PC Emanuel Keralyo Waitara, mmoja wa askari aliyeuawa na Hamza

PC Emanuel Keralyo Waitara, mmoja wa askari aliyeuawa na Hamza

Mkuu jana wametoka kumpiga dereva wangu wa daladala hapo banana bila sababu, eti wana haraka kwanini anasabisha foleni, walivyojibiwa kuna ajali, kuna gar zimepigana pasi, ndo wanashangaa wakati wameshamuumiza mkono hadi umevimba balalaa na kidonda juu. Wanatumia nguvu nyingi, akili kidogo
Hawa polisi wanajiona kama wamefika, kuna mmoja alinifanyia mambo fulani ya hovyo sana halafu siku moja akaniomba zawadi za nilikotoka, nikampa soda za takeaway katoni moja, akaanza kuzinywa palepale tena kwa ulafi. Imagine ningeamua kumwekea sumu siku nyingine si angekufa
 
Hivi kuna justification gan ya kusema huyo jamaa alidhulumiwa na polisi? Na kama alidhulumiwa ndio ajichukulia sheria mkononi? Personally naamin yule jamaa ni jangiri tu wala sio muuza madin. Mnataka kuwaonea polisi bure
 
Gaidi wa kwenye keyboard, nyumbu mkubwa wewe
Shida ya polisi wetu wameshindwa kufanya majukumu yao wako busy na CHADEMA.

Mbowe gaidi, tangu lini? CHADEMA wakifanya mkutano kidogo tu polisi wameshafika.

Fanya zoezi dogo tu
Chukua watu 6 wavae tshirt za CHADEMA halafu watembee kwa pamoja. Uone kama hawajakamatwa.

Chukua watu 6 tena wavae T-shirt za CCM uone kama watakamatwa.
Polisi badala walinde sheria wao ndiyo wanavunja sheria.
 
Ivi kuna justification gani ya kusema huyo jamaa alidhulumiwa na polisi ? Na kama alidhulumiwa ndio ajichukulia sheria mkononi ? Personally naamini yule jamaa ni jangiri tu wala sio muuza madini. Mnataka kuwaonea polisi bure
Haujawahi kupitia kwenye mateso na kadhia za polisi. Ukishapitia kwenye kadhia ya hawa watu, kama unaroho nyepesi lazima uwe kama Hamza tu.

Ujiulize, kwanini hakuua raia wakati walikuwa wengi?

Kesho sikiliza kipindi cha Leo tena Clouds.

Mtu unafungwa miaka 10 halafu unabainika hauna hatia. Huo muda nani anaufidia?

Siyo huyo tu yupo mwingine naye alisingiziwa ameua, amekaa jera zaidi ya miaka 10 akaachiwa huru. Huo muda nani anafidia?

Uchunguzi gani unafanyika zaidi ya miaka 10?
 
Yaani mtu una silaha, umejeruhiwa unakimbilia ufukweni, huo muda anamvua askari mwingine silaha we unakimbia, anakufuata ulipokimbilia anakufyatulia risasi, anachukua tena silaha yako...

Hii habari kama haijapikwa... basi kama ni kweli... ni uzembe wa huyo askari aliyekimbia.... wadau wanasema kaacha dona kizembe sana....

Hizo nguvu za kukimbia ni bora angejihami, mbinu bora ya kujilinda ni kushambulia... any way RIP wazee, acheni tamaa...
Askari wa bongo waoga sana, basi tu wanajua kuonea raia..
Pili niliona hata ulengaji wao wa shabaha ni wa mashaka sana.. jamaa alitoka wazi kweupe kabisa bila kizuizi ila ilichukua zaidi ya dakika mbili kwa risasi za askari kumpata, na milio iliyosikika ni zaidi ya risasi 50 zilipotea.
 
Yaani mtu una silaha, umejeruhiwa unakimbilia ufukweni, huo muda anamvua askari mwingine silaha we unakimbia, anakufuata ulipokimbilia anakufyatulia risasi, anachukua tena silaha yako...

Hii habari kama haijapikwa... basi kama ni kweli... ni uzembe wa huyo askari aliyekimbia.... wadau wanasema kaacha dona kizembe sana....

Hizo nguvu za kukimbia ni bora angejihami, mbinu bora ya kujilinda ni kushambulia... any way RIP wazee, acheni tamaa...
Wamezoea kuwadaka kina Zitto wasio na silaha, sasa wamekutana na kidume kikawapa tuition kidogo
 
Kajificha kichwa tu, huku mata..ko na mkvndv wake viko nje. We mwache baada ya siku 3 hutomuona tena hapa jukwaani na haitohitajika mtu yoyote kuuliza kuhusu kupotea kwake.
Aah! Mfia nchi mmoja.
 
Anaandika Christopher Cyrilo.
___
PC Emanuel Keralyo Waitara. Amezaliwa 24/12/1991, Kabila Mkurya. Ni askari wa kikosi cha FFU aliyeuawa kwa kushambuliwa na Bw.Hamza kwa kushtukiza.

Kabla ya tukio hilo, Hamza alionekana maeneo ya ufukweni akiwa na mawazo sana. Hata watu waliomsalimia hakuwajibu, ni kama vile alikuwa kwenye dunia yake tofauti. Labda alishaona dunia si mahali salama tena kwake.

Punde, akatoka ufukweni na kurudi uelekeo wa barabara kuu ya Ali Hassan Mwinyi. Akafika kwenye kibanda cha polisi kilichokuwa pembeni ya barabara, akachomoa bastola yake ndogo kutoka kiunoni, akawapiga risasi askari wawili waliokuwemo. Askari mmoja alikufa papo hapo, mwingine alikimbia kuelekea baharini.

Hamza alimvua silaha askari aliyekufa na kuivaa shingoni. Kisha akamfuata askari aliyekimbilia baharini ambaye alikuwa ameishiwa nguvu kutokana na jeraha la risasi. Akampiga risasi nyingine kummalizia kisha akachukua bunduki yake. Hapo akawa na bunduki mbili alizopora baada ya kuwaua Polisi.

Hamza akarudi barabarani na kuanza kuwatafuta askari wengine ili awaue. Alifanikiwa kumuona askari wa barabarani (trafic), akiongoza magari eneo la makutano ya barabara karibu na ubalozi wa Ufaransa. Akamfyatulia risasi na kumuua. Akayapita magari binafsi na daladala za abiria akitafuta askari wengine.

Akamuona askari wa kampuni binafsi ya ulinzi ya SGA, wanaolinda ofisi za Ubalozi wa Ufaransa. Yule askari akataka kukoki silaha kupambana na Hanza lakini akachelewa. Hamza akamuwahi, akampiga risasi na kumuua. Kisha akasogea eneo la ubalozini kupambana na askari wengine waliokuwepo. Lakini polisi wengine wakawa wamefika na katikati ya mapambano wakamuua.

Moja kati ya askari waliouawa na Hamza ni PC Emanuel Keralyo (pichani). Anatajwa kuwa mtu mwema asiye na shida na mtu. Anazungumzwa vizuri na askari wenzie hadi na jamaa waliosoma na kukua nae. Kijana mtulivu, mwenye kumheshimu kila mtu.

Zipo taarifa kuwa Hamza alidhulumiwa madini na askari. Lakini inadaiwa askari waliouawa sio wale waliomdhulumu. Kama ni hivyo, basi dhuluma ya askari wachache wasio waadilifu imegharimu maisha ya askari wasio na hatia. Mungu awapumzishe kwa amani.!View attachment 1909791
🤣🤣🤣👆👆👆 Mnatengeza scenario ya kumfanya Hamza innocent, pumbavu kabisa
 
Back
Top Bottom