PayTrade ya tradecarview


Hawa japanese car auction agent kuwa mwangalifu sana. Lucas nao wapo pale Mikocheni Shoppers Centre, lakini ni watafutaji zaidi kuliko kufanya biashara ya kwali ndio uswahili. Kwa walioishi bongo tu uswahili huo wameuzoea, lakini waliotoka kidogo kuonja wenzetu wanavyofanya biashara hawa wa bongo ni wachovu wa kutafuta pesa kwa mkato na kwa njia mteremko bila kuithamini biashara yao. Ninachoandika nakifahamu na nimeshuhudia watu hao. Ukijiamini ku-deal nao okay, lakini kwangu nimeshawatolea nje.

Tatizo wengi wetu hawana jinsi wala option ya kuagiza gari hivyo inabidi kuwatumia tu mradi upate gari, lakini je ni gari bora unayotazamia au mradi lina sura nzuri kwa nje wakati baada ya muda mfupi unatembea na koleo mkononi huku umeshika usukani.
 
Paytrade ni insuarance inayomilikiwa na wenye mtandao yaani tradecarview, malipo yao si chini ya usd 150 hata kama ni kama unanua gar la cif 200 , ni wazur sana coz unakuwa huna bp, utapeli ulizidi ndo maana wakaanzisha paytrade
 
Tutakuaminije? We bwana acha wizi!

Nimeshazungumza mimi sifanyi biashara ya kuagiza magari ya watu. Nilichofanya kuwasaidia wengine njia ambayo mie nimetumia ambayo haijaniumiza kichwa na nimeridhika nayo. Vinginevyo unaweza kuwatumia Lucas wa Mikochoni ambao wapo tradecarview utalipa pesa pale na utachagua gari online pamoja nao watakusaidia kkulipata haraka na kwa ufanisi, lakini tatizo la ubora litabaki palepale kwa vile tunaangalia picha ya gari bila ukaguzi wa ubora.
 
Paytrade ni insuarance inayomilikiwa na wenye mtandao yaani tradecarview, malipo yao si chini ya usd 150 hata kama ni kama unanua gar la cif 200 , ni wazur sana coz unakuwa huna bp, utapeli ulizidi ndo maana wakaanzisha paytrade

Hapa jamii forums na watanzania kwa vile tumezoea kutapeliana wanafikiri kila mwenye kutoa maoni na mapendekezo mazuri ni kutaka kupata kitu au kutapeli. Sory for that.
 
Acha kuwatisha wenzako,Paytrade is guarnteed.Kuwatumia watanzania ni sawa lakini nimekuja gundua wengi waTz nao wa huko wanaongeza sana cha juu,kwani wengi hulipwa commission na washikaji wanaowapelekea wateja.......for instance niliwahi kuwa na jamaa mmoja tunabrowse hii trade car view website kila kampuni alikuwa anaitoa kasoro,mwisho wa siku akataka anilengeshe kwa mshkaji wake,at the end through my patience and searching nikapata gari usd1500 cheaper tofauti na mshkaji wake wa huko Japan aliyeniunganishia.......sometimes dealing straight na credible companies is better than hawa ndg zetu WaTz walio huko,kwani zimwi likujualo.........:coffee:


 

Mimi siishi Japan, na sina nia ya kumtafutia mtu wateja, ila hapa kila kinachowezekana kizuri kusaidiana ni jambo zuri na ndivyo nilivyofanya.

Sina nia ya kumtisha mtu, nilichosema kimetokea ni kweli, kama we umebahatika hivyo si kila mmoja atabahatika. Kumbuka mfanya biashara ni mfanyabiashara tu, anachotaka mali aliyo nayo iuzike na kesho alete nyingine.

Magari yaliyotumika huuzwa 'AS IS" maana yake lolote litakalotokea kama gari ni mbovu mwuzaji hahusiki, ndio maana ya kusema unaweza pata gari zuri au kanyagaboya. Ukweli tuuweke wazi tusiufunike halafu wenzetu wapate hasara ka kila walichotaabikia kwa miaka.

Gari zuri ni lile ambalo mtu mwenye uzoefu analikagua katika mambo ya msingi ya kawaida kuona kama linafaa na linaweza kufanya kazi muda mrefu au la. Huo ndio ukweli wenyewe. Thanks kwa kunielewa, na asiye nielewa ni haki yake. Hapa ni kuelimishana.
 
Hapa jamii forums na watanzania kwa vile tumezoea kutapeliana wanafikiri kila mwenye kutoa maoni na mapendekezo mazuri ni kutaka kupata kitu au kutapeli. Sory for that.

Taratibu baba - mfumo wa kijanja wa nchi umetuaharibu akili hata jambo genuine lazima tuhoji - kwa hoja hii haijalishi unatoa mapendekezo mazuri au vipi lazima machale yatucheze tu
 
sasa sikia usiangaike mie nimeshaagiza mara mbili kwenye hiyo site......kuna jamaa anaitwa patrick ni wakala wa tradecarview Tanzania, ofisi zao zipo pale opposite na shule ya mbezi beach secondary, mitaa ya tangibovu........for more details utanambia
 


Tatizo linabaki pale pale, maana gari haichunguzwi ubora, unachoweza kufanya pamoja na huyo Patric ni kubrowse mtandaoni na kuchagua mvuto wa gari bila kujua undani wa gari kama litakufaa kwa muda gari.

Tofauti na kumtumia mtu ambaye atalichunguza gari na kukuhakikishia ubora. Haya magari ya "as is" baada ya kutumia pesa nyingi za kulikomboa bandarini utaishia kuliweka juu ya mawe baada ya muda mfupi, kwani wengi wetu Tanzania hatuna uzoefu na ubora wa magari, tunavutiwa na mtindo, mwundo na rangi bila kuangalia ubora.

Nchi zilizoendelea gari huzeeka injini na transmisheni, lakini bodi lake linaonekana lenye mvuto kutokana na kuwa na kiwango cha barabara zote kuwa cha hali ya juu kisichochakaza body la gari.
 
maneno mengi hayavunji mfupa njoo tufanye biashara .chunga pesa na upate unachohitaji kwa ubora unaotaka ,wakati muafaka .arusha no maneno mengi lipa deposit kazi inaanza haraka sana .jaribu leo japanese car auction agent arusha
 
ukishaliwa hela zako uje na karatasi tutakusaidia kuwatafuta hawa jamaa kule japan ila kumbuka hawana ofisi kule ofisi iko kwenye laptop komputa mpakato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…