Pendekezo: Kuwe na Daladala VIP kukabiliana na foleni

Hizo nauli ni plates za chakula kwetu sisi wanyonge! Nauli iwe buku tu sio zaidi
 
Wafanye buku bee angalau wengine tuwe tunapumzika ku-drive daily na siku tukikosa pesa ya wese tusiongeze mbanano kwenye daladala.....ninachoona msongamano kwenye daladala unaenda kuwa mkubwa sana kwa sababu hata baby-walker hazitaendesheka kwa hizi bei za mafuta.
 
Wazo zuri sana. Kuna bwana mmoja tulikaa naye jirani alikua na Noah yake kila siku asubuhi saa 12 anachukua abiria wake sita kwenda town, anashusha anaenda zake kazini. Jioni tena saa 11 anarudi home na abiria wake waliokua tayari. Bei elfu 2 one way.
Kwa sababu ilikua ya mtaani na wote tunajuana ilikua na maudhi kidogo. Mfano mtu kachelewa asubuhi anampigia simu jamaa amsubiri, hasa akina mama. Jioni nayo hivo hivyo. Sasa akishakua jirani mnayefahamiana kunakua na ugumu kidogo.
Jamaa akajenga nyumba yake sehemu nyingine kwetu akahama. Watu wanamkumbuka mpaka leo.
Kwa hiyo abiria wapo, tena wengi tu
 
Wengi wanasahau hilo.

Utoke bonyokwa hadi stand kuu na suti yako?

Ushuke Morroco uende TMJ na suti yako kwa boda?

Ofisi nyingi hazipo arround stand.
 
Wengi wanasahau hilo.

Utoke bonyokwa hadi stand kuu na suti yako?

Ushuke Morroco uende TMJ na suti yako kwa boda?

Ofisi nyingi hazipo arround stand.
Yaa, hili nalo ni angalizo....maana unaweza kutumia pesa nyingi zaidi ukaona bora utumie gari lako. Nafikiri waziweke tu ila wawe makini kwenye kupanga nauli zisiende juu sana, labda ziwe kati ya 1,000 na 2000.
 

Mimi walete tu
Nimechoka kubambbiwa kwenye mwendokasi
 
Yaani mtu alipe 6000 ambayo ni sawa na lita 2.5 ambayo ni kama km 16 tena asiwe na privacy?
 
Nilikuwa nafikiria zikisajiliwa daladala za VIP ambazo zitakuwa na Air conditioning usafi wa hali ya juu zikapiga ruti mfano Tegeta- Posta kwa Tsh 3,000 na abiria wote level seat hakuna kusimamisha abiria.
Hii ni nzuri sana, ila 3000 ni kubwa sana labda 1000 meaning one way mtu ana uhakika wa 28K kule Morogoro kuna bus mbili ninasafiri kati ya Morogoro na Gairo, hakuna abiria kusimama, na ni nadra kuchukua abiria wa njiani kama ikiwa imeeneza abiria kwenye viti
 
Hivi foleni husababishwa na magari?
Kumbe magari yako mengi

Ova
Nadhani hoja yake ni kwamba kukiwa na coaster moja ikapakiwa watu 28 maana yake kuna magari matano yataondoka kwenye msongamano na ikiwa kuna coaster 5 basi kuna magari 25 yataondoka kwenye msongamano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…