Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle amesema Watu ambao wamekuwa na changamoto ya kudai kucheleweshewa kupata Pasi ya Kusafiria (Passport) wanatakiwa kufika Ofisi za Uhamiaji waelezee changamoto zao.
Amesema hayo wakati akijibu hoja za Wadau wa JamiiForums waliodai kuwa kumekuwa na ucheleweshwaji wa kutolewa kwa Passport kwa zaidi ya miezi mitatu hadi Sita huku baadhi wakidai wamekuwa wakijibiwa kuwa hakuna material ya kuchapisha Pasi mpya.
Mselle amesema “Wafike ofisini, tumesikia hizo taarifa, kuna wakati mtu anaweza kulalamika hata Passport hajaomba, anasikia kutoka kwa Mtu mwingine kuwa kuna shida fulani naya anasema tu bila kuwa na Ushahidi.”
Anaongeza “Nachelea kutoa hayo majibu wanayosema, suala la Passport ni suala tofauti kidogo, wanapofika ofisini watakutana na ufafanuzi mzuri zaidi.”
Kusoma Hoja za Wadau bofya hapa:
~ Miezi mitatu nafuatilia Passport mpya, napigwa kalenda tu, ni kweli UHAMIAJI mmeishiwa material ya kuprinti Passport mpya?
~ Upatikanaji wa Passport kwenye ofisi ya Uhamiaji pale Kibaha Mjini bado ni changamoto