Kuna malalamiko mengi na wengi kupoteza fedha zao kwa njia hii. Kwani unafanya biashara na mtu usiyemjua, huna pa kuanzia kufuatia pesa zako. Wengine wanaletewa magari tofauti na waliyoyachagua. Huna hakika na ubora wa gari unayoiona kwenye picha kwa vile mfanya biashara anataka gari litoke nawe huna wa kukuhakikishia kama gari ni salama au kanyagaboya.
Nilikuwa na mpango wa kufanya hivyo, lakini nilisita kwa vile siku hizi ziwezi kuamini sana njia ya kulipa online kiwango kikubwa cha pesa kutokana na wengi kuingizwa majaribuni na kuishia kupata presha. Wenye bahati hubahatika na asiye na bahati ndo hivyo tena. Ujeavyo wauzao magari si kampuni mmoja bali na watu binafsi na makampuni mbalimbali ya car dealers.
Ushauri:
Uzoefu wangu ni bora kumtumia mtu mwaminifu mtanzania aishiye huko Japan ambaye anafanya kazi kwenye moja ya makampuni ya dealership. Kuna mmoja ambaye namfahamu mwaminifu, mwazi na atakutafutia gari unalotaka na kwa kiwango cha kuridhisha. Utaweza kuongea naye kwa simu na kuwa na mawasiliano kwa email naye kwa nini kinatakiwa, na atakupa msaada wa kufaa. Hata wamissionari wanamtumia sana mtu huyo. Mimi mwenyewe nimeagiza gari kutumia yeye alinipa ushauri mzuri, na kunipa tahadhari kwa baadhi ya magari niliyofikiria mazuri kumbe ni bomu tupu. Alinichagulia gari zuri na nilipolichukua bandarini Dar sikuamini na walioona walifikiri ni jipya kwa jinsi alivyokuwa makini katika kufanya uchaguzi makini.
Yeye anafanya dealership kwa hiyo hiyo tradecarview, lakini mimi niliweza kulipa moja kwa moja kwenye kampuni nilikonunua gari kupitia kwake na kwa gharama nafuu. Huyu Kaka namfahamu kwa miaka mingi wakati yupo Tanzania, na sasa ndio yuko Yokohama - Japan.
Anayetaka kuagiza gari kupitia kwa huyu ndugu mtanzania halisi ambaye ni mwaminifu na mcha Mungu, anipm nimpe contact zake. Siwezi kuanika tu hapa kwa vile hajaniruhusu kufanya hivyo. I'm serious, nawahurumia watanzania wenzangu, pesa yako umeitokea jasho unauchungu nayo. Thanks.