Pay as you earn inafikirisha na kuumiza kichwa sana!

Pay as you earn inafikirisha na kuumiza kichwa sana!

Sijawahi kuelewa yale makato aisee..
Nilishwahi kuuliza nikaambiwa ila sikuelewaa..

Nilipewa tu mfano,
Eti Hata kama mna basic salary moja ila kama mmoja anakatwa loan board mwingne hakatwi, basi makato mtatofautiana.
fafanua zaidi hapa mkuu
 
PAYE ipo dunia nzima kuna formular ya kuipata based on your income,iko mbsli ntakuwekea hapa.
Hiyo ni mbinu mujarabu ya kurudisha oesa serikalini,ndio maanamatumizo yaserikali huwayaovyo naana pesani nsli
ya serikali sio mali yako😐🙂😐
Wewe inaazimwa ili ufanyie maendeleo kwa niaba ya serikali
 
Nimelinganisha salary slip za watu wawili tofauti, mmoja ana basic salari sh 2100000 analipa Kodi sh 412000, na mwingine basic salary sh 1100000 analipa Kodi sh 101000.

Je, Kodi hizi zina uwiano Gani na kipato chetu watumishi wa serikali?
The more educational level u have the more money u are going to be paid as employee (Salary) and the more taxes from gavo gonna take from you ipo hvyo.
 
Nimelinganisha salary slip za watu wawili tofauti, mmoja ana basic salari sh 2100000 analipa Kodi sh 412000, na mwingine basic salary sh 1100000 analipa Kodi sh 101000.

Je, Kodi hizi zina uwiano Gani na kipato chetu watumishi wa serikali?
Na walisema PAYE ni single digit halafu tazama huyu👇

1722636766422.png

Huyu alitakiwa kulipa PAYE ya 144,000 ila analipa x2 = 18%
 
Nimelinganisha salary slip za watu wawili tofauti, mmoja ana basic salari sh 2100000 analipa Kodi sh 412000, na mwingine basic salary sh 1100000 analipa Kodi sh 101000.

Je, Kodi hizi zina uwiano Gani na kipato chetu watumishi wa serikali?

Msingi wa makato ya kodi kwenye mshahara ni neno kificho PAYE=Pay as You Earn/Lipa kwa Kadri unavyopata.

Wanasiasa na viongozi wetu huwa mara nyingi wanazungumzia makato ya kiwango cha chini kabisa, ndo utasikia tumeshusha PAYE kwenda single digit (9%). Ndani yake kuna msumeno mkali sana.

Fomula/kikokotoo cha PAYE kinazingatia ukubwa wa pato lako na kuongeza ukataji ngazi kwa ngazi kwa kadri mshahara/pato lako linavyoongezeka. Hapa huwa kuna PAYE ya Tanganyika na ya Zanzibar ukiingia kwenye mfumo wa TRA utazipata. Chini hapa ni mnyumbuliko wa hii ya Tanganyika(Tanzania bara).

Tazama kiambata👇

1722651991413.png

MCHANGANUO:
1: Kama mshahara wako ni ndani ya: 270,000/=(Hukatwi kodi).

2: Kama mshahara wako ni ndani ya: 270,001-520,000/=(Utakatwa 9%).

3: Kama mshahara wako ni: 520,001-760,000/=(Ziada ya hapa itakatwa 20%). Hii itafanya jumla ya kodi kuwa (namba 2+ namba 3).

4: Kama mshahara wako ni: 760,001-1,000,000/=(Ziada ya hapa hukatwa 25%). Hivyo, makato yatakuwa ni: namba 2+namba3+namba4).

5: Ikiwa mshahara wako ni zaidi ya 1,000,000/=, ziada ya hapa itakatwa 30%. Makato yako yatakuwa ni: (namba2+namba3+namba4+namba5).
 
Back
Top Bottom