JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepost video fupi katika ukurasa wake wa Instagram akionyesha yupo mbugani akiwa anakula maisha.
Japo hajaeleza kuwa yupo katika mbuga ipi lakini video inaonyesha ni mazingira ya mbugani, na hajaandika chochote kuelezea video hiyo ambayo ameonekana akipata burudani ya muziki.
Wiki iliyopita Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ilitoa kibali cha kuchapisha gazetini wito wa kumuita Mahakamani Makonda na kuubandika wito huo katika Makazi yake ya Dar na Kijijini kwao Koromije.
Katika kesi hiyo, Saed Kubenea anaomba kuweza kumshtaki Paul Makonda japokuwa Makonda hajaonekana Mahakamani. Kesi, ambapo Mahakama imesogeza mbele suala hilo hadi Machi 2, 2022.