM Ruling class wakithubutu kufanya kama anachosema
britanicca, basi wajiandae kuiba kura kwa kutumia vifaru na brigade za jeshi manake uibaji wa kawaida hautawasaidia!
That's one but two, wana-CCM Vigogo wa Bara wenye busara sidhani kama wanaweza kuruhusu uhuni kama huo! Kuruhusu uhuni huo itakuwa ni kama kuifufua serikali ya Tanganyika in other way around!! Yaani huku JPM ndie Rais, kule Bashite ( or the like) Makamu wake... PM nae ndo hivyo aendelee kuwa Braza Maja or the like! Hiyo ni serikali ya Tanganyika, and there'll be no justification!
Hawa wenye CCM na nchi yao wameapa kuulinda muungano na Mwenge wa Uhuru kwa gharama yoyote ile! Na hata vigogo wa Bara wanavyo-engineer kumpora madaraka Maalim Seif wala si kwamba wanawapenda sana akina Mohammed Shein na CCM Zanzibar kwa ujumla bali wanafahamu Seif akishaingia pale, muungano waliokula yamini kuulinda utakuwa kwenye majaribu ya karne!!! Ukweli usio na shaka Wazanzibari wengi hawaupendi kabisa muungano na kama ni lazima, basi ni serikali 3!
Sasa kama watakuwa tayari kukifumbia macho kiashiria hatari kabisa kinachoonesha hatimae kuna serikali ya Tanganyika, basi ningefurahi sana hilo litokee kwa sababu, ningefurahi sana kuona wanavyovurugana.