Salamu kwa wanaJF.
Nina pendekezo la namna ya kumuenzi Hayati Rais John Pombe Magufuli tukizingatia huduma aliyoitoa katika kuendeleza miundombinu nchini Tanzania.
Ni vyema ukaanzishwa mfuko wa uchangiaji fedha ambazo zitagharamia ujenzi wa miundombinu mbalimbali haswa ya Madarasa,Vituo vya Afya na barabara.
Wapenzi na wafuasi wa kazi na falsafa za Magufuli waweze kuchangia katika mfuko huo.
Michango ya kuonesha soliderity iende huku.
Fedha za mfuko huo zitumike kuboresha miundombinu ya huduma.
Naomba kuwasilisha kwa unyenyekevu.
Kama walivyofanya Kikwete na Mkapa naye Magufuli anatakiwa awe na Mungufuli foundation ambayo ndiyo itaamua kitu gani na mradi gani wafanye. Hii sio shughuli ya serikali kufanya na haitakiwi kuingilia. Hii inatakiwa kuwa inajitegemea kama foundation nyingine na zitafute pesa hata kama ni Kenya, USA .... na wadau wote waliokuwa wanampenda. Lakini siungi mkono serikali kuanza kufanya vitu vya kupongezana kwa pesa za wananchi. Foundation nyingine za wastaafu zinajiendeleza zenyewe.