I thought i was asking from friends!
Nimenunua Gari Mara 2 via paytrade! Ni Huduma inayohakikisha kwamba hela yako haitaibiwa! Tradecarview ni kampuni na ndani Yake pana watu wameregister wanauza magari, when you use paytrade actually hela ukituma zaenda kwa trade car view na wakiridhika Gari limetumwa na ni Kama like la kwenye invoice Ndio Wana release funds kwenda kwake, ikitokea shida they refund you.
Sikumbuki kama niliwahi wauliza hili, naomba
jamani nijuzeni juu ya uhakika wa hii njia ya
kununua gari japan kwa kutumia Paytrade.
Na
ona wahusika waniongelea kama secure method je, ni kweli au ndo
mpango mzima wa kutaka kuingizana kingi?
Nijuzeni please, nataka nilisahau lile swali la
'hivi jirani kwa nini hununui gari'?.
Nawasubiria!
mkuu hii huduma ni sahihi, salama na ya uhakika zaidi. Ingawa unailipia kidogo, ni bima ya uhakika ya pesa zako. Muuzaji analipwa na paytrade meli yenye gari lako ikishaondoka bandarini kuja tz. Vinginevyo kama atakuwa hana uwezo wa ku-supply gari, paytrade watakurudishia pesa yako. Nazungumza kwa uzoefu maana nimeshawatumia mara 3.
Ofcoz using Paytrade you get guarantee of your money by the car showroom so called tradecarview.
nashukuru mkuu,kwa ushauri wako mzuri,itabidi niwatumie hawa jamaa.
Nina mpango wa kuagiza usafiri,please naombeni mnijuze kuh hili, kuagiza gari kutoka kwenye makampuni yaliyo kwenye tradecarview kupitia huduma yao ya paytrade iwapo ni njia sahihi,salama na ya uhakika ya uagizaji magari?
Watu wanataka kukutapeli kijana, hao wanaokuambia eti ni-PM kuwa nao makini. Watu tumeagiza magari, tumeyapata, mazuri kama tulivyotegemea. Usifikiri eti mtanzania mwenzio ndio mwaminifu sana kuliko wajapan!!, Paytrade haina shida, kama unahofu na ubora wa gari, tumia makampuni yenye uhakika kama vile AUTOREC japo garama zao huwa ni kubwa kidogo kuliko wengine
Kuna malalamiko mengi na wengi kupoteza fedha zao kwa njia hii. Kwani unafanya biashara na mtu usiyemjua, huna pa kuanzia kufuatia pesa zako. Wengine wanaletewa magari tofauti na waliyoyachagua. Huna hakika na ubora wa gari unayoiona kwenye picha kwa vile mfanya biashara anataka gari litoke nawe huna wa kukuhakikishia kama gari ni salama au kanyagaboya.
Nilikuwa na mpango wa kufanya hivyo, lakini nilisita kwa vile siku hizi ziwezi kuamini sana njia ya kulipa online kiwango kikubwa cha pesa kutokana na wengi kuingizwa majaribuni na kuishia kupata presha. Wenye bahati hubahatika na asiye na bahati ndo hivyo tena. Ujeavyo wauzao magari si kampuni mmoja bali na watu binafsi na makampuni mbalimbali ya car dealers.
Ushauri:
Uzoefu wangu ni bora kumtumia mtu mwaminifu mtanzania aishiye huko Japan ambaye anafanya kazi kwenye moja ya makampuni ya dealership. Kuna mmoja ambaye namfahamu mwaminifu, mwazi na atakutafutia gari unalotaka na kwa kiwango cha kuridhisha. Utaweza kuongea naye kwa simu na kuwa na mawasiliano kwa email naye kwa nini kinatakiwa, na atakupa msaada wa kufaa. Hata wamissionari wanamtumia sana mtu huyo. Mimi mwenyewe nimeagiza gari kutumia yeye alinipa ushauri mzuri, na kunipa tahadhari kwa baadhi ya magari niliyofikiria mazuri kumbe ni bomu tupu. Alinichagulia gari zuri na nilipolichukua bandarini Dar sikuamini na walioona walifikiri ni jipya kwa jinsi alivyokuwa makini katika kufanya uchaguzi makini.
Yeye anafanya dealership kwa hiyo hiyo tradecarview, lakini mimi niliweza kulipa moja kwa moja kwenye kampuni nilikonunua gari kupitia kwake na kwa gharama nafuu. Huyu Kaka namfahamu kwa miaka mingi wakati yupo Tanzania, na sasa ndio yuko Yokohama - Japan.
Anayetaka kuagiza gari kupitia kwa huyu ndugu mtanzania halisi ambaye ni mwaminifu na mcha Mungu, anipm nimpe contact zake. Siwezi kuanika tu hapa kwa vile hajaniruhusu kufanya hivyo. I'm serious, nawahurumia watanzania wenzangu, pesa yako umeitokea jasho unauchungu nayo. Thanks.
Mzee wa Busara sasa hapa unatusaidia kus-solve problem au unatuvunja moyo.
Mbona siye tumekuwa tukiagiza magari kupitia makapuni ya kuuza magari - Japan na tumekuwa tukiyapata bila matatizo - kimsingi wajapan ni watu waaminifu sana - japo kwenye kundi la mijusi nyoka hawezi kosekana.
Halafu badala ya kutuweka sawa kwenye tatizo la msingi unatutoa kwenye hukomun atupeleka kwingine ambako wewe binafsi unafikiri ni salama - je tutajuaje kama na wewe ni unatupeleka kwa mtu ambaye atatuingiza mjini.
Najua kuna makampuni mengi ya kitapeli lakini si yote tatizo ni kujua lipi - na hii inataokana na ushahidi wa awatu mbali mbali ambao wameisha watumia