Pendekezo: Naomba shule zifunguliwe baada ya zile siku 30

Pendekezo: Naomba shule zifunguliwe baada ya zile siku 30

Mimi mnanishangaza mnao ng'ang'ania kuwa kuna magonjwa mengine kama kipindu pindu,malaria yanayoua watanzania kila siku,hivi nani alisema corona ikija itaondoa hayo magonjwa???? Corona inakuja na magonjwa hayo yaliopo yataendelea kuwepo...inamaanisha ni Zaidi ya matatizo yaliyopo..
 
Mkuu msaada maana sielewi kabisa hasa lile Tangazo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa hii likizo italipiwa mwezi Julai hatutafunga
Sasa shule zetu za Private mwaka huu watatuua
eti Ada ipo palepale hata kama watoto wako nyumbani kuna Walimu, walinzi na Makarani wanahitaji Mshahara, sasa watoto km ni Day hawaendi km ni Hostel hawalali wala chakula
hapo Masomo wameyakosa kwanini wasikubali na wao kuikosa hiyo pesa maana huku nyumbani ndio tunawanunulia kila kitu
Mgoma km ni mpaka september ina maana Ada yote tuwape kweli si wizi Mkubwa km Wafanyakazi na walimu bora watusamehe hatuwezi walipia ni janga la wote
Kuhusu September hiyo Ni Israel siyo Tz,,Kama wanafunzi watakaa home mwezi mmoja ama na wiki mbili zaidi halafu July wasirudi likizo itakuwa imejifidia,,tatizo hii Hali ikiendelea tuseme Hadi june ama August,,mambo yataharibika
 
Hamna mrija wangu uliofungwa, ni suala la facts tu. Wiki 3 sasa zimepita tangu mgonjwa wa kwanza. Ile wave death haitatokea Africa
Mkuu hiyo conclusion tuipe wiki moja zaidi Hali ikiwa hivi ntakubaliana na hii conclusion
 
Hamna mrija wangu uliofungwa, ni suala la facts tu. Wiki 3 sasa zimepita tangu mgonjwa wa kwanza. Ile wave death haitatokea Africa
USA ITALY SPAIN CHINA UK tena hao ni hatuwapati kwa chochote kile katika dunia wao nao walianza kama sisi ila najua kwa sasa hali zao unajua zipoje tena wao walianza na kisa 1 ila sasa haielezeki nakushangaa ulivyo na tamaa na roho mbaya sana kwamba unaona ni kawaida tu eti mambo yaendelee kaka unantia shaka sana na akili yako kama ipo sawa sawa serikali haijasema labda kupunguza taharuki na ni lazima wanaficha ila waziri wa Afya leo kauli yake ukiangalia kauli ya Makonda na wakuu wa mikoa ma wilaya nyingine wanavyohangaika kwa mtu ambaye una akili timamu unajua hapa pana jambo sasa nashangaa ambavyo hujiongezi unakuwa box tupu kichwani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna mrija wangu uliofungwa, ni suala la facts tu. Wiki 3 sasa zimepita tangu mgonjwa wa kwanza. Ile wave death haitatokea Africa
Mkuu March 12 Liverpool kulikuwa na wagonjwa chini ya 13 sasa zimepita wiki3 tu kuna wagonjwa zaidi ya 300 na wao wameanza mapema lockdown flani.
Weka akiba ya maneno.

Spain, Italy na USA ilianza taratibu hivyo hivyo kisha ikalipuka ghafla boom!
Sisemi kwamba na hapa TZ hali itakuwa kama kule.
Naomba hali isiwe hivyo lakini tuchukue tahadhari, kinga ni bora kuliko tiba.

Shule zipo tu hata mwaka ujao lakini uhai ukiupoteza huwezi kusema upo mwingine wa kufidia au kuendelea nao mwaka ujao.
 
Tunaomba Mungu janga hili lisienee zaidi, mhimu tuzidi muomba Mungu kwa imani zetu. Zaidi ya watoto kurudi shule pia kuondoa hofu miongoni mwetu ili shughuli zote ziendelee normal, tofauti na Sasa kuna wogawoga fulani ktk sekta nyingi za uchumi na kijamii. Lakini tusibeze hata kidogo na kudhani ugonjwa huu ni lelemama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom