Limbwata Alilomuwekea Bosi Wake Lampandisha Kizimbani
Mwanamke mmoja raia wa Indonesia amepandishwa kizimbani nchini Hong Kong kwa tuhuma za kuweka damu za hedhi kwenye chakula cha bosi wake kwa nia ya kuukuza uhusiano wao.
Indra Ningsih, mwenye umri wa miaka 26, alichanganya damu zake za hedhi kwenye sufuria la mboga za majani kwa nia ya kufanya uhusiano wake na bosi wake uwe mzuri zaidi, gazeti la The Standard la nchini humo liliripoti.
Damu za hedhi zinaaminika kuwa na nguvu kubwa za kuzidisha uhusiano kwa mujibu wa utamaduni wa mataifa ya kusini mashariki mwa bara la Asia.
Mwanamke huyo ameshtakiwa kwa makosa ya "kuweka sumu au kitu chenye madhara" kwa nia ya kudhuru lakini bado hajapandishwa kizimbani.
Taarifa za jalada la kesi hiyo zilisema kwamba Ningsih aliyekuwa ameajiriwa kama mfanyakazi wa ndani alishtukiwa kuweka limbwata lake hilo na bosi wake mwanamke aliyetajwa kwa jina la Mok ambaye aliingia jikoni na kumkuta mfanyakazi wake huyo wa ndani akifanya mambo ya kutia mashaka.
Mok aliingia jikoni na ghafla msaidizi wake huyo akatupa kitu kwenye mfuko wa taka.
Wakati alipofunua sufuria la mboga alikuta damu damu zikiwa zimechanganywa na maji na mboga za majani.
Mok baadae aligundua taulo la hedhi (Pads) lililotumika kwenye mfuko wa taka na kuamua kuwaita polisi, gazeti hilo lilisema.
Ningsih aliwaambia polisi kuwa bosi wake amekuwa hafurahishwi na kazi zake tangia alipomchukua mwezi julai mwaka jana hali iliyopelekea kumwekea limbata hilo.
Ningsih ameendelea kuwekwa mahabusu hadi kesi yake itakapotajwa tena, tarehe 13 mwezi ujao.
Hong Kong ina wafanyakazi wa majumbani 200,000 wengi wao wakitoka nchi za Philippines na Indonesia.
Source: http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=1771834&&Cat=7
Swali; kuna uhusiano gani kisayansi?