Pendekezo Rasmi kwa Wizara ya Elimu – Kitengo cha MitaalaYahusu: Umuhimu wa Kutenga Somo la Maadili (Ethics) kama Fani Inayojitegemea

Pendekezo Rasmi kwa Wizara ya Elimu – Kitengo cha MitaalaYahusu: Umuhimu wa Kutenga Somo la Maadili (Ethics) kama Fani Inayojitegemea

Ndugu yangu elimu ya bongo utaumiza kichwa Bure hamna atakayekuelewa.

Chuo kikuu masomo ya sayansi yalikuwa na somo.maalumu la practical linalojitegemea Kama course.

TCU wamekuja na maamuzi Yao kwamba practical isiwe course inayojitegemea badala yake practical itatoka ndani ya somonhusika analofundisha mwalimu. Hii ni kwa wale wanaofanya BSc with edu. Haya si mambo ya sekondari Sasa...

Anyway acha tunyamaze
 
Nchi imeoza sikuiz adi storekeeper anasomea degree Kiongozi akishaona ndugu yake kilaza anabadili mfumo ili tu aingie kweny system
 
Unajua walimu na Serikali wote mna akili ndogo Sana ya kuelewa mambo .
Samahani,hiyo elimu uliyokuwa nayo umeipata kupitia watu gani na serikali gani?? Yaani wewe una akili kuliko watu wote??

"Educated but ignorant" describes someone who has received a formal education and possesses knowledge in certain areas, yet still lacks a broader understanding of the world or critical thinking skills.

From AI

Nafikiri wewe ni :

limbukeni

mtu anayeanza kutumia au kupata kitu kwa mara ya kwanza

 
Mimi, kama mwalimu wa shule za sekondari, ninapenda kutoa maoni yangu kuhusu mtaala mpya wa elimu kuanzia shule ya msingi hadi sekondari. Baada ya kupitia kwa makini, nimebaki na hofu kubwa kwamba kutokuwepo kwa somo la Maadili (Ethics) kama fani inayojitegemea kutaathiri malezi na mwongozo wa kizazi chetu katika karne hii.

Cha kushangaza, maadili yameunganishwa ndani ya somo la Historia ya Tanzania, ilhali historia tayari ipo kama somo huru. Kitendo hiki kimepunguza nguvu na uzito wa kufundisha maadili ipasavyo. Ni muhimu kujiuliza: kwa nini tusiyatenganishe masomo haya mawili? Tukiyatenganisha, tunaweza kuweka mkazo mahsusi katika kuandaa wataalamu wa maadili ambao watasaidia taifa kukabiliana na changamoto za mmomonyoko wa kimaadili.View attachment 3443157

Aidha, somo la Uraia (Civics) na General Studies limeondolewa katika mtaala. Je, dhamira ni nini? Je, tunataka kizazi kinachokuja kisijue namna serikali inavyofanya kazi, mgawanyo wa mihimili ya dola na uhusiano kati ya dola na wananchi? Hili ni kosa kubwa litakalotuletea gharama kubwa baadaye.

Wataalamu wa mitaala mnapaswa kuwa wazi: je, mlijadiliana na wabobezi wa falsafa na maadili kabla ya kufanya uamuzi huu? Kuna vyuo vikuu vikuu nchini vyenye idara za Falsafa na Maadili – kama UDSM, UDOM na SAUT – ambavyo vinafundisha somo hili kitaalamu. Kwa nini wasishirikishwe kuunda mtaala huu muhimu? Je, ni sahihi kuunda somo nyeti la maadili bila ushauri wa kitaalamu?View attachment 3443158

Ni jambo la kutia moyo kuwa masomo ya dini (Ukristo na Uislamu) yameingizwa rasmi katika mtaala, lakini ni lazima tukumbuke kwamba maadili ni msingi wa wote, hata wale wasio na dini. Maadili si historia; ni nguzo ya utu na ustawi wa taifa.
Mada Nyeti za Ethics zinazopaswa kufundishwa

  1. Uundaji wa dhamira (Formation of conscience)
  2. Utu na heshima ya binadamu (Human dignity & personhood)
  3. Maamuzi ya kimaadili na changamoto zake (Ethical decisions & dilemmas)
  4. Critical Thinking and Ethics – kufikiri kwa kina na kupima hoja za maadili
  5. Creative Problem Solving in Ethics – kutumia ubunifu kutatua changamoto za kimaadili
  6. Haki, usawa na wajibu wa kijamii (Justice, equality & social responsibility)
  7. Maisha ya ndoa na familia (Marriage, family & values)
  8. Haki za binadamu na uhuru wa kimaadili (Human rights & moral freedom)
  9. Maadili ya uongozi na utumishi wa umma (Leadership & integrity)
  10. Uwajibikaji katika mazingira na uumbaji (Environmental ethics)
  11. Maadili ya teknolojia na matumizi ya mitandao (Digital & AI ethics)
  12. Maadili ya kazi na taaluma (Professional & work ethics)
  13. Mizozo, amani na usuluhishi (Peace, conflict & reconciliation ethics)
  14. Maadili ya afya na tiba (Bioethics)
    Mapendekezo ya Haraka kwa Wizara ya Elimu
    1. Kuwashirikisha wataalamu wa falsafa na maadili ili kuandaa mtaala imara wa Ethics kama somo linalojitegemea.
    2. Kufanya mjadala mpana na wadau wa elimu kabla ya maamuzi ya mwisho pale tunapo fanya mabadiliko ya mitaala.
    3. Kutenga somo la Maadili na kulipa hadhi yake sawa na masomo mengine ya msingi.
    4. Kurudisha somo la Uraia na General Studies ili wanafunzi wajue muundo na uendeshaji wa serikali.
    5. Kuweka mkazo katika mafunzo ya maadili ya kisasa (Digital ethics, AI ethics, bioethics) ili kuandaa kizazi kinachokabiliana na changamoto za karne ya 21.

      Maadili si historia, wala uraia si kitu cha hiari. Elimu bila msingi wa maadili na uraia ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga. Kama taifa, tusipochukua hatua sasa, tutajipatia anguko kubwa la kijamii na kimaadili katika siku zijazo.

      Waziri wa Elimu na Katibu Mkuu, chukueni hatua za haraka.
      La sivyo, baada ya miaka michache, mtalaumiwa kwa maamuzi haya yaliyofanywa na vitengo vya mitaala pasipo kushirikisha wataalamu husika. Tukipuuzia nafasi ya Ethics katika elimu rasmi, tutaandaa mazingira ya anguko kubwa la kijamii, kiuchumi, na kimaadili nchini kwetu.
Kumbukeni Aristotle aliwahi kusema (Educaing the mind without educating the soul is not education at all)
Katika zama hizi za utandawazi, changamoto ya kudorora kwa maadili imekuwa kubwa kwa jamii zetu. Wengi huamini kwamba shule zina wajibu wa kufundisha kila kitu, ikiwemo maadili. Lakini je, kila jambo lazima lifundishwe shuleni?
Ukweli ni kwamba familia ndiyo shule ya kwanza ya mtoto. Hapa ndipo mtoto hujifunza misingi ya heshima, upendo, mshikamano na uwajibikaji. Ikiwa malezi haya hayatawekwa nyumbani, shule itabeba mzigo mkubwa unaozidi uwezo wake wa kutoa elimu ya kitaaluma na kiufundi.
Shule, kwa upande wake, huchangia katika kuimarisha malezi kwa kuongeza elimu ya uraia, stadi za maisha na nidhamu ya kijamii. Hata hivyo, shule haiwezi kuchukua nafasi ya familia. Hivyo, mshikamano kati ya wazazi na walimu ni jambo lisiloepukika katika kujenga kizazi chenye maadili.
Jamii pia ina nafasi kubwa. Watoto na vijana wanapoishi katika mazingira yenye mifano mizuri ya uongozi, urafiki, na hata burudani, hujengeka kwa urahisi katika misingi bora. Kinyume chake, jamii isiyo na maadili huwaharibu hata wale waliopata malezi mazuri nyumbani na shuleni.
Ni kweli pia kuwa tasnia ya sanaa imekuwa na mchango mkubwa katika kuporomosha au kuinua maadili. Wasanii ni walimu wasio rasmi wa jamii. Wanapoweka misingi bora katika kazi zao, hujenga kizazi chenye mwelekeo chanya. Lakini kinyume chake, vijana huiga yale wanayoona na kusikia, na hatimaye jamii huathirika.
Kwa hiyo, jukumu la malezi bora ni la pamoja: familia huweka msingi, shule huimarisha, na jamii hukamilisha. Kama Watanzania, tunalo deni la kuhakikisha kuwa kizazi kinachokuja kinawarithi wazazi waliowalea kwa mfano wa heshima, maadili na uzalendo.
Huu ndiyo msingi wa taifa imara na maendeleo endelevu.
 
Umeongea vyema sana lakin pia watunga sera wamekua wababishaji sana madharani wanchokono chokonoa mofumu yet mfano kufuta somo la urai au general studies maana yake nini? Au wanataka ndo kizazi hiki kiwe cha ajabu zaidi? Elimu yetu imekua ya majaribio sana kiasi kwamba kila mtu anaeingia kwenye mfumo anaufanyia majaribio.
Mbili, kunasomo limeanzishwa hapo historia ya tanzania na maadili hoja msingi waache historia iwe historia na maadili yawe maadili walau wazazi wanapo kosa mda wa kukumbusha watoto wao walimu walio kasimishwa julumu hilo wawafundishe watoto taboa njema yaani the oughts to do and not to do! Tusipo kua serious na jambo hili tutaangaukia pua mda sio mrefu na dalili zote zinaonekana.
Dunia inaenda kasi sana wizara husika ishirikishe wabobezi kusaidia katika kuunda huu mtaala. Maadili ni somo nyeti sana ambalo kama nchi tunalipuuza sana.
 
Samahani,hiyo elimu uliyokuwa nayo umeipata kupitia watu gani na serikali gani?? Yaani wewe una akili kuliko watu wote??

"Educated but ignorant" describes someone who has received a formal education and possesses knowledge in certain areas, yet still lacks a broader understanding of the world or critical thinking skills.

From AI

Nafikiri wewe ni :

limbukeni

mtu anayeanza kutumia au kupata kitu kwa mara ya kwanza

Achana nae hajui anacho ongea inawezeakan ni mmoja wa wanafaika wali piga fedha za kuandaa mitaala kwa connection bila kushirikisha wataalum wa fani husika ndo maana hata argument zake zote ni emotional rather than clear with clarity! Mpuuze hajuia nalotenda likini ipo siku mwanae atatenda ndivyo sivyo na atakumbuka umuhimu wa somo hilo la maadili.
 
Back
Top Bottom