Paza sauti, taja taasisi za umma/serikali ambazo zinapaswa kufutwa, kubinafsishwa au kuunganishwa. Jana serikali imethubutu, lakini bado uchafu upo

"Asilimia 60 ya watendaji wa serikali uwezo wao ni mdogo sana kiutendaji." — Profesa Mussa Assad
It has to do with control and that is role of senior management, kila mwaka report ya CAG inaonesha weak spots.

Hao wenye hizo nafasi hawafanyi lolote kuzuia hiyo mianya, hao wanaotakiwa kupendekeza majina ya watu wanaofaa hawana uwezo wa kufanya vetting sahihi na huyo anaetua hana muda wa kujiridhisha majina anayopewa.

Don’t stress yourself in banana republic politics.
 
Vyama vyote vya siasa vifutwe nchi ibaki bila chama.
 
GPSA na NEST iwe Taasisi moja.

MSL ,TPA na TASAC iwe Taasisi moja na vitengo vingi .

TCAA na TAA iwe Taasisi moja.

TARURA na TANROAD iwe ni taasisi moja na vitengo lukuki .

TMDA na NIMR iwe Taasisi moja.

TRC na TAZARA iwe Taasisi moja na vitengo kibao.

USHAURI: Wanapofuta na ku'merge izo taasisi zinatakiwa zile na title za kudili na shughuli katika ngazi ya taifa ....
Mfano title NATIONAL ROAD CONSTRUCTION AND MAINTENANCE.
 
Kwangu hata bunge ,mahakama ,na jeshi la polisi achana na vi-taasisi uchwana kama TANESCO sijui Tan-road

USSR
TANROADS + TARURA
Hizi nazo zilipaswa kuunganishwa. Hakukua na sababu ya kuanzisha TARURA kwa jambo ambalo TANROADS wanalifanya.

Kodi ya majengo ilihamishwa kukusanywa na halmashauri na ikaanza kukusanywa na TRA na sasa inakusanywa na TANESCO. Hakuna ofisi mpya iliyoanzishwa, vivyo hivyo, barabara za miji na vijiji zingetolewa chini ya usimamizi wa halmashauri na kupelekwa TANROADS lakini sio kuanzisha TARURA. Ni kupeana vyeo tu na mzigo wa kodi kulipa mishahara isiyo ya lazima.
 
sasa mnaotaka mashirika yavunjwe na kuungwa mmejiuliza watoto wenu wanaajiriwa wapi kesho?
 
When it comes to strategic planning decision.

It’s either an internal team doing the work or you hire a specialised team (consultants) even them you must provide them with the data.

Kuunda team ya watu wa nje kuandika dira ya taifa ni ujinga tu wa Tanzania.

For god sake it’s not even easier to form teams out of the blue why do you think people like ‘Meredith Belbin’ theories are important in team theories or management theories are concerned with inter proffesional working.

Hao wapuuzi watakutana na mwisho wa siku nchi itapata report ya upuuzi tu.

You have to understand the process or prior thinking on how things are done kuona upuuzi wa hawa watu.

Shida ni kwamba asilimia kubwa ya viongozi wetu uwezo wowote ndio maana nchi ni maskini; hakuna kingine.
 
Kitila kapiga porojo bungeni kuhusu dipiwedi kapewa nafasi ya uwaziri wa sector ya (uchumi/biashara) japo hana uwezo nayo.
Ila kwa Kitila na wenzake, tatizo ni katiba yetu. Tumesema waziri ni lazima awe mbunge, na mbunge ni mtu yoyote aliyegombea anayejua kusoma na kuandika na awe na miaka 21+, kwa hiyo ni ngumu sana kukwepa kupata watu wajinga wanaojali pesa kwa nafasi hizo za ubunge na uwaziri.

Tungeweza kwa kupunguza mishahara ya wabunge iwe kama ya wakuu wa idara za serikali (halmashauri), tungepata wabunge na mawaziri wenye dhati ya kutumikia wananchi.
 
Mahakama+Polisi+Magereza ziunganishwe, wizara ya kitila mkumbo ifutwe, ipelekwe Sanaa na michezo
 
sasa mnaotaka mashirika yavunjwe na kuungwa mmejiuliza watoto wenu wanaajiriwa wapi kesho?
Kwenye hayo mashirika yaliyounganishwa.

Tunaondoa mabosi na wakuu wa idara wanaokula fedha nyingi pasipo ufanisi, ila idadi ya wafanyakazi wa chibi itakuwa namba ileile.
 
Wala usiwe na hofu, ccm miaka nenda rudi inaongoza nchi huku ikiwa na watu wenye uwezo mkubwa marekani,nchi za ulaya zenyewe zinasubiri
Ondoa shaka subiriaa tu ule neema

Ova
 
@FaizaFoxy anawashangilia sana dipiwodi mbona na anasema bandari
Sahv kuko vizuri

Ova
 
Hapo kwa (nida na Rita) wasiishie ku-unganisha tuu ingekuwa vyema kama wangebinafsisha kabisa ili kuongeza ufanisi .
 
Tanesko itafutiwe muwekezaji mwenye akili timamu aiendeshe au ikiwezekana ziruhusiwe kampuni binafsi za nje ya nchi zilete ushindi kwa tanesko labda watajirekebisha
 
Taasisi zote zimetushinda hata ile taasisi kubwa kabisa inayoongoza na kutawala taasisi zote na watu wake.

Kwangu mimi, tunahitaji kutawaliwa tena miaka mingi sana na viboko juu. Somo la utawala limetushinda kabisa.
 
Constitutionally nchi inaongozwa na chama cha siasa kilichopata ridhaa ya wananchi.

Technically nchi inaongozwa na civil servants (hawa ndio technocrats).

Wanasiasa wakishinda uchaguzi wanaingia madarakani na ilani yao (ni jukumu la civil servants kupanga hiyo ilani strategically inatekelezeka vipi).

Ndio maana makatibu wakuu wanatakiwa kuwa na level five of management competence (long story kuelezea what it implies) na maafisa usalama (hizo nafasi sio za kila mtu) matter of fact mkurugenzi wa wizara na sectary wa wazuri huwa ni wanaokula viapo usalama.

Sasa hadi kufikia hizo nafasi kuna mlolongo mrefu wa merit za performance on skills requirements to hold those posts. Na katibu mkuu amongst their criteria ni level five of management skills (ability to devise a strategy plan ya wizara) stragey plan ina mambo mengi na inahusisha wataalamu wengi, data nyingi, mipango pamoja na ilani ya chama husika; jumlisha na dira ya nchi ya muda mrefu kutoka usalama wa taifa.

Kuelezea mambo yote ya nchi inavyoendesha ni hadithi ndefu na raia kujua wajibu.

Sasa ukisoma JF hata wafanya biashara wenye mafanikio concept ya kodi hawajui kweli tuanze kuangaika na changamoto za kujadili changamoto za kuendesha nchi which are very complicated matters.

Tupo hapa tulipo kwa sababu tunaongozwa na watu wasio na uwezo.
 
Hapo kwa (nida na Rita) wasiishie ku-unganisha tuu ingekuwa vyema kama wangebinafsisha kabisa ili kuongeza ufanisi .
Wasilipe wafanyakazi mishahara. Wafanyakazi walipwe kamisheni kwa kazi wanazofanya.

Mtu ahesabiwe idadi ya vitambulisho alivyovizalisha kwa mwezi ndio alipwe kamisheni yake. Huu ujinga wa kulipana mishahara unafanya watu warelax, wasifanye kazi maana mwisho wa mwezi watakinga tu
 
Hii nimeielewa lakini pia wapunguze ubabaishaji
 
@FaizaFoxy anawashangilia sana dipiwodi mbona na anasema bandari
Sahv kuko vizuri

Ova
Huyo Ajuza anasumbuliwa na udini ukishamzoea, rarely she applies logic in her reasoning.

Sio mtu kukunyima usingizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…