Paul Makonda yupo mbugani anakula bata

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepost video fupi katika ukurasa wake wa Instagram akionyesha yupo mbugani akiwa anakula maisha.

Japo hajaeleza kuwa yupo katika mbuga ipi lakini video inaonyesha ni mazingira ya mbugani, na hajaandika chochote kuelezea video hiyo ambayo ameonekana akipata burudani ya muziki.

Wiki iliyopita Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ilitoa kibali cha kuchapisha gazetini wito wa kumuita Mahakamani Makonda na kuubandika wito huo katika Makazi yake ya Dar na Kijijini kwao Koromije.

Katika kesi hiyo, Saed Kubenea anaomba kuweza kumshtaki Paul Makonda japokuwa Makonda hajaonekana Mahakamani. Kesi, ambapo Mahakama imesogeza mbele suala hilo hadi Machi 2, 2022.

 
Hata Sabaya naye time za mwisho alikuwa anakula bata lodge
Aina ya kesi aliyonayo haina nguvu. Kubenea alipaswa kumshinikiza dpp kumfungulia jinai bashite.
 
Aina ya kesi aliyonayo haina nguvu. Kubenea alipaswa kumshinikiza dpp kumfungulia jinai bashite.

Jambo ambalo haliwezekani hata kidogo. Maana ccm ina utamaduni wao kulindana. Na huwezi kumtenganisha huyo Dpp na chama! Wote ni walewale tu. Hata Sabaya ni basi tu imetokea wakamgeuka!
 
Hapo ni tarangire kmaanina!! Huyo aliyempiga picha hakumwambia asije mjini? Akifikiria kuja mjini ataishia kisongo,hata mbauda havuki
 
na hapa yuko mbuga gani ?

 
Masikini na wenye chuki tuendelee kununa, kuvimba na hadi kupasuka. Umasikini ni mbaya sana.

Siyo kila mtu anaye mdiss Makonda, ni maskini wewe! Utuambie kwanza huo utajiri aliupata wapi? Maana miaka michache tu iliyopita alikuwa ni omba omba tu! Kiasi cha kupewa hifadhi na Mzee Samwel Sitta, JK, nk!!

Makonda ni kiburi! Lakini pia ni mjivuni. Hivyo anastahili kabisa kuchukiwa na wale alio wadharau wakati ana yale mamlaka yake ya kupewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…