Wazo lako ni zuri. Ila limejikita kwenye ukweli kwamba Serikali inaweza ikaendelea kukulipa mshahara huo ambao unaupata kwa sasa. Lakini uchumi wa Dunia umeyumba vibaya sana. Wamarekani karibu milioni kumi hawana kazi. Tatizo hili pia linaweza kutokea hapa petu kwani sisi si kisiwa. Utalii ambao unachangia fedha nyingi za kigeni sasa si shwari tena. Na hata sekta ya Madini, Biashara, Usafiri hata zile sekta binafsi zote zinayumba. Je, Serikali inaweza kuhimili vishindo hivi vyote? . Ni wazi itafika mahali hata mishahara inaweza isipatikane na mkaombwa kugawana kidogo kitakachokuwepo. Ndoto ya asilimia mbili itaishia hapo hapo.