A
Anonymous
Guest
Hivi karibuni Wabunge wa Zanzibar ambao wanawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano walijichanga na kutaka kutoa zawadi kwa Wananchi wa Pemba, ambapo waliandaa nyama.
Nyama hiyo iliingizwa Pemba kupitia Bandari ya Wete, haijulikani nini kilitokea, ilichelewa au ilikwama au ni yenyewe tu haikuwa na ubora, kwani baada ya ukaguzi wa Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) ikabainika haifai kuliwa.
Hivyo, ZFDA wakakubaliana iteketezwe, hawakusema wazi kuwa nyama ina tatizo gani, lakini wakati wakukubaliana likajitokeza kundi la watu na kuamua kuichukua sehemu ya nyama husika na kuondoka nayo.
Wapo waliochukua kwa lengo la kwenda kula wao na familia zao na wapo ambao wamechukua hatujui wanaenda kuwapa mifugo au wanaingiza kwenye mzunguko wa nyaka buchani.
Hii ni hatari, kwani kama nyama hiyo ina madhara au ina vimelea ambavyo vinaweza kuwa hatari kwa afya hilo ni jambo baya na ni hatari kwa Wananchi wote.
Viongozi wa Jimbo la Ole, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini, ZFDA, Mamlaka zinazoshughulikia Mifuko na hata hao Wabunge waliotoa msaada wote wapo kimya, hakuna aliyejitokeza hadharani kutoa tahadhari, mfano vipi kama nyama hiyo ina magonjwa ya mlipuko?
Ufafanuzi soma ~ Mbunge wa Jimbo la Ole, Pemba asema nyama iliyoteketezwa ilikaa muda mrefu baharini ikaharibika