Zipo njia nyingi sana za kuongwza pesa kwa serikali kama:-
Kuhimiza Watanzania wengi wawe na passport na wafanye iwe rahisi kwao kusafiri nje ya nchi kufanya biashara na kazi.
Kupata passport haitakiwi utoe sababu yoyote iwe haki ya kimsingi.
Wapunguze ukiritimba, longolongo kupata export licenses. Watu wakitaka kuuza mazao yao, madini, samaki, maua, bidhaa zozote iwe rahisi.
Kutumia njia za ubunifu kuongeza watalii nchini. Kufanya process yote iwe rahisi kwa watalii kama kupata visa, usafiri, hotel, ndege, customer service nk.
Muhimu kuongeza vyanzo vya mapato kwa serikali kuliko kuwakamua watu wale wsle.
Watu milioni mbili tatu wakichukua passport, mapato makubwa kwa serikali.
Export licenses na biashara zao za kuuza nje zitaleta mapato zaidi kwa serikali.
Kwanini tusiwe na soko la kimataifa la mtandaoni kama Alibaba ambapo wakulima, wafanyabiashara wa Tanzania watauza bidhaa zao kwa yoyote,popote duniani kwa bei za ushindani.
Hapo serikali inaweza kuwa mtu wa kati kuhakikisha viwango na hakuna utapeli.