Pendekezo: Kama Zitto Kabwe atagombea ubunge jimbo la Muhambwe basi CHADEMA imuunge mkono

Pendekezo: Kama Zitto Kabwe atagombea ubunge jimbo la Muhambwe basi CHADEMA imuunge mkono

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
ACT Wazalendo imesema watashiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Muhambwe kujaza nafasi ya mbunge iliyo wazi baada ya mbunge wa awali kufariki dunia.

Katibu mkuu wa ACT Wazalendo mh Shaibu amesema kuna tetesi kuwa Zitto Kabwe anataka kugombea lakini wao kama chama Zitto hajawaambia kama ana nia hiyo lakini kama itampendeza kugombea milango iko wazi kwa sababu ana sifa zote.

Nashauri endapo Zitto Kabwe ataamua kugombea basi CHADEMA imuunge mkono lakini siyo lazima.

Kila zama na kitabu chake.
 
Wapinzani wanachelewesha Maendeleo bana, nyie chukueni tu jimbo lenu.
 
Huyo ni mfanyabiashara ya siasa CHADEMA wekeni CHUMA.
 
Ah! Kila zama na kitabu chake eeh?

Kwanini hujapendekeza Steven Masatu Wasira akagombee huko au wale waliopigwa chini kwenye utawala wa Chato?
 
Ah! Kila zama na kitabu chake eeh?

Kwanini hujapendekeza Steven Masatu Wasira akagombee huko au wale waliopigwa chini kwenye utawala wa Chato?
Sijapendekeza akagombee bali nimesema kama atagombea akina Felix Mkosamali wamuunge mkono.

Uwe unaelewa bwashee!
 
Hiki kitakuwa kipimo kizuri cha kuona nguvu za CCM bado ziko au ndio arijojo.
 
Back
Top Bottom