Pelekeni watoto Hospitali, msiwafunge hirizi –DC Tanga

Pelekeni watoto Hospitali, msiwafunge hirizi –DC Tanga

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa, amewataka wazazi kuwapeleka hospitali watoto wanaozaliwa wakiwa na changamoto kama vile kuwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi badala ya kuishia kuwafunga hirizi na kubaki nao nyumbani.

"Kuna wakati unaona mtoto kazaliwa akiwa na changamoto tamaduni zetu baadhi yao unakuta mtoto badala ya kupelekwa hospitali amekimbizwa kufungwa mahirizi miguuni na shingo tuondokane na hizo dhana badala yake tuwapeleke watoto hospitali ili wapatiwe matibabu” amesema DC huyo.

Mgandilwa amesema hayo jijini Tanga katika maadhimisho ya siku ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Kiwilaya, ambapo kitaifa yafanyika kesho Oktoba 25, mwaka huu.

Chanzo: Nipashe
 
Tukiwapiga sachi kila mmoja ana hirizi kiunoni😂🤣🤣🤣, kweli kabisa tuachane na huu ushenzi
 
Back
Top Bottom