Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Kukaaa kimya siku zoote yaaani ndo kaja na hili la katiba yoooote yanayotoke kimya!!!! 00
 

Hapana. JPM haungwi mkono na kanisa. Pengo ni askofu wa dar es salaam. Unapoongelea kanisa katoliki Tz, unaongelea TEC. Sidhani kama TEC imetoa tamko la kumuunga mkono Magufuli.
 
Kadinali Pengo huwa namkubali sana huwa ana msimamo thabiti lakini kikubwa zaidi ana uelewa wa hali ya juu sana,
 
Pengo ilibidi atoe maoni yake binafsi kama alivyofanya Niwemugizi, hakupaswa kumwongelea kabisa, akiulizwa amekula maharage ya wapi ataanza kununa bure
 
Samahani naomba kuuliza, hivi kitendo cha Askofu wa jimbo kuu la Dar kujigeuza kuwa msemaji wa baraza la Maaskofu Tanzania siyo utomvu wa nidhamu? Hatakiwi kuwajibishwa? Hivi katika historoa ya Kanisa Katoliki Duniani, imeshawahi kutokea kukawa na Kardinali asiye na impact yoyote kwa jamii na kwa taifa kama tuliyemwona leo kwenye TV? Hivi ni kwanini kuna pengo kubwa sana kati ya Pengo na wananchi?
 
Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.
Mkuu katiba mpya muhimu lakini sio kipaumbele chetu.

Elimu na Afya pamoja na huduma za jamii kama maji safi ndio vipaumbele. Hata Lowassa na UKAWA waliipa elimu kipaumbele ktk ile kauliu ya ELIMU, ELIMU, ELIMU.

Pia usiwasemee watu kwamba wengi kipaumbele chetu ni katiba kabla ya kura ya maoni. Hivi sasa ukizunguka nchi nzima ukauliza tufute elimu bure na mipango ya maendeleo kisha pesa tuelekeze kwenye kupata katiba mpya utapata kuungwa mkono na angalau 51% ya watanzania wote?
 
Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.
Hawezi kukemea kama alivyofanya kwenye utawala wa jk. Kwasababu sasa hivi wao kila kitu wanachotaka kutoka serikalini wanapata bila shida yoyote na wala hawahojiwi na mtu. Ndoomana hujasikia hata siku moja kanisa likilaani mambo yanavyokwenda kwa sasa.

Na kama unakumbuka ni lazima aseme hivyo kumbuka kwanini pendo alitukanwa na Gwajima? Kwasababu yeye aliwazunguka wenzake na kwenda kamshauri jk akatae katiba mpya. Na kumbuka wakati jk anahutubia bunge alisemaje? Ameshauriwa na kiongozi mkubwa wa dini kwamba.
 
Reactions: BAK
Jamani mbona Yule Askofu alisema yale yalikuwa mawazo yake? Sio mawazo ya kanisa, na alisema yuko tayari kuitwa mchochezi mbona mnapotosha?
 
Hivi haya ulosema hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba?,hivi hizo Huduma mnazosema ni akina nani zinawahusu?,katiba inalinda utu wa MTU,inasimamia taratibu sahihi za kustawisha utu na maisha ya MTU,sasa ni MTU wa aina gani ambae hata akipewa Huduma bora lkn anafinyangwa utu wake atae furahia Huduma hizo,
 
Ni mtu mwenye akili finyu tu ambaye anaweza kusema katiba mpya si kipaumbele cha nchi. Huwezi kuwa na Serikali bora ambayo inajua fika itaiba kura ili kung'ang'ania madarakani hivyo hata IVURUNDE vipi haina hofu tena kwa wapiga kura maana wanajua watashinda tu. Kutoongwa mkono na 51% ya Watanzania katika kupata katiba mpya haina maana katiba hiyo haina umuhimu. Tatizi ni hao watakaoikataa hiyo katiba mpya kiwango chao cha elimu ni kipi?

Hata vyama vingi wengi hawakuvitaka kama si Baba wa Taifa leo hii baada ya miaka 56 bado tungekuwa na chama kimoja. Imagine madudu chungu nzima ya hawa wahuni na mafisadi ambayo yamewekwa hadharani na vyama vya upinzani tangu tulipoanza rasmi mfumo huo 1992. Fungua akili yako uone mbali zaidi.


 
Kwa hiyo hii kauli yako ndiyo msimamo wa kanisa...au nayo ni maoni yako binafsi!?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…