Pendekezo: Majimbo watakayoshinda upinzani kodi zao zibaki jimboni mwao

Pendekezo: Majimbo watakayoshinda upinzani kodi zao zibaki jimboni mwao

Joined
Feb 18, 2019
Posts
53
Reaction score
539
Napendekeza, endapo atashinda JPM basi yale majimbo yatakayokuwa yameangukia upinzani kodi zao wabaki nazo ili wapange mipango yao ya maendeleo. Nadhani hili halitakuwa na ubishi kwa sababu JPM ametamka waziwazi kwamba hatapelekea maendeleo kwenye majimbo watakayochagua wabunge wa vyama vingine tofauti na CCM.

Kuna watu watasema HAKUNA JIMBO LENYE UWEZO WA KUJITEGEMEA. Ni kweli kabisa, lakini ni bora kubaki na kidogo chenu mlichochanga kisha mkaplan kwa hicho kidogo, kuliko kuchanga kisha msikirudishiwe hata hicho kidogo chenu. Hilo ni bora mara 1000.

Nadhani endapo atashinda huyu mzee kutakuwa na kesi nyingi sana za kikatiba zinazohusu majimbo ya upinzani kujitoa kwenye mfumo wa kodi wa pamoja, kisha kutaka kujitenga sababu Rais ameshadeclare kwamba hapeleki maendeleo kwenye majimbo ya upinzani. Kuna haja gani ya kuchangishwa kodi ambayo haikunufaishi?

Wanasiasa kwenye akili zenu msisahau Tanzania ni moja japokuwa kuna vyama vingi vya kisiasa. Kama kuna chama hakitaki watanzania wachague chama tofauti na chama chao basi wapeleke muswada bungeni ili nchi irudi kuwa ya chama kimoja. Na chama kinachowabagua watanzania kwa sababu tuu wamechagua chama tofauti na wao basi kimeshakosa legitimacy ya kuongoza sababu kinagawa wananchi na nchi kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom