Mimi, kama mwalimu wa shule za sekondari, ninapenda kutoa maoni yangu kuhusu mtaala mpya wa elimu kuanzia shule ya msingi hadi sekondari. Baada ya kupitia kwa makini, nimebaki na hofu kubwa kwamba kutokuwepo kwa somo la Maadili (Ethics) kama fani inayojitegemea kutaathiri malezi na mwongozo wa kizazi chetu katika karne hii.
Cha kushangaza, maadili yameunganishwa ndani ya somo la Historia ya Tanzania, ilhali historia tayari ipo kama somo huru. Kitendo hiki kimepunguza nguvu na uzito wa kufundisha maadili ipasavyo. Ni muhimu kujiuliza: kwa nini tusiyatenganishe masomo haya mawili? Tukiyatenganisha, tunaweza kuweka mkazo mahsusi katika kuandaa wataalamu wa maadili ambao watasaidia taifa kukabiliana na changamoto za mmomonyoko wa kimaadili.
Aidha, somo la Uraia (Civics) na General Studies limeondolewa katika mtaala. Je, dhamira ni nini? Je, tunataka kizazi kinachokuja kisijue namna serikali inavyofanya kazi, mgawanyo wa mihimili ya dola na uhusiano kati ya dola na wananchi? Hili ni kosa kubwa litakalotuletea gharama kubwa baadaye.
Wataalamu wa mitaala mnapaswa kuwa wazi: je, mlijadiliana na wabobezi wa falsafa na maadili kabla ya kufanya uamuzi huu? Kuna vyuo vikuu vikuu nchini vyenye idara za Falsafa na Maadili – kama UDSM, UDOM na SAUT – ambavyo vinafundisha somo hili kitaalamu. Kwa nini wasishirikishwe kuunda mtaala huu muhimu? Je, ni sahihi kuunda somo nyeti la maadili bila ushauri wa kitaalamu?
Ni jambo la kutia moyo kuwa masomo ya dini (Ukristo na Uislamu) yameingizwa rasmi katika mtaala, lakini ni lazima tukumbuke kwamba maadili ni msingi wa wote, hata wale wasio na dini. Maadili si historia; ni nguzo ya utu na ustawi wa taifa.
Mada Nyeti za Ethics zinazopaswa kufundishwa

- Uundaji wa dhamira (Formation of conscience)
- Utu na heshima ya binadamu (Human dignity & personhood)
- Maamuzi ya kimaadili na changamoto zake (Ethical decisions & dilemmas)
- Critical Thinking and Ethics – kufikiri kwa kina na kupima hoja za maadili
- Creative Problem Solving in Ethics – kutumia ubunifu kutatua changamoto za kimaadili
- Haki, usawa na wajibu wa kijamii (Justice, equality & social responsibility)
- Maisha ya ndoa na familia (Marriage, family & values)
- Haki za binadamu na uhuru wa kimaadili (Human rights & moral freedom)
- Maadili ya uongozi na utumishi wa umma (Leadership & integrity)
- Uwajibikaji katika mazingira na uumbaji (Environmental ethics)
- Maadili ya teknolojia na matumizi ya mitandao (Digital & AI ethics)
- Maadili ya kazi na taaluma (Professional & work ethics)
- Mizozo, amani na usuluhishi (Peace, conflict & reconciliation ethics)
- Maadili ya afya na tiba (Bioethics)
Mapendekezo ya Haraka kwa Wizara ya Elimu- Kuwashirikisha wataalamu wa falsafa na maadili ili kuandaa mtaala imara wa Ethics kama somo linalojitegemea.
- Kufanya mjadala mpana na wadau wa elimu kabla ya maamuzi ya mwisho pale tunapo fanya mabadiliko ya mitaala.
- Kutenga somo la Maadili na kulipa hadhi yake sawa na masomo mengine ya msingi.
- Kurudisha somo la Uraia na General Studies ili wanafunzi wajue muundo na uendeshaji wa serikali.
- Kuweka mkazo katika mafunzo ya maadili ya kisasa (Digital ethics, AI ethics, bioethics) ili kuandaa kizazi kinachokabiliana na changamoto za karne ya 21.
Maadili si historia, wala uraia si kitu cha hiari. Elimu bila msingi wa maadili na uraia ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga. Kama taifa, tusipochukua hatua sasa, tutajipatia anguko kubwa la kijamii na kimaadili katika siku zijazo.
Waziri wa Elimu na Katibu Mkuu, chukueni hatua za haraka. La sivyo, baada ya miaka michache, mtalaumiwa kwa maamuzi haya yaliyofanywa na vitengo vya mitaala pasipo kushirikisha wataalamu husika. Tukipuuzia nafasi ya Ethics katika elimu rasmi, tutaandaa mazingira ya anguko kubwa la kijamii, kiuchumi, na kimaadili nchini kwetu.