Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 2,318
- 8,464
Maendeleo hayana ubaguzi, kwakuwa ndani ya miaka zaidi ya 60 tumeshindwa kufanya mapinduzi kwenye sekta hata 1 niombe kwa heshima na taadhima tuiombe nchi ya Marekani itupatie vichwa 100 vitusaidie kutengeneza mfumo utakaoleta matokeo haraka na kutengeneza katiba mpya yenye tija.
Kwanza hao watu waje wazunguke nchi nzima waone rasilimali zilizopo kisha wakae chini waseme tukiwapa hii nchi kwa miaka 10 watatufikisha wapi, baada ya kutwambia tuwaruhusu waanze kazi.
Kwenye hivyo vichwa apatikane rais 1, waziri mkuu 1, speaker 1, mawaziri wa wizara zote, makatibu wakuu halafu sisi tujifunze toka kwao. Tuwape miaka 10 tu mtanishukuru.
In addition kipindi cha hiyo miaka 10 marekani na Tanzania tuingie makubaliano kuwa kwenda marekani itakuwa ni kama kwenda Zanzibar yaani ukiwa na kitambulisho cha NIDA tu unaenda na unaweza kufanya kazi, kusoma au kufanya biashara.
Naamini jambo hili litakuwa na tija sana na ndani ya miaka 10 kila Muafrika atatamani kuzamia Tanzania kutafuta maisha.