Pendekezo: Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu, ili tukomboke kifikra

Pendekezo: Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu, ili tukomboke kifikra

Rawasha,
Ni mazoea tu na si kwamba hayo maneno ya kiingereza ni rahisi kuliko kiswahili kwanza kuna hayo kiingereza sawa tunayajua lakini hata kuyatamka hatuwezi kutamka vizuri,sasa unakuta mtu hata kiingereza hajui ile kabisa yani hata kusoma tu neno la kiingereza(acha kujua maana yake) hawezi halafu unakuta anasema kiswahili kwenye simu ni kigumu kuliko kiingereza wakati kumbe hata hayo maneno yenyewe ya kiingereza hajui maana yake.
 
MASSHELE,
Kinachonifurahishaga haohao wanaopigia chapuo kiswahili kutumika unakuta watoto wao wanawapeleka academy unajuliza ka sio kingereza kuzuri nn haswa wanachokifata
 
Mnaopigia debe kiswahili kitumike kufundishia huwa siwaelewi. Ila kwa taarifa
1. Somo la Kiswahili ni miongoni ya masomo Wanayofeli wanafunzi wetu.
Kuna Mwaka Raia wa China aliongoza ktk somo la kiswahili matokeo ya kidato cha nne
2. Tafiti zinaonesha Kenya wanaongea Kiswahili Fasaha kuliko Sisi.
 

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    92.9 KB · Views: 1
Ni pendekezo zuri, ila kwa maoni yangu naona kwamba, hili litaleta shida, mi nashauri kishwahili klichopo sasa, ufumo wake waufundishaji uboreshwe na Kiswahili kisionekane kigumu kama vile tunavyoona ikitumika zaidi ya mawasiliano.

Wenzetu Kenya wanatumia Kingereza ila bado Kiswahili chao kidogo wanachofundishwa ni tofauti na fasaha kuliko chetu. Na wanamafanikio makubwa kuliko sisi. Sisi wenye hiyo lugha tunashindwaje?
 
Kiswahili kutumika kufundisha mpaka elimu ya juu ni ndoto zilizokuwepo zamani wakati watu wana mapenzi na nchi yetu kipindi tuna tabia za umimi - ona tulipoishia

Kutekeleza hilo jambo ni kama kufanya majaribio ambako matokeo yakee hujajipanga kuyadhibiti, tufahamu ya kuwa dunia ya sasa ni ya utandawazi, hii dunia tunaishi kama jamii moja na English ndio daraja.

Mambo mengine bora yabaki kama ndoto tuu siyo ya kutekelezeka, ni kama idea ya Utopia tu
 
Asilimia kubwa ya wanafunzi wa sekondari wanafeli kutokana na tatizo la lugha ya kiingereza kutokuwa na uwezo nayo. Sasa kipi kifanyike ili hawa wanafunzi/watoto wetu wavuke hiki kikwazo.

1. Mkazo uwekwe kwa lugha ya
kiingereza kuanzia ngazi ya chekechea,tofauti na sasa ambapo elimu hii
 
Kipeto Lugha cha Kiolesura cha Windows 7

Kipeto Lugha hiki Kiolesura cha Windows (LIP) hutoa toleo lililofasiriwa nusu la maeneo yanayotumika sana ya Windows. Baada ya kusanidi LIP, matini katika vigagula, vikasha ongezi, menyu, na mada za Msaada na auni zitaangazishwa katika lugha ya LIP. Matini ambayo hayajatafsiriwa yatakuwa katika lugha msingi ya Windows 7. Kwa mfano, kama ulinunua toleo la Kihispania la Windows 7, na ukasanidi LIP ya Kikatalani, matini mengine yatabaki katika Kihispania. Unaweza kusanidi zaidi ya LIP moja kwa lugha moja msingi. LIPs za Windows zinaweza kusanidiwa kwa matoleo yote ya Windows 7.

Mifumo ya Uendeshaji Inayokubaliwa:
Windows 7


  • • Microsoft Windows 7
    • Usanidi wa lugha msingi unaohitajika wa Windows 7: Kiingereza
    • 4.63 Mb ya nafasi huru ya kupakua
    • 15 Mb ya nafasi huru ya kusanidi

ONYO: Kama una usimbaji fiche wa BitLocker uliowezeshwa, tafadhali usitishe kabla ya kusanidi LIP. Fungua Control Panel, teua System and Security, kisha BitLocker Drive Encryption. Bofya kwenye Suspend Protection.

Kwa sababu kuna vipakuaji vya kando vya matoleo ya 32-biti na 64-biti vya Windows 7 LIP, kabla ya kuanza kupakua, unahitaji kubainisha ni toleo lipi la Windows 7 ulilosanidi. Hivi ndivyo unavyostahili kubainisha ni toleo lipi la Windows 7 ulilosanidi:

Bofya kwenye kitufe Start kisha bofya kulia kwenye Ngamizi na uteue Properties. Hii italeta maelezo msingi kuhusu ngamizi yako.
Angalia katika sehemu ya Mfumo ya aina ya Mfumo. Hii itaashiria kama Mfumo wako Endeshi wa Windows 7 ni Mfumo Endeshi wa 32-biti au kama ni Mfumo Endeshi wa 64-biti.


I Rest My Case
 
bahati93,
Sasa mbona Tanzania inajulikana kuwa kiingereza ni shida kwetu na wengi hawajui kiingereza pamoja na kuwa kinatumika kufundishia huko mashuleni?
 
Mnaopigia debe kiswahili kitumike kufundishia huwa siwaelewi. Ila kwa taarifa
1. Somo la Kiswahili ni miongoni ya masomo Wanayofeli wanafunzi wetu.
Kuna Mwaka Raia wa China aliongoza ktk somo la kiswahili matokeo ya kidato cha nne
2. Tafiti zinaonesha Kenya wanaongea Kiswahili Fasaha kuliko Sisi.
Kuna tofauti kubwa ya kiswahili kama somo na kiswahili kama lugha. Na kuna tofauti kubwa ya english kama somo na english kama lugha. Hata somo la english Language tunalofundishwa, kiukweli tunafundishwa kama somo na sio kama lugha kwa lengo la kumfanya mtu ajue lugha. Mimi bado napendelea kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia, na english ibaki kama somo la lazima kuanzia chekechea hadi chuo kikuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa mbona Tz inajulikana kuwa kiingereza ni shida kwetu na wengi hawajui kiingereza pamoja na kuwa kinatumika kufundishia huko mashuleni?
Kwa sababu hatujajipanga kimkakati kubadili hali hio kama ilivyo masomo mengine pia
 
Dunia inatarajia kubaki na lugha moja miaka 100 ijayo kutokana na Kasi ya science na technolojia probably lugha zenyewe itakua Kati ya English, mandarin na spanishi
 
Walimu wa Kiswahili tupo wa kutosha nayo hii ni bahati sana ila taifa hili linatuona takataka kabisa... Ni kweli lugha ni uchumi. Ukitaka kukuza lugha yako kuza kwanza uchumi wako kisha uchumi wako utakuza lugha!
 
Kwa sababu hatujajipanga kimkakati kubadili hali hio kama ilivyo masomo mengine pia
Sasa mbona kuna kuwa na hoja ya kwamba tukitumia kiswahili kufundishia tutakuwa hatujui kiingereza na kushindwa kuwasiliana kwa kiingereza hali ya kuwa hivi sasa hicho kiingereza hatujui?
 
Manelezu,
Hao siyo kwamba wanafundisha kwa lugha zao kwasababu wameendelea kwenye sayansi na teknolojia bali wameendelea kwenye sayansi na teknolojia sababu wanatumia lugha zao.

Unaangalia matokeo badala ya chanzo. Soma Meiji restoration jinsi wajapan walivyoitafsiri elimu ya magharibi kwenda kijapan. Huwezi endelea wala kuelimika kama unajifunza kwa kutumia lugha usiyoielewa vizuri.
 
maganjwa,
Hili ni tatizo kubwa ambalo wengi wanaliona kinyumenyume. Iko hivi, Matajiri na wanasiasa wanapeleka watoto wao shule za kiingereza toka wana miaka 3. Sisi wengine tunapeleka chekechea na shule za msingi. Kufika sekondari kinaanza kiingereza, watoto wao wanafaulu wakati wetu wanapata 0 na 4.

Mtu anasema kujifunza kwa kiswahili hadi elimu ya juu kutafanya watoto wetu watawaliwe, hawajui mfumo wa sasa unafanya watoto wa maskini wawe form four failures wakutumikishwa. Matumizi ya kiingereza kuanzia sekondari yanampendelea mtoto wa tajiri eliesoma english medium.
 
Back
Top Bottom