kiwatengu
Platinum Member
- Apr 6, 2012
- 19,493
- 18,387
Wakuu, Nawasalimu,
Kwa heshima na taadhima, napenda kutoa wito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda Tume Huru ya Kuchunguza Mwenendo wa Jeshi la Polisi, yenye dhamira ya kuhakikisha kuwa utendaji wa jeshi hilo unazingatia haki za binadamu, uwajibikaji, na matumizi ya madaraka kwa mujibu wa sheria.
Tume hii itakuwa na majukumu ya:
Ninaamini kuwa kwa kuwepo kwa chombo huru, Serikali itaimarisha zaidi misingi ya utawala bora, haki za binadamu, na amani nchini.
Naomba kuwasilisha;
cc; Bashungwa, na Waziri Gwajima.

- Kufuatilia na kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na nguvu kupita kiasi.
- Kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu vitendo visivyofaa vinavyofanywa na askari.
- Kuwasilisha mapendekezo ya maboresho ya maadili na uwajibikaji katika utendaji wa polisi.
- Kusaidia kujenga imani kati ya wananchi na Jeshi la Polisi, kwa kuweka uwazi na uadilifu mbele.
Ninaamini kuwa kwa kuwepo kwa chombo huru, Serikali itaimarisha zaidi misingi ya utawala bora, haki za binadamu, na amani nchini.
Naomba kuwasilisha;
cc; Bashungwa, na Waziri Gwajima.