ameandika MalisaGJ*
Sio kwamba ripoti hizi zina mpya sana, bali kuna mtu mpya ambaye ameamua kuzifanyia kazi. Zamani zilikua zikisomwa zinawekwa kapuni maisha yanaendelea.
Kuna watu wanadhani hii ndio hasara ya kwanza kwa ATCL. CAG aliyepita Prof.Assad amewahi kuibua hasara kubwa zaidi ya hizi. But who cares?
Mwaka 2015/16 ATCL ilipata hasara ya 94.3Bil. Mwaka 2016/17 hasara ya 109.3Bil, na mwaka 2017/18 hasara ya 113.8Bil.
Kwahiyo hii 60Bil aliyoibua Kichere ni "cha mtoto" someni ripoti za Prof.Assad mtaona hasara ya mabilioni mengi zaidi. Tofauti ni kwamba wakati wa Assad ripoti zilizimwa. Wakubwa hawakupenda serikali "ichafuke". Lakini mama amekua tofauti. Anataka mambo yawekwe hdharani wananchi wajue. Transparency and accountability.
ZZK aliwahi kusema, sio kwamba serikali ya JPM ni safi sana, bali ilijitahidi kuficha taarifa watu wasijue. We unadhani JPM angekuwepo hii ripoti ya CAG ingesomwa kama ilivyosomwa? Thubutu.!
Watu wengi walisema serikali ya JK ilijaa ufisadi, lakini wasichoelewa ni kwamba JK mwenyewe alitaka watu wajue. We unadhani alishindwa kuzuia taarifa ya Richmond, EPA, Escrow etc? Alikua na uwezo wa kuzuia na wananchi wasijue chochote. Na angeondoka madarakani mnamsifia serikali yake ni clean. Lakini JK hakutaka "mapambio fake" aliamua kuweka kila kitu hadharani ili penye makosa paonekane na hatua zichukuliwe.
Serikali ya JPM haikutaka madhaifu yawekwe hadharani. Ndio maana CAG Assad aliibua madudu mengi lakini badala ya kupongezwa, akaonekana eti anaichafua nchi. Si unakumbuka ile kashfa ya 16Bil za jeshi la polisi kununua sare hewa? Iliishia wapi zaidi ya Kange Lugola kusema anajivua nguo na kumuita Prof.Assad muongo.
Bandarini kumejaa ufisadi mkubwa, lakini mkurugenzi wa bandari amekua akisifiwa sana na serikali ya JPM kuongeza mapato. Ndo ujue kuna watu walifanya ufisadi na kujificha kwenye kichaka cha Uzalendo. Leo mama ameagiza apelekewe ripoti ya BOT kuanzia January hadi March. Inadaiwa kuna mabilioni yalichotwa kwa "kisingizio" cha matibabu ya JPM.
Kwahiyo mama ameanza vizuri, lakini asiishie hapa. Mikataba ya miradi yote mikubwa iwekwe wazi. Wananchi wana haki ya kujua. Uwazi na uwajibikaji ni silaha muhimu kwenye utawala bora.!