Pendekezo: Kama Zitto Kabwe atagombea ubunge jimbo la Muhambwe basi CHADEMA imuunge mkono

Pendekezo: Kama Zitto Kabwe atagombea ubunge jimbo la Muhambwe basi CHADEMA imuunge mkono

Hivi yule anayejiita mbunge nje ya bunge ELIA F MICHAEL Kama sikosei n Jimbo gani yule kilaza
 
Z
ACT wazalendo imesema watashiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Muhambwe kujaza nafasi ya mbunge iliyo wazi baada ya mbunge wa awali kufariki dunia.

Katibu mkuu wa ACT wazalendo mh Shaibu amesema kuna tetesi kuwa Zitto Kabwe anataka kugombea lakini wao kama chama Zitto hajawaambia kama ana nia hiyo lakini kama itampendeza kugombea milango iko wazi kwa sababu ana sifa zote.

Nashauri endapo Zitto Kabwe ataamua kugombea basi Chadema imuunge mkono lakini siyo lazima.

Kila zama na kitabu chake!
Zitto atamaliza majimbo yote ya Kigoma kwa urafi wa kutaka kuwa mbunge, jamani kuna maisha nje ya ubunge, demokrasia ni kuwaachia na wengine wajaribu bahati yao,kwa sasa hatumhitaji Zitto kwani ni muongo na hana lolote,kuna wakati alisema atawataja walioficha pesa Uswisi lakini kumbe hiyo ilikuwa ni gia ya kuwa blackmail hao wenye vijisenti vyao huko Uswisi.
 
Jimboni Muhambwe CCM tuna TAMIM JAMAL

CDM, ACT, NCCR, CUF nk leteni wagombea ili wajipatie ruzuku ila kusema ushindi ni ndoto - nimeyaandika leo 29/03
Msakila M Kabende
CCM No. 75
 
ACT wazalendo imesema watashiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Muhambwe kujaza nafasi ya mbunge iliyo wazi baada ya mbunge wa awali kufariki dunia.

Katibu mkuu wa ACT wazalendo mh Shaibu amesema kuna tetesi kuwa Zitto Kabwe anataka kugombea lakini wao kama chama Zitto hajawaambia kama ana nia hiyo lakini kama itampendeza kugombea milango iko wazi kwa sababu ana sifa zote.

Nashauri endapo Zitto Kabwe ataamua kugombea basi Chadema imuunge mkono lakini siyo lazima.

Kila zama na kitabu chake!
Wanafki mkiwa kazin, Mungu atawachoma asee. Hata marehemu hajamaliza wiki kaburini mshaanza kumgeuka??

Sent from my vivo 1611 using JamiiForums mobile app
 
ACT wazalendo imesema watashiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Muhambwe kujaza nafasi ya mbunge iliyo wazi baada ya mbunge wa awali kufariki dunia.

Katibu mkuu wa ACT wazalendo mh Shaibu amesema kuna tetesi kuwa Zitto Kabwe anataka kugombea lakini wao kama chama Zitto hajawaambia kama ana nia hiyo lakini kama itampendeza kugombea milango iko wazi kwa sababu ana sifa zote.

Nashauri endapo Zitto Kabwe ataamua kugombea basi Chadema imuunge mkono lakini siyo lazima.

Kila zama na kitabu chake!
Si mnasema Chadema imekufa?
 
ACT Wazalendo kwa vyovyote vile watashinda huu uchaguzi. Hawahitaji kuungwa mkono na Chadema maana sasa hivi lengo ni kupata upinzani ambao angalau utaonekana makini. Chadema wakijihusisha kwa namna yeyote kabla ya matakwa yao ya Tume Huru na Katiba mpya kutawapotezea imani ya wanachama wao wengi. Kwa vile ACT Wazalendo wameisha shiriki kwenye chaguzi Zanzibar na wameonyesha kuwa wao ni chama rafiki cha CCM hawatakuwa na pingamizi kushiriki. Chadema wasijihusishe kwa namna yeyote ile.

Amandla...
 
Ah! Kila zama na kitabu chake eeh?

Kwanini hujapendekeza Steven Masatu Wasira akagombee huko au wale waliopigwa chini kwenye utawala wa Chato?

Tz sasa hivi raha sana. Kwamba sress za bwana yule hazipo tena?

Yaani mambo yote burudani tu!
 
Kwa hiyo Kigoma pekee mpaka sasa ina majimbo mawili yaliyo wazi Buhigwe na Muhambwe...

Naunga mkono Zito Kabwe (ACT - Wazalendo) agombee mojawapo ya majimbo hayo hasa jimbo la Muhambwe...

Aidha kijana Felix Mkosamali (CHADEMA) arudie tena kugombea jimbo la Buhigwe ambalo alishinda mwaka 2020 lakini akaporwa kwa nguvu na Magufuli...
 
Jimboni Muhambwe CCM tuna TAMIM JAMAL

CDM, ACT, NCCR, CUF nk leteni wagombea ili wajipatie ruzuku ila kusema ushindi ni ndoto - nimeyaandika leo 29/03
Msakila M Kabende
CCM No. 75
Kama kamati kuu ya CCM itampitisha Jamal, Zitto atakuwa na njia nyeupe ya kuchukua jimbo hilo
 
CHADEMA wakisimamisha mgombea huko lazima watakuwa na kichaa.
 
Na VP mteuli anatoka Jimbo gani? Nalo hilo jimbo lake si liko wazi?
 
Kumbe anatoka Buhigwe...ili Jimbo nalo si liko wazi? baada ya Philip Mpango kuwa VP
 
Hata nikigombea mimi kwa tiketi ya chama chochote against CCM ni dhahili nitashinda - cha msingi sasa CCM waanze kuona aibu - nchi na dunia nzima wanachekwa kwa namna walivyoendesha zoezi la uchaguzi Mkuu uliopita - Mama Samia usikubali matope haya wakupake na wewe !! Waambie atakayechezea chaguzi hizi ndogo zikileta maafa ni wewe na yeye !!

Otherwise Kigoma yote by nature ni Opposition sababu waha wanajua HAKI zao na wanajitambua.... Muha by nature si mtu wa kujikombakomba eti asaidiwe - ni wapambanaji.

Miaka ya 90's walianza vuguvugu la kutaka kuanzisha State yao baada ya kuona Serikali imewasahau mno as if wao si sehemu ya nchi ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom