Pengine Umeshalishwa....

Ikena

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2007
Posts
553
Reaction score
397
Limbwata Alilomuwekea Bosi Wake Lampandisha Kizimbani

Mwanamke mmoja raia wa Indonesia amepandishwa kizimbani nchini Hong Kong kwa tuhuma za kuweka damu za hedhi kwenye chakula cha bosi wake kwa nia ya kuukuza uhusiano wao.
Indra Ningsih, mwenye umri wa miaka 26, alichanganya damu zake za hedhi kwenye sufuria la mboga za majani kwa nia ya kufanya uhusiano wake na bosi wake uwe mzuri zaidi, gazeti la The Standard la nchini humo liliripoti.

Damu za hedhi zinaaminika kuwa na nguvu kubwa za kuzidisha uhusiano kwa mujibu wa utamaduni wa mataifa ya kusini mashariki mwa bara la Asia.

Mwanamke huyo ameshtakiwa kwa makosa ya "kuweka sumu au kitu chenye madhara" kwa nia ya kudhuru lakini bado hajapandishwa kizimbani.

Taarifa za jalada la kesi hiyo zilisema kwamba Ningsih aliyekuwa ameajiriwa kama mfanyakazi wa ndani alishtukiwa kuweka limbwata lake hilo na bosi wake mwanamke aliyetajwa kwa jina la Mok ambaye aliingia jikoni na kumkuta mfanyakazi wake huyo wa ndani akifanya mambo ya kutia mashaka.

Mok aliingia jikoni na ghafla msaidizi wake huyo akatupa kitu kwenye mfuko wa taka.

Wakati alipofunua sufuria la mboga alikuta damu damu zikiwa zimechanganywa na maji na mboga za majani.

Mok baadae aligundua taulo la hedhi (Pads) lililotumika kwenye mfuko wa taka na kuamua kuwaita polisi, gazeti hilo lilisema.

Ningsih aliwaambia polisi kuwa bosi wake amekuwa hafurahishwi na kazi zake tangia alipomchukua mwezi julai mwaka jana hali iliyopelekea kumwekea limbata hilo.

Ningsih ameendelea kuwekwa mahabusu hadi kesi yake itakapotajwa tena, tarehe 13 mwezi ujao.

Hong Kong ina wafanyakazi wa majumbani 200,000 wengi wao wakitoka nchi za Philippines na Indonesia.

Source: http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=1771834&&Cat=7

Swali; kuna uhusiano gani kisayansi?
 
Du! hadi inatia kinyaa

Yak!!!

Binadamu kwa kweli wanatia kinyaa .. mimi ningeichukua hiyo pedi na kuhakikisha anailamba mpaka inakauka na anameza!

Duh... sijui hawa wa kwangu hapo hom wako sawa au ndio mambo ya mapishi!!!
 
Jamani waletaji wa mada zingine kuweni makini mnapozileta hapa TZ ,hawa dada zetu kwa akili zao za kuamini mambo kama hayo wanaweza kuja kujaribu. akili zao zinawatosheleza wenywe.
 
Yuuuuccck!!! Penzi halina dawa bana....utamlishaje mtu uchafu bila ridhaa yake? That's just plain nasty....yuuuuuck
 
Yuuuuccck!!! Penzi halina dawa bana....utamlishaje mtu uchafu bila ridhaa yake? That's just plain nasty....yuuuuuck
hakuna u nasty kwenye mapenzi.....kila kitu toka mwanamke ni sunna.....
 
Yuuuuccck!!! Penzi halina dawa bana....utamlishaje mtu uchafu bila ridhaa yake? That's just plain nasty....yuuuuuck

...nakweli, 🙁

hiari yashinda utumwa... hata wataalamu wa 'lamba-lamba' akilazimishwa alambe atauliza, "kulikoni?!"
 
Jamani waletaji wa mada zingine kuweni makini mnapozileta hapa TZ ,hawa dada zetu kwa akili zao za kuamini mambo kama hayo wanaweza kuja kujaribu. akili zao zinawatosheleza wenywe.

Inawezekana hasa kwa wanaopenda ushirikina. Wanaweza kudhani ndio aina mpya ya libwata.Kama tujuavyo,ushirikina unatabu zake.
 
umeshakula vingapi bila kujua bana? usiende kugombana na mkeo bure kama damu imewekwa kwenye supu ya moto si inaiva na inakuwa na zero infection, CHAUMBILE MUNGU NI CHA KUMEMENA
 
umeshakula vingapi bila kujua bana? usiende kugombana na mkeo bure kama damu imewekwa kwenye supu ya moto si inaiva na inakuwa na zero infection, CHAUMBILE MUNGU NI CHA KUMEMENA

... naaaam, inageuka kisusio 🙂
 
umeshakula vingapi bila kujua bana? usiende kugombana na mkeo bure kama damu imewekwa kwenye supu ya moto si inaiva na inakuwa na zero infection, CHAUMBILE MUNGU NI CHA KUMEMENA

Well, they say ignorance is bliss....kwa hiyo kama hujui basi hujui na mara ujuapo mambo hayatakuwa kama yalivyokuwa kabla ya kujua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…