Paypal account Tanzania tunasubiri nini?

Paypal account Tanzania tunasubiri nini?

Ngoja niwaandikie Dm Mpango na nduguru , watu tunapiga Sana pesa nje Ila kuzileta bongo ndo miyeyusho alag wenyewe wamelaza matumbo Yao na mi vx
Old minded people.. Sijui kama wanajua ugumu tunaopata. Tunauza huduma kupitia mitandaoni na ili wateja wawe na hakika ya huduma zetu wanalipa kupitia mitandao husika na baadae tukisha wahudumia ndo malipo yetu huidhinishwa. Sasa lazima kuwe na njia rahisi ya kupata pesa zetu na serikali ikusanye kodi. Vinginevyo tutabaki masikini miaka yote
 
Na
Mkuu hebu tueleze, sababu kwa uelewa wangu PayPal kwa Tanzania inafanyakaz upande wa kutuma tu tena kupitia Bank.. So wew unapokea kupitia PayPal?? How!?
Nadhani ili ipokee ndo hivyo usajilie nchi nyingine
 
talentbrain,
Binafsi natumia Payoneer..... Niko na online account na ATM master Card ya Payoneer, naweza ku withdraw toka kwa ATM yoyote Inayo support Master Card Worldwide!

Kuna Uzi nilifungua muda kidogo, tembelea upate uelewa kidogo.
 
Thanks ila ungenipa link hapa ingesaidia
 
Hii nchi inatia hasira sana yaani, kuna mamtu yako so linearly hayafikirir wala kujigumza toka kwa nchi zilizoendelea..
B.O.T nimewatukana kisirisiri na viongozi wote upande Wa fedha na uchumi mabangladesh kabisa wote ni medula oblangata useless.
 
Hivi wizara ya fedha imeshaeleza kwanini huduma hii imezuiliwa Tanzania?
BOT juzi kati walisema biashara ya fedha za mtandaoni ni kinyume cha sheria, wenda hawataki kuruhusu paypal maana kwa akili zao wanaamini ni kinyume cha sheria!
 
Hii naitumia vipi kwenye malipo yanayohitaji option mbili tu za aidha PayPal au bank na kwa bank wanatoa Mara moja tu kwa mwezi?
Hiyo yenyewe no bank na unapewa na ac,so ikiingia kule wewe unatoa huku kwenye atm
 
BOT juzi kati walisema biashara ya fedha za mtandaoni ni kinyume cha sheria, wenda hawataki kuruhusu paypal maana kwa akili zao wanaamini ni kinyume cha sheria!
Mfano Mimi nauza package zangu za utalii kupitia TripAdvisor na wanapitishia malipo yao Viator ambao wanalipa kwa njia hizo mbili aidha bank au PayPal. Kosa kisheria ni lipi hapa? Kuuza huduma mtandaoni au kupokea pesa mtandaoni. Vipi utalii utakuwa kama tunataka kuuza huduma manually?
 
Hiyo yenyewe no bank na unapewa na ac,so ikiingia kule wewe unatoa huku kwenye atm
Nitafuatilia nione kama wanaweza rahisisha kazi yangu. Maana Nina account kadhaa Nazi namba zinavyotumika ni kupokea once a month
 
Hii nchi inatia hasira sana yaani, kuna mamtu yako so linearly hayafikirir wala kujigumza toka kwa nchi zilizoendelea..
B.O.T nimewatukana kisirisiri na viongozi wote upande Wa fedha na uchumi mabangladesh kabisa wote ni medula oblangata useless.
Dah, tunachelewa sana ndugu yangu.
 
Wasiwasi wangu ni kutumia laini ya MTU naweza kupoteza pesa yangu
Ni kweli risk ya kupoteza pesa ni kubwa, ila unaweza kwenda Kenya ukasajili laini kwa kutumia passport ya kusafiria ya Tanzania.
Yes utapata laini kwa jina lako
 
Ni kweli risk ya kupoteza pesa ni kubwa, ila unaweza kwenda Kenya ukasajili laini kwa kutumia passport ya kusafiria ya Tanzania.
Yes utapata laini kwa jina lako
Hiyo ndio option yenye uhakika japo laini isiyotumika kwenye kupiga na kupokea simu pia unaweza kufungwa.
 
Hiyo ndio option yenye uhakika japo laini isiyotumika kwenye kupiga na kupokea simu pia unaweza kufungwa.
Yes, option sahihi, na suala kufungiwa unaweza kuliepuka kabisa, uwe unanunua salio japo maramoja ndani ya miezi mi3, na utanunua salio kupitia mpesa yake, kama unavyonunua salio kutoka mpesa au Tigo pesa
 
Mfano Mimi nauza package zangu za utalii kupitia TripAdvisor na wanapitishia malipo yao Viator ambao wanalipa kwa njia hizo mbili aidha bank au PayPal. Kosa kisheria ni lipi hapa? Kuuza huduma mtandaoni au kupokea pesa mtandaoni. Vipi utalii utakuwa kama tunataka kuuza huduma manually?

Angalia vizuri hapo kwenye bold...

"wenda hawataki kuruhusu paypal maana kwa akili zao wanaamini ni kinyume cha sheria! "

Nadhani kwa njia nyingine unaweza kutumia line ya safaricom ku verify your account au ukatumia VPN (google tapata maelezo maana bado sijajaribu) ili uweze ku cheat location, yaani location yako itasoma uko USA kumbe uko chato! from there utaweza ku verify you account na kutumia kama kawa!!
 
Hiyo ndio option yenye uhakika japo laini isiyotumika kwenye kupiga na kupokea simu pia unaweza kufungwa.
Nna swali la ufahamu...mfano unataka kumuuzia mtalii kitu (physical good) na uko bongo na yeye yupo ulaya, je usafirishaji unakuaje? unatumia dhl au posta? kama posta delays una deal nazo vipi?
 
Back
Top Bottom