Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,053
- 2,207
Tanzania kwa mara nyingine tena inashuhudia tukio la pili la kigaidi ambalo limevuta hisia kutoka jamii mbalimbali za kimataifa.ukiacha tukio la kulipuliwa kwa ubalozi wa marekani utaona tukio la Olasiti linazidi kudhihirisha kuwa Tanzania yaweza kuwa eneo linalotoa mwanya kwa magaidi kupanga na kutekeleza mashambulizi ya kigaidi iwe ndani ya Tanzania au nchi za jirani.
Tumewahi kusikia kuwa mmoja wa waliolipuwa mabomu huko kampala na kuleta madhara kwa wale waliokuwa wakifuatilia fainali za kombe la dunia alikuwa ni mtanzania/aliishi Tanzania.
Kwa maoni yangu watanzania ni wamoja mno nikimaanisha pamoja na matukio kadhaa ya misuguano ya kidini bado wameendelea kusalimiana,kutaniana,kuzikana,kuzungumza na kufanya kazi pamoja.
Lakini kuna kikundi cha watu wachache sana ambao wanataka kuharibu amani ya nchi hii na mataifa kwa ujumla.ni kikundi chenye fedha,wataalamu na mikakati mifupi na mirefu yenye malengo maalumu ambayo hayana tija kwa waislamu,wakristu na wapagani.
Kwa mwelekeo ulivyo tunazidi kuzama kwenye jahazi la ugaidi(wala sio udini)
kuna mtu aliwahi kuleta thread hapa jamvini kwamba ameona kundi la vijana wakiwa kwenye mafunzo ya karate na dini huko njiro Arusha,kuna mtu yoyote anayewafuatilia kujua lengo la mafunzo hayo ni lipi?wakitoka hapo wanaenda wapi?je serikali inafahamu au kuratibu mafunzo ya namna hii?
Kimsingi hoja yangu inataka kujikita katika kuanzishwa kwa kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi(counter terrorism unit) ili kufuatilia nyendo za magaidi nchini.
Hivi karibuni tunaweza kuwa wachimbaji wazuri wa madini ya urani ,sitegemei kama magaidi watakaa mbali na nchi yetu!tusisubiri kufika maeneo ya matukio na kutoa pole bali tujipange kwa kuepusha ugaidi.
Ni vizuri sheria ya ugaidi ikapitiwa vizuri kuona kama inaruhusu/itaruhusu kuundwa kwa kikosi hiki maalumu cha kupambana na ugaidi.
Ni aibu pia kwamba kila wakati tunahitaji msaada wa CIA,FBI ili kufuatilia matukio ya kigaidi ni vyema tukawa na CTU yetu!