Paul Makonda: Ukitaka kujua kwanini Tanzania ni maskini pitia mkataba wa Yanga wanaosaini Leo

Paul Makonda: Ukitaka kujua kwanini Tanzania ni maskini pitia mkataba wa Yanga wanaosaini Leo

Afadhali mkataba wa Yanga tutauona mikataba ya gesi mbona hatuioni.
Ile mikataba ya kichina inatutia mashaka sana maana inawezekana tukawa tumepigwa bei
 
Yaani kwa hiki alichokiandika Makonda ingekuwa nchi za wenzetu asingeendelea kuwa katika nafasi hiyo kwani ni wazi uwezo wake wa kufikiri na kutenda ni mdogo sana.
 
Mi nilifikiri huyu jamaa angetuambia kwamba tunataka kujua kwa nini Dar ni chafu hadi leo tunakumbwa na kipindupindu, basi tusome mikataba ya usafi baina ya kampuni za kuzoa taka na halmashauri za jiji...........
Umenikumbusha ile kampuni ya budege
 
Watanzania tuna tatizo gani? Ina maana kama tumeibiwa kwenye mikataba ya gesi na madini basi ni halali kwa Yanga kuwa na mkataba wa kinyonyaji?
 
Mh paul Makonda kajaribu kuonyesha ni jinsi gani Mikataba inayoingiwa serikalini bila hata kupitiwa kwa makini inaitia nchi katika umaskini .Tusipinge kila kitu
 
Hadi hapa sijaona hata mmoja aliyeonyesha dhamira ya kujua hoja ya Makonda inalala kwenye msingi gani, badala yake nimeona mashambulizi binafsi na excuse ya makosa ya huu kwa ulinganishaji wa hili na madudu ya mikataba mingine tofauti
 
Huyu aachane na mambo ya mkataba wa watu, yeye amfate manji amwombe mchango wa madawati full stop.
 
Mh paul Makonda kajaribu kuonyesha ni jinsi gani Mikataba inayoingiwa serikalini bila hata kupitiwa kwa makini inaitia nchi katika umaskini .Tusipinge kila kitu
Pata like yangu mkuu, kingine amejaribu kuonesha jinsi tunavyojifunga muda mrefu. Just imagine miaka 10??seriously
 
Tatizo sio mkataba, tatizo tunaingia mkataba gani na kwa muda gani?? Okay after ten years yanga itakuwa inakipi cha ziada kipya?? Atajenga uwanja?? Atafungua vitega uchumi?? Yaani ataifanyia nin yanga
 
Pengine Makonda yupo sahihi mana hapo kaongea kama mdau wa mpira na si mkuu wa mkoa(kisiasa zaidi) hivyo yawezekana anawaonea huruma watani zake Yanga mana ye ni Simba damu.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Kaongea kama mkuu wa mkoa au shabiki? Hashindwi kutoa tamko kisa yanga iko mkoa wake
 
Alianza Zito, akaja tundu lisu, sasa makonda.

Coincidently, hawa wote ni Simba damu!! Lakini pamoja na hilo, mkataba wa Manji (wanachama wanapata 25%) bado ni bora kuliko wa madini (ambao serikali inapata 3%).
 
Nime jidanganya kuamini kuwa niko kwenye Jukwaa sahihi kuburudisha akili yangu huku nako siasa zime shikamana,dah!
 
  • Thanks
Reactions: MC7
makonda anaelewa kuwa masuala ya michezo hayaingiliwi na serikali?....kwahiyo ajitahidi kuongea kama mshabiki au mwanachama wa yanga na sio kiongozi wa serikali. na afuate taratibu na kanuni za uendeshaji wa vilabu vya mipira tanzania na duniani....vikao ndiko hutolewa maoni na malalamiko...sasa anapokuja kutoa kwenye mitandao ya kijamii kwanini hakuuliza kwenye mkutano mkuu wa jumamosi iliyopita?

Naamini ni wewe kati ya wake wanaodai demokrasia! Iweje umshutumu Makonda kwa uhuru alio nao, kama Mtanzania, kuongea yaliyo moyoni bila ulazima wa kuyasema hayo kwenye vikao vya kilabu, kwa jinsi ya kanuni zake!
 
Naamini ni wewe kati ya wake wanaodai demokrasia! Iweje umshutumu Makonda kwa uhuru alio nao, kama Mtanzania, kuongea yaliyo moyoni bila ulazima wa kuyasema hayo kwenye vikao vya kilabu, kwa jinsi ya kanuni zake!
Mpira wa miguu hauna democrasia... Democrasia ipo kwenye siasa tuu
 
Back
Top Bottom