Pendekezo la Kuundwa kwa Tume Huru ya Kuchunguza Mwenendo wa Polisi Tanzania

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,493
Reaction score
18,387
Wakuu, Nawasalimu,

Kwa heshima na taadhima, napenda kutoa wito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda Tume Huru ya Kuchunguza Mwenendo wa Jeshi la Polisi, yenye dhamira ya kuhakikisha kuwa utendaji wa jeshi hilo unazingatia haki za binadamu, uwajibikaji, na matumizi ya madaraka kwa mujibu wa sheria.

Tume hii itakuwa na majukumu ya:
  1. Kufuatilia na kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na nguvu kupita kiasi.
  2. Kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu vitendo visivyofaa vinavyofanywa na askari.
  3. Kuwasilisha mapendekezo ya maboresho ya maadili na uwajibikaji katika utendaji wa polisi.
  4. Kusaidia kujenga imani kati ya wananchi na Jeshi la Polisi, kwa kuweka uwazi na uadilifu mbele.
Kwa kuzingatia changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara kwa mara, kama vile tuhuma za ukatili, vitisho, na kutotendewa haki kwa baadhi ya wananchi, tume hii itakuwa chombo muhimu cha kuhakikisha kuwa wahusika wote wanawajibika bila upendeleo.

Ninaamini kuwa kwa kuwepo kwa chombo huru, Serikali itaimarisha zaidi misingi ya utawala bora, haki za binadamu, na amani nchini.

Naomba kuwasilisha;
cc; Bashungwa, na Waziri Gwajima.
 
Wanaopaswa kuiunda hiyo tume ndio wanasifia kila siku lina weledi na kwamba limefikia viwango wanavyotaka kwa maslahi yao! Katiba mpya itafumua haya maincompentence sehemu zote maana nchi imeoza kuanzia kichwani so kukata mkono hakutatibu hii kansa mkuu! Mawazo yangu...
 
Ikiwa bado hatujashughulika na katiba hakuna tume huru ya uchunguzi itakayotuletea matokeo. Anaetakiwa kuunda hiyo tume ndio mnufaika mkuu wa matukio yanayofanywa na jeshi la polisi. Kwa, tume nyingi sana za kijaji zimeundwa zimefanya uchunguzi na kuleta majibu aidha kwa kupindisha ukweli, au ukweli ukafunikwa na kuwekwa kabatini au majibu yakasomwa ila wanufaika wasiyafanyie kazi. Tumeshuhudia tume nyingi zilizofanya uchunguzi ukawekwa kabatini ukakataliwa.

Tatizo la msingi hapa ni katiba, bila kushughulika na katiba ili kumuondolea mkuu wa nchi imprints kwenye mihimili yote ya serikali, vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi za umma, hakuna tume utafanya uchunguzi tukapata matokeo na kuwaona wanaotakiwa kuwajibishwa wanawajibishwa.

Wazo la kuundwa tume ni upotevu wa rasilimali na muda tu.
 
Pendokezo ni kwa jinsi gani Lema anaweza tunza familia nje ya nchi na hana kipato chochote ni muhimu sana aisee.
 
Hahaha utakuwa na mapepo, shetani hachunguzwi anafukuzwa.

Mungu alipomshindwa shetani hakuunda tume, alimfukuza tu.

Yani ccm waunde tume halafu upate matokeo gani wewe?

Nchi hii ukihesabu tume zinaweza kuzidi idadi ya raia wa nchi hii lakini matokeo zero.
 
Kenya wana kitu kinitwa INDEPENDENT POLICE OVERSIGHT AUTHORITY..........................
 
Ww nae ni matako kabisa, police wanafanya kwa maagizo ya hiyo serikali
 
Haitasaidia kwa sasa bila na kuwa na katiba mpya.

Nchi kila wenye cheo anaweza waamurisha police, kuanzia mkuu wa wilaya mpaka juu.

Katiba ni muhimu itakayo weka mipaka nani wa kutoa amri kwa jeshi la police, sio kila mtu akiamuka tu anaweza amrisha, katiba itakayo wapata police mamlaka ya kufanya kazi yao kwa weledi.

Leo unashangaa watu wanapigwa na kutupwa polini, Mulilo anasema hao sio police ,sasa kama sio police ni wakina nani,

Tuseme sio police may be ni vibaka flani ambao wamefanya vile kuchafua chombo chao.

Je mpaka sasa wamekamatwa wangapi ?
 
Pendokezo ni kwa jinsi gani Lema anaweza tunza familia nje ya nchi na hana kipato chochote ni muhimu sana aisee.
Akili ya watz inasikitisha sana yani, tulinyang'anywa ufahamu kabisa yani, watu wanafikiria mambo makubwa ya kitaifa hii mbuzi inafikia kula, kunywa na kwenda chooni! Lema alikwambia ana njaa? Ongeza ufahamu wako kwenda veta uache kujitia aibu ndogondogo hizi we baba mtu mzima na watoto wako watakuja kusoma huu uharo miaka 20 ijayo! Na mama anakulipa tu kwa huu uharisho?
 
Wazo lako ni zuri ila nasikitika sana, hilo halitatokea. Unayetaka aseme Tume iundwe, ndiyo kwamza kawapongeza policcm kwa kuwapa magari mapya.

Na haya maalumu kwa uchaguzi. Usifikirie hao policcm wanajiamulia tu, kwenda kupiga watu. Ukiona kuna mbwa basi jua mfuga mbwa yupo.
 
Ikiwa Tume Huru ya Uchaguzi kindende itakuja kuwa Tume Huru ya Polisi, si tashangaa wakakusikilizeni na kuiunda.
 
Wangeweza kuiga magereza tungefika mbali sana
 
Wajumbe watakaoteuliwa utawakubali?
 
We zombie kaunde tume kujua kwanini we ni mpumbavu hivyo?
 
Uchafu km wa chooni
 
Sidhani kama ilishatokea tume kama hiyo
tume huru inapaswa kuundwa kwa mamlaka ya bunge ili repoti yake iwasilishwe bungeni na iwe wazi kwa wananchi na wajumbe wa tume watakuwa na utaratibu maalum wa kuteuliwa

Tz zinakuwepo tume za rais na sio tume huru
tatizo ni sheria za nchi za kupata hiyo tume huru
 
Polisi wapo kwa ajili ya kulinda maslahi binafsi ya Wanasiasa na Mali zao.....alafu unataka hao hao Wanasiasa wawachunguze polisi? 🤔🤔🤔 HILO LITAWEZEKANA ITAKAPOBADILISHWA KATIBA TOFAUTI NA HAPO HAKUNA HICHO KITU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…