PC Emanuel Keralyo Waitara, mmoja wa askari aliyeuawa na Hamza

PC Emanuel Keralyo Waitara, mmoja wa askari aliyeuawa na Hamza

Acheni kutetea uovu!

Kuweni waungwana!

Mauaji siyo jambo la kushabikia hata kidogo!

RIP policemen
 
Kimsingi hakuna sababu yoyote inayohalalisha mauaji/majeruhi na taharuki hasa kwa wasiohusika.

Tuache uchunguzi ufanyike. Tuamini haki ya mtu hapotei, japo mhusika amepoteza maisha.

Kwa mfuatiliaji mzuri wa Media, matukio ya aina hii yapo kwa wingi katika nchi zilizoendelea. Mfano, Brazil sio eneo la vita lakini inaongoza kwa mauaji ya vurugu za silaha (gun violance deaths) ikifuatiwa na USA..."Through the first five months of 2021, gunfire killed more than 8,100 people in the United States, about 54 lives lost per day, according to a Washington Post analysis of data from the Gun Violence Archive, a nonprofit research organization. That’s 14 more deaths per day than the average toll during the same period of the previous six years".

Wito kwa mamlaka husika, ipo haja ya kufanyika uchunguzi wa kina kwa wanaoomba kumiliki silaha.
 
Kimsingi hakuna sababu yoyote inayohalalisha mauaji/majeruhi na taharuki hasa kwa wasiohusika.

Tuache uchunguzi ufanyike. Tuamini haki ya mtu hapotei, japo mhusika amepoteza maisha.

Kwa mfuatiliaji mzuri wa Media, matukio ya aina hii yapo kwa wingi katika nchi zilizoendelea. Mfano, Brazil sio eneo la vita lakini inaongoza kwa mauaji ya vurugu za silaha (gun violance deaths) ikifuatiwa na USA..."Through the first five months of 2021, gunfire killed more than 8,100 people in the United States, about 54 lives lost per day, according to a Washington Post analysis of data from the Gun Violence Archive, a nonprofit research organization. That’s 14 more deaths per day than the average toll during the same period of the previous six years".

Wito kwa mamlaka husika, ipo haja ya kufanyika uchunguzi wa kina kwa wanaoomba kumiliki
Huko hakufai kabisa
Mambo ya kuuana kawaida tu

Ova
 
Shujaa wa kweli lala salama

2897435_IMG-20210825-WA0023.jpg
 
Polisi ni polisi tu, hata akiwa ndugu yako sio mtu mzuri huyo, wamejaa dhulma na uonevu.

Apumzike kwa amani shujaa wetu Hamza, tuliobaki tutaendelea kuwapukutisha polisi mdogomdogo.
Kuna mmoja alikuwa anawaponda polisi kama wewe, leo nimemkuta na mabarua ya kuomba kazi ya polisi ! Machadema bana!!
 
Anaandika Christopher Cyrilo.
___
PC Emanuel Keralyo Waitara. Amezaliwa 24/12/1991, Kabila Mkurya. Ni askari wa kikosi cha FFU aliyeuawa kwa kushambuliwa na Bw.Hamza kwa kushtukiza.

Kabla ya tukio hilo, Hamza alionekana maeneo ya ufukweni akiwa na mawazo sana. Hata watu waliomsalimia hakuwajibu, ni kama vile alikuwa kwenye dunia yake tofauti. Labda alishaona dunia si mahali salama tena kwake.

Punde, akatoka ufukweni na kurudi uelekeo wa barabara kuu ya Ali Hassan Mwinyi. Akafika kwenye kibanda cha polisi kilichokuwa pembeni ya barabara, akachomoa bastola yake ndogo kutoka kiunoni, akawapiga risasi askari wawili waliokuwemo. Askari mmoja alikufa papo hapo, mwingine alikimbia kuelekea baharini.

Hamza alimvua silaha askari aliyekufa na kuivaa shingoni. Kisha akamfuata askari aliyekimbilia baharini ambaye alikuwa ameishiwa nguvu kutokana na jeraha la risasi. Akampiga risasi nyingine kummalizia kisha akachukua bunduki yake. Hapo akawa na bunduki mbili alizopora baada ya kuwaua Polisi.

Hamza akarudi barabarani na kuanza kuwatafuta askari wengine ili awaue. Alifanikiwa kumuona askari wa barabarani (trafic), akiongoza magari eneo la makutano ya barabara karibu na ubalozi wa Ufaransa. Akamfyatulia risasi na kumuua. Akayapita magari binafsi na daladala za abiria akitafuta askari wengine.

Akamuona askari wa kampuni binafsi ya ulinzi ya SGA, wanaolinda ofisi za Ubalozi wa Ufaransa. Yule askari akataka kukoki silaha kupambana na Hanza lakini akachelewa. Hamza akamuwahi, akampiga risasi na kumuua. Kisha akasogea eneo la ubalozini kupambana na askari wengine waliokuwepo. Lakini polisi wengine wakawa wamefika na katikati ya mapambano wakamuua.

Moja kati ya askari waliouawa na Hamza ni PC Emanuel Keralyo (pichani). Anatajwa kuwa mtu mwema asiye na shida na mtu. Anazungumzwa vizuri na askari wenzie hadi na jamaa waliosoma na kukua nae. Kijana mtulivu, mwenye kumheshimu kila mtu.

Zipo taarifa kuwa Hamza alidhulumiwa madini na askari. Lakini inadaiwa askari waliouawa sio wale waliomdhulumu. Kama ni hivyo, basi dhuluma ya askari wachache wasio waadilifu imegharimu maisha ya askari wasio na hatia. Mungu awapumzishe kwa amani.!View attachment 1909791
So smart
 
Huyu jamaa kwanza sikufikiria kua na police wala kuja kua police, alimaliza kidato cha sita Rungwe High School Tukuyu-Mbeya (pia nmesoma apo)nadhani 2013 kijana mpole sana, msikivu na pia alikua kiongozi, kwa kweli hakustahili kufa na nmeumia mnoo, sidhani kama alihusika kwenye iyo dhulma!so sad for sure R.I.P mate 😭😭
 
Kwahiyo ulitaka polisi wamzungumzie vibaya polisi mwenzao?
Hawa polisi wetu wengi wameshindwa kutumia kidogo chao kuzalisha kikubwa kwa kufanya biashara, ufugaji au kilimo badala yake wanaamua kuishi kwa kudhulumu matajiri na maskini

Kweli kabisa
 
Askari wa bongo waoga sana, basi tu wanajua kuonea raia..
Pili niliona hata ulengaji wao wa shabaha ni wa mashaka sana.. jamaa alitoka wazi kweupe kabisa bila kizuizi ila ilichukua zaidi ya dakika mbili kwa risasi za askari kumpata, na milio iliyosikika ni zaidi ya risasi 50 zilipotea.
Ni basi tu, kuna muda inabidi tuwaheshimu... lakini hawajiheshimu...
 
Back
Top Bottom