Uchaguzi 2020 Pendekezo: John Mrema agombee ubunge jimbo la Vunjo

Kweli, ni muda muafaka wa watanzania kuacha na hawa wazee ambao wanaona majimbo ni Mali yao....

Leo yupo CDM jimbo lake akienda CCM anataka kuondoka nalo eboo... kwani jimbo limegeuka mkeo?
 
Huyo ni mla ruzuku na mpambe wa kudumu wa Mh. Mbowe!
 
Mrema ni mkazi wa kuzaliwa na kukulia Vunjo , ndiye aliyepewa kijiti na Chadema kugombea ubunge Vunjo 2015 , lakini ilibidi ajiondoe ili kuheshimu UKAWA

Mkuu sina matatizo na majibu yako mazuri, lakini nauliza ana makazi ya kudumu huko Vunjo? Ni vyema cdm wakajenga utaratibu wa kuwapa nafasi wawakilishi wenye makazi ya kudumu katika jimbo husika. Hii itasaidia mbunge kuwa na wananchi waliomchagua muda wote. Huu mchezo wa kuchagua mtu mwenye makazi ya kudumu sehemu nyingine, kisha kuwaacha wapigania chama wenye makazi ya kudumu eneo husika, inawavunja watu moyo kukipiginia chama. Huu mtindo wa kuleta watu ambao sio wakazi wa kudumu wa jimbo husika, ndiyo ulichangia kuokota wanaccm dakika za mwisho uchaguzi uliopita, kisha wanaccm hao 95% wakarejea ccm! Cdm inapaswa kujifunza kwa kosa lile. Ni kweli John Mrema ni mzuri, lakini hastahili huko Vunjo kama hana makazi ya kudumu. Ni vyema akagombea hapa hapa Dar ambako ana makazi ya kudumu.

NB: Hii mikakati mnaipanga tumeshapata tume huru ya uchaguzi? Ujue kama hakuna tume huru ya uchaguzi, sisi wapiga kura wa upinzani hatutapoteza muda wetu kupiga kura.
 
Uko sawa kabisa Mkuu ,Hutu bwana mpaka mda huu namuona ameiva kwenye mambo ya siasa ,akipanda kwenywe jukwaa kupiga kampeni anaweza kua tishio sana
 
Kwanza hakuna mchaga yeyote mwenye hela asiye na makazi yake binafsi kwao , lakini juhudi zetu kudai tume huru unazifahamu , na labda kwa sauti ya chini sana nikunong'oneze kwamba pamoja na mambo mengine , Lissu hayuko Ulaya kifala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…