PENDEKEZO: Nani kumrithi Dkt. Msonde NECTA?

PENDEKEZO: Nani kumrithi Dkt. Msonde NECTA?

Nimesoma hii comment yako nimecheka sana. Kwahiyo unataka kusema kwa kuwa Msonde alikua mkristo ndio alikua anafelisha shule za waislamu?

Duuh namashaka na uwezo wako wa kufikiri..

Acheni kuchanganya mambo ya Dini.. unajidharilisha bure na kama itakuwa ni hivyo kuondolewa kwake ili kudanganya watu katika matokeo. Ni kukuza kizazi mbumbumbu.
Ukirejea historia ya malalamiko hewa yaliyowahi kutolewa na upande wa Waislam hasa kipindi cha Mkapa na Ndalichako huwezi kudharau maoni ya mtoa hoja uliyemjibu hapo juu.

Pia rejea yaliyowahi kutokea chuo kikuu cha Dodoma kati ya mwaka 2012, 2013 na 2014 yanayohusiana na maswala ya dini.

Kuna vitu vinaendelea vya kipuuzi ambavyo Kama si mfuatiliaji na mdadisi wa Mambo huwezi kuvielewa ukivisikia kwa mara ya kwanza

Amini amini nakwambia uwezekano wa mchezo huo kufanyika pale NECTA ni mkubwa sana hasa Kama wanaomzunguka/mshauri Rais hawatakuwa makini sana. Kikwete alijaribu akashindwa

Swali la kujiuliza pia, Kwanini amemtoa kipindi hiki cha kuelekea kusahihisha mitihani ya watoto wanaotarajia kujiunga vyuo vikuu? (Form VI?)

Pili, kwanini amemtoa kabla hata hajamuandaa anayeshika nafasi yake!?? Mbona wengine nafasi zao zimewekwa watu ila NECTA nafasi hajatangazwa leo leo!? Je, anapima upepo Kwanza? Tusubiri tuone
 
Yaani nasikitika, mwanangu anaendelea na mitihani, sijui usahihishaji utakuwaje
Ondoa shaka na uwe na amani, at inidividual level mitihani itasahihishwa poa tu. Lakini linapokuja suala la favouring ikilenga taasisi au kundi fulani (kama litatokea), standard huenda zikabadilika.
 
Kama hujui tu, maslahi (mishahara na marupurupu) ya manaibu katibu mkuu nchi nzima yanafanana. Na yako kawaida sana. Na wengi wao wamechakaa tu, hawana mamlaka yoyote kwa sababu post hizo zinawafanya kuwa makarani wa makatibu wakuu.

Lakini Katibu mkuu wa Necta ni mtu mmoja tu, ni post moja tu, mshahara wake na marupurupu yake ni special package, ni mtu mwenye mamlaka katika taasisi anayoisimamia. Huyo anaweza akapiga hata 10% ya tender ya uchapishaji wa mitihani ya taifa, maana yeye ndio mwenye kuidhinisha tender nk.
Ni kweli yanafanana ila Mzee Tamisemi-Elimu pale ndio Kila kitu,kuna mabilioni na mabilioni
 
Alikuwa ni mtendaji kweli, na akipanga kuanza, kusahihisha mitihani kwa cccomp
Yaani mtendaji super chapakazi. Aliipa heshima NECTA. Teuzi nyingine zinaharibu kabisa. Mama watu wako humu wakuletee kilio chetu kuwa Dr. Msonde arudi NECTA. Fanya kama TPDC
Kwa nn mama anaondoa Sana watendaji wazuri.?Pale Wizara ya ardhi alimuondoa Lukuvi.Au washauri wake ,Wana watu wao?
 
Naona ni wakati muafaka na sahihi kabisa NECTA iwe chini ya Dr.Kasheku Msukuma. Nadhani NECTA itakuwa na maboresho yenye tija.
 
Naibu Katibu mkuu wa wizara anawezaje kusogelea Ikulu?
Hiyo ni full demotion.
Msonde atastaafu miaka michache.
Kimuundo hiyo inaweza isiwe demotion Kama baadhi wanavyodhani kwani NECTA ni baraza tu (Taasisi) ambayo iko chini ya wizara ya Elimu.

Kwa mtazamo huo, kiongozi wa NECTA anafanya kazi chini ya maelekezo ya katibu na Naibu wake wa wizara hiyo.

TAMISEMI nayo ni wizara hivyo kuna Taasisi nyingi (japo kwa TAMISEMI hakuna taasisi nyingi zinazoshughulika na elimu zaidi ya kugombana na Walimu na Maafisa Elimu tu) chini yake kama Naibu katibu Mkuu wa wizara yote.

Kwa mtazamo huo amepanda cheo kutoka kuongoza Baraza na kwenda kuongoza Wizara
 
Yaani mtendaji super chapakazi. Aliipa heshima NECTA. Teuzi nyingine zinaharibu kabisa. Mama watu wako humu wakuletee kilio chetu kuwa Dr. Msonde arudi NECTA. Fanya kama TPDC
NECTA YA MSONDE NI CHUJIO LA MATUNDU MAKUBWA USOME USISOME DIV ONE . VILAZA WATAMTETEA SANA. KILA FORM 4 ANA PTS 7

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Katika mazingira ambayo Msonde akiwa Necta na Magufuli akiwa madarakani, ghafla matokeo ya mitihani ya shule za Chato (ikiwemo primary school aliyosoma Magufuli) na Geita zikawa kinara kitaifa kwa miaka mfululizo, na mara Magufuli alipofariki tu ghafla zikaporomoka na kupotea kabisa!
Tunaweza tukatafsiri nini katika hili kuhusu utendaji wa Msonde na Necta ulivyo?
 
Yule mzee mwendazake alikuwa akitakacho ndicho,

Alitaka shule za gvt zirudi zikarudi
 
Kimuundo hiyo inaweza isiwe demotion Kama baadhi wanavyodhani kwani NECTA ni baraza tu (Taasisi) ambayo iko chini ya wizara ya Elimu.

Kwa mtazamo huo, kiongozi wa NECTA anafanya kazi chini ya maelekezo ya katibu na Naibu wake wa wizara hiyo.

TAMISEMI nayo ni wizara hivyo kuna Taasisi nyingi (japo kwa TAMISEMI hakuna taasisi nyingi zinazoshughulika na elimu zaidi ya kugombana na Walimu na Maafisa Elimu tu) chini yake kama Naibu katibu Mkuu wa wizara yote.

Kwa mtazamo huo amepanda cheo kutoka kuongoza Baraza na kwenda kuongoza Wizara
Endelea kuwaza hivyo hivyo tu, huenda hata Pole Pole aliwaza hivyo hivyo alivyopewa ubalozi wa Malawi kuwa amepata promotion!
 
Katika mazingira ambayo Msonde akiwa Necta na Magufuli akiwa madarakani, ghafla matokeo ya mitihani ya shule za Chato (ikiwemo primary school aliyosoma Magufuli) na Geita zikawa kinara kitaifa kwa miaka mfululizo, na mara Magufuli alipofariki tu ghafla zikaporomoka na kupotea kabisa!
Tunaweza tukatafsiri nini katika hili kuhusu utendaji wa Msonde na Necta ulivyo?
Aina ya mitihani na matokeo ndio vimemtoa . Unawapa sifa ya kujiunga chuo Watu wasio na uwezo unasababisha serekali gharama kubwa . Umeona pt 7 za mwaka huu F4?

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Yule mzee mwendazake alikuwa akitakacho ndicho,

Alitaka shule za gvt zirudi zikarudi
Maana yake ni kuwa Necta inaweza kutumika kutakatisha elimu kwa gharama ya ujinga na upumbavu, na Msonde chini ya Magufuli alitumika kufanikisha hayo.

Sasa katika mazingira ya itikadi za Ugalatia na Ufilisti, nini kinaweza kuzuia Necta kutumika na upande wowote?
 
Katika mazingira ambayo Msonde akiwa Necta na Magufuli akiwa madarakani, ghafla matokeo ya mitihani ya shule za Chato (ikiwemo primary school aliyosoma Magufuli) na Geita zikawa kinara kitaifa kwa miaka mfululizo, na mara Magufuli alipofariki tu ghafla zikaporomoka na kupotea kabisa!
Tunaweza tukatafsiri nini katika hili kuhusu utendaji wa Msonde na Necta ulivyo?
Mchumia tumbo
 
Tumeona ,Msonde kawa promoted to TAMISEMI, (kwa mtazamo wangu hii ni demotion)

Swali la kujiuliza kwanini aondoke MITIHANI YA A LEVEL NECTA ikiwa inaendelea?

Je, kwa mtazamo wako unadhani Nani ni sahihi Kumrithi, Msonde NECTA?

Mimi, nampendekeza Mr.Mbwaga,Innocent (Ana deserve),atafanya mazuri zaidi ya NDALICHAKO na MSONDE.
JF Kuna watu wenye mandate ya kuteua? Kwanini utupe ramli chonganishi? Hiyo ni kazi ya Rais SSH.
 
JF Kuna watu wenye mandate ya kuteua? Kwanini utupe ramli chonganishi? Hiyo ni kazi ya Rais SSH.
Kwa taarifa yako baadhi ya watu pendekezwa teuzi Zao zimeanzia zote humu,

Isipokuwa Paschal tu ambaye bado anasugua benchi
 
Back
Top Bottom