Pendekezo: Kuwe na Daladala VIP kukabiliana na foleni

Mbona hizo VIP zipo sana kuanzia saa 11 alfajili. Inaelekea unalala sana. Shida kubwa ipo kwa LATRA hawa wanaleta msongamano wa magari jijini. Wanaua route kijinga sana wanatakiwa watengeneze route ndefu mfano Simu 2000 Chalinze ama simu 2000 Bagamoyo. Ukishakuwa na route ndefu unapunguza sana uwepo wa vituo vidogo vidogo vingi ambavyo havina sababu. Hili la VIP route wangelianzisha hawa DART mwendokasi. Wangekuwa na VIP muda wa asubuhi na jioni. Mbezi Kivukoni 3000 na Kimara kivukoni Tshs 2500. Pia wafanye na kariakoo watahudumia hasa.
 
Nairobi ndo wanaweza hilo
 
Hii siyo kwa wabongo.
Mwaka fulani hapo kulikuwa na Coaster, Mwananyamala to Posta imefanya kazi miezi kadhaa mara chali.

Sababu hatujui ila ingekuwa na ufanisi nina uhakika ingekuwepo au kuongezeka. Biashara ya usafirishaji inalipa sana but ni biashara unayotakiwa kutumia akili.

Mfano; Usione kuna kampuni zipo ulingoni mpaka leo kuna dhoruba huko ndani we acha kabisa.
 
Vibali vilimtoa
 
Wazo zuri.
 
Una wazo zuri sana. Kusema kweli dala dala za Dar ni kero mbaya sana.
 
Wazo zuri sana, zamani pale posta kuna gari zilikuwa nafikiri zinasajiliwa kwa leseni ya tour walikuwa wanatoa hii uduma, unalipia kwa kadi ya mwaka au miezi sita au mwezii mmoja ikifika saa 9:00 inapark pale PPF TOWER abiria wanapanda ilikuwa inapiga route ya Mbezi Kimara
 
Nani ataekubali lipa 3000 ashukie njiani?
Huu uzi umewalenga Wale wenye magari binafsi, kwa hiyo nauli hata kama itakuwa ni tzs 5,000 bado ni ndogo kwao na wanamudu. Na lengo ni kupunguza Foleni
nafikiri likikifanyika litapunguza msongamano wa magari kwa asilimia kubwa.
Nilikuwa nafikiria zikisajiliwa daladala za VIP ambazo zitakuwa na Air conditioning usafi wa hali ya juu zikapiga ruti mfano Tegeta- Posta kwa Tsh 3,000 na abiria wote level seat hakuna kusimamisha abiria.
Point ya msingi ya kuzingatia ni kuwa, Wale wenye magari binafsi, wako tayari kuacha magari nyumbani na kutumia usafiri wa umma ulioboreshwa, bila kujali ghalama ya nauli kuwa kubwa, wao wanachotaka ni ubora wa huduma ya usafiri. Root
 
Kujali nauli lazima kwasababu haina maana ikiwa nauli hio itazidi au kukaribia gharama za mafuta atakayotumia kwa gari yake. Pia wengi wanatoka ndani kidogo sio barabara kuu ambapo kufika main road itabidi achukue boda mwisho wa siku atatumia 8000/- kwenda na kurudi ambayo akiweka kwenye gari yake inatosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…