PC Emanuel Keralyo Waitara, mmoja wa askari aliyeuawa na Hamza

PC Emanuel Keralyo Waitara, mmoja wa askari aliyeuawa na Hamza

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
822
Reaction score
2,095
Anaandika Christopher Cyrilo.
___

PC Emanuel Keralyo Waitara. Amezaliwa 24/12/1991, Kabila Mkurya. Ni askari wa kikosi cha FFU aliyeuawa kwa kushambuliwa na Bw. Hamza kwa kushtukiza.

Kabla ya tukio hilo, Hamza alionekana maeneo ya ufukweni akiwa na mawazo sana. Hata watu waliomsalimia hakuwajibu, ni kama vile alikuwa kwenye dunia yake tofauti. Labda alishaona dunia si mahali salama tena kwake.

Punde, akatoka ufukweni na kurudi uelekeo wa barabara kuu ya Ali Hassan Mwinyi. Akafika kwenye kibanda cha polisi kilichokuwa pembeni ya barabara, akachomoa bastola yake ndogo kutoka kiunoni, akawapiga risasi askari wawili waliokuwemo. Askari mmoja alikufa papo hapo, mwingine alikimbia kuelekea baharini.

Hamza alimvua silaha askari aliyekufa na kuivaa shingoni. Kisha akamfuata askari aliyekimbilia baharini ambaye alikuwa ameishiwa nguvu kutokana na jeraha la risasi. Akampiga risasi nyingine kummalizia kisha akachukua bunduki yake. Hapo akawa na bunduki mbili alizopora baada ya kuwaua Polisi.

Hamza akarudi barabarani na kuanza kuwatafuta askari wengine ili awaue. Alifanikiwa kumuona askari wa barabarani (trafic), akiongoza magari eneo la makutano ya barabara karibu na ubalozi wa Ufaransa. Akamfyatulia risasi na kumuua. Akayapita magari binafsi na daladala za abiria akitafuta askari wengine.

Akamuona askari wa kampuni binafsi ya ulinzi ya SGA, wanaolinda ofisi za Ubalozi wa Ufaransa. Yule askari akataka kukoki silaha kupambana na Hamza lakini akachelewa. Hamza akamuwahi, akampiga risasi na kumuua. Kisha akasogea eneo la ubalozini kupambana na askari wengine waliokuwepo. Lakini polisi wengine wakawa wamefika na katikati ya mapambano wakamuua.

Moja kati ya askari waliouawa na Hamza ni PC Emanuel Keralyo (pichani). Anatajwa kuwa mtu mwema asiye na shida na mtu. Anazungumzwa vizuri na askari wenzie hadi na jamaa waliosoma na kukua nae. Kijana mtulivu, mwenye kumheshimu kila mtu.

Zipo taarifa kuwa Hamza alidhulumiwa madini na askari. Lakini inadaiwa askari waliouawa sio wale waliomdhulumu. Kama ni hivyo, basi dhuluma ya askari wachache wasio waadilifu imegharimu maisha ya askari wasio na hatia. Mungu awapumzishe kwa amani!

FB_IMG_1629994673109.jpg

PIA SOMA:

- Kinondoni, Dar: Mtu asiyejulikana, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi
 
Yaani mtu una silaha, umejeruhiwa unakimbilia ufukweni, huo muda anamvua askari mwingine silaha we unakimbia, anakufuata ulipokimbilia anakufyatulia risasi, anachukua tena silaha yako.

Hii habari kama haijapikwa, basi kama ni kweli ni uzembe wa huyo askari aliyekimbia, wadau wanasema kaacha dona kizembe sana.

Hizo nguvu za kukimbia ni bora angejihami, mbinu bora ya kujilinda ni kushambulia any way RIP wazee, acheni tamaa.
 
Yaani mtu una silaha, umejeruhiwa unakimbilia ufukweni, huo muda anamvua askari mwingine silaha we unakimbia, anakufuata ulipokimbilia anakufyatulia risasi, anachukua tena silaha yako.

Hii kama sio chai, basi kama ni kweli ni uzembe wa huyo askari aliyekimbia wadau wanasema kaacha dona kizembe sana.

"Hii nchi kila kitu hewa. Shahidi hewa, mashitaka hewa, habari hewa ... nk" -- Jiwe kwenye ubora wake.
 
Back
Top Bottom