Paulina ukifukuzwa uanachama CCM kimbilia Mahakamani ukazuie ubunge wako kama wale akina Mdee

Paulina ukifukuzwa uanachama CCM kimbilia Mahakamani ukazuie ubunge wako kama wale akina Mdee

Unafahamu kuna watu wameuliwa kwenye hilo sakata la akina Mdee ? kuua watu na kuingizwa chupa lipi kubwa ? Makonda ameua ( kwa mujibu wa USA ) lakini kateuliwa , hili jambo halikushangazi ?
Nani kauliwa kwenye sakata la Mdee? Acha uzushi.
 
Ukitazama hili jambo kwa jicho la tatu kwa kuangalia pongezi alizopewa Mh. Rais ni kwamba watanzania hawafurahishwi na watu wanyanyasaji kuwa madarakani au na vyeo fulani. Pauline hayuko mwenyewe,je kwa hatua hii itambidi kuwachukulia hatua na wengine wanaolalamikiwa? Tricky!
IMG_20211218_014906.jpg
 
View attachment 2826112

Huu ni ushauri ambao naupeleka kwa Ndugu Paulina Gekul, ambaye ametumbuliwa kwa ukatili dhidi ya Ubinadamu, kwamba Nchini Tanzania unaweza ukafutwa uanachama na chama chako au ukajifuta mwenyewe lakini bado ukaenda mahakamani kuupigania ubunge wako.

Halima Mdee na Wasaliti wenzie hadi leo wako bungeni pamoja na kutimuliwa kisheria na Mkutano Mkuu wa Chadema, Mwingine ni Mamluki Mwambe wa Ndanda, huyu alijiondoa mwenyewe Chadema baada ya kununuliwa na Humphrey Polepole, akajivua ubunge na kurudi kwao kulima korosho, akarudisha mpaka chumba cha Gesti aliyopanga Dodoma, lakini akaitwa na Spika wa wakati ule Job Ndugai arejee bungeni bila Chama na akarejea na kumalizia ubunge wake.

Kwahiyo tunatarajia Gekul naye apite njia hiyo hiyo.

Angalizo: Siungi mkono Unyama wake kama vile nisivyounga mkono unyama wa Makonda, bali nataka wana JF muone wenyewe jinsi Katiba ya Tanzania inavyosiginwa

View attachment 2826111
Mwenyekiti wao alisema Katiba Ni "kijitabu tu"..
Unategemea Nini!!?
 
Huyu hana refa ataliwa kichwa mapema sana.
 
Siasa zimeharibu sana jamii yetu na bongo zetu...... mitazamo ya kisiasa imefubaza bongo zetu na kuzifanya ziwaze kuelekea upande mmoja........

Kila tukio linalotokea kwenye jamii kwanza mtu kabla ya kutoa maoni anaangalia huyo mtenda Yuko upande Gani wa shilingi.......ili abishe au amponde sio kutokana kitendo alichofanya bali kwa mlengo wa kisiasa.......

Fikra huru zimekwenda na maji kutokana na chuki na uhasama wa kisiasa
 
Kina Mdee walifanya uhalifu kama huu wa Gekul? Wewe Erythrocyte ungeandika huu uzi kama mwanao angeingiziwa chupa huko nyuma? Sio kila kitu siasa mkuu... suala la kina Mdee ni la kisiasa na hili la Gekul ni jinai na hata viongozi wako wa CHADEMA wamelaani hiki kitendo alichofanya. Nchi nzima iko against Gekul. Ni wewe na wapuuzi wachache mnaotaka kuingiza siasa hapa.
Kwahiyo suala la kina Mdee sio la kisheria tena baada ya kufikishwa mahakamani?
 
CCM wanaheshimu utawala wa sheria, sio Chadema Kila siku wanamlazimisha SSH awavue ubunge akina Mdee wakati kesi iko mahakamani.

N.B: Gekul alimpa mwendazake bila hiyana, na watu wa kule wanavyopenda rangi Sasa, na yeye akawa jeuriii sababu the big boss alishafyatua. Angekuwepo, hata uwaziri asingetolewa.
 
Kina Mdee walifanya uhalifu kama huu wa Gekul? Wewe Erythrocyte ungeandika huu uzi kama mwanao angeingiziwa chupa huko nyuma? Sio kila kitu siasa mkuu... suala la kina Mdee ni la kisiasa na hili la Gekul ni jinai na hata viongozi wako wa CHADEMA wamelaani hiki kitendo alichofanya. Nchi nzima iko against Gekul. Ni wewe na wapuuzi wachache mnaotaka kuingiza siasa hapa.
Kumbe kuvuruga uchaguzi ni madai eti!!??
 
Hilo kwa CCM halipo, siku anafukuzwa na siku hiyo hiyo ubunge hana, akienda mahakamani kesi haifunguliwi kwa dosari za kisheria za hapa na pale


Cha msingi ajiondokee CCM salama kama anajipenda..
 
Kwamba kufanyika makosa kuna justify kuendelea kuvunja sheria? Hii Law school ya wapi?
 
Back
Top Bottom