Mwaka huu ni miaka 10 tangu rais wa China, Xi Jinping, alipotoa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.
Zaidi ya miaka 1000 iliyopita, misafara ya ngamia ilipita katika Njia ya Hariri ya Kale, ikikabiliwa na upepo mkali na jua, ikichukua hariri na chai kutoka China na kuzipeleka katika nchi za Asia ya Kati na bara la Ulaya. Hivi sasa, bidhaa zisizo na uchafuzi zinafikishwa katika nchi zilizo kwenye Ukanda Mmoja, Njia Moja kwa kutumia usafiri wa ndege na treni za mizigo, na kubadili upepo na jua kuwa vitu vya thamani kubwa.
Wakati maendeleo ya kijani yanaendelea kushika kasi duniani, kampuni nyingi Zaidi za China zimekuwa nguvu kubwa katika kujenga Ukanda Mmoja, Njia Moja usio na uchafuzi.
Katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi la Ulaya na Asia la mwaka 2023 uliofanyika Xi’an, mji mkuu wa mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, mkuu wa ofisi ndogo ya Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi na Jamii ya Asia na Pasific, Nikolay Pormoshchnikov alisema, eneo la Asia ya Kati lina rasilimali kubwa ya nishati safi ikiwemo nishati ya jua, upepo, na maji, na jukwaa hilo linatoa fursa nzuri ya ushirikiano kati ya China na nchi za eneo hilo.
Mji wa Xi’an, ambao ni mwanzo wa Njia ya Hariri ya Kale, umeshuhudia maendeleo ya kijani kupitia mabadilishano ya kibiashara kati ya China na nchi zilizojiunga na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.
Mwishoni mwa mwezi April mwaka huu, mji huo ulizindua treni ya kwanza ya mizigo kati ya China na Ulaya, inayotumika kusafirisha magari mapya yasiyo na uchafuzi (NEVs).
Takwimu kutoka Shirikisho la Watengenezaji wa Magari la nchini China zinaonyesha kuwa, kuanzia mwezi Januari mpaka Agosti mwaka huu, China imesafirisha magari 727,000 yasiyo na uchafuzi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.1 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.
Mkuu wa Chama katika Kampuni ya Teknolojia ya Nishati ya Kijani ya LONGi, Li Wenxue, anasema kampuni hiyo imetoa moja ya tatu ya vifaa muhimu kwa mradi wa photovoltaic katika nchi tano za Asia ya Kati, huku treni za mizigo kati ya China na Ulaya ambazo kampuni hiyo imeumia kusafirisha PV ikizizidi 100, ambazo zimekwenda katika nchi kadhaa ikiwemo Netherlands, Ujerumani na Ubelgiji.
China imesaini Makubaliano ya Awali na Programu ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa kuhusu ujenzi wa kijani wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuanzisha Uhusiano wa Nishati wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na nchi 32, na kutoa mafunzo kwa watu 3,000 kutoka Zaidi ya nchi 120 zilizojiunga na program ya Mabalozi wa Njia ya Hariri ya Kijani.