Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Wasiliana na japanese car auction agent wapo arusha wanadili na minada moja kwa moja ni guarantee kupata gari watumie email yako utatumiwa gari unayotaka na kiwango cha pesa unachotaka .gari japan huuzwa kwa njia za minada kwa kupitia kwenye computer zilizounganishwa moja kwa moja ,minada huanza jumatatu hadi jumamosi .kumbuka huwezi ka access hapa hadi uwe member .
Hawa japanese car auction agent kuwa mwangalifu sana. Lucas nao wapo pale Mikocheni Shoppers Centre, lakini ni watafutaji zaidi kuliko kufanya biashara ya kwali ndio uswahili. Kwa walioishi bongo tu uswahili huo wameuzoea, lakini waliotoka kidogo kuonja wenzetu wanavyofanya biashara hawa wa bongo ni wachovu wa kutafuta pesa kwa mkato na kwa njia mteremko bila kuithamini biashara yao. Ninachoandika nakifahamu na nimeshuhudia watu hao. Ukijiamini ku-deal nao okay, lakini kwangu nimeshawatolea nje.
Tatizo wengi wetu hawana jinsi wala option ya kuagiza gari hivyo inabidi kuwatumia tu mradi upate gari, lakini je ni gari bora unayotazamia au mradi lina sura nzuri kwa nje wakati baada ya muda mfupi unatembea na koleo mkononi huku umeshika usukani.