Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakati wa Jakaya Kanisa lilishiriki kuishinikiza Serikal kuleta Katiba Mpya japo hapakuwa na Huduma bora, Leo Wanatumia kigezo cha Huduma bora kukataa Katiba Mpya, kweli Mchezaji kwao hutuzwa,
Hongera Rais John Joseph kwa kuungwa Mkono na Kanisa kwa kila jambo
Mwadhama Kadinali, Polycarp Pengo amesema kwamba kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge mkoani Kagera, Severine Niwemugizi kwamba Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni binafsi siyo msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.
Pengo alisisitiza hilo wakati akitoa ufafanuzi juu ya sintofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.
“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo siyo msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimao wa kanisa kwa sababu sisi tuna taratibu zetu za kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.
Alifafanua zaidi kwamba kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndio msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge, Ngara lakini kimsingi kauli ile imekosa vigezo vya kuichukulia kama msimamo wa kanisa au jimbo anakotoka.
Kadinali Pengo alisema yeye binafsi kipaumbele chake ni kuona huduma za jamii kama zile elimu na afya zinaendelea kuboreshwa kwa kasi kama ambavyo Serikali ilivyoanza kufanya.
“Mtu akiniambia priority (kipaumbele) ya Tanzania ni Katiba mpya inabidi anithibitishie huo ukipaumbele maana siwezi kuona mtoto anakufa kwa njaa au kwa kukosa dawa eti kwa sababu ya Katiba mpya. Kwangu mimi Katiba ni kitu ambacho kije baadaye, si cha haraka.
“Wanasiasa wasiache watoto wetu wafe kwa njaa kisa malumbano ya Katiba. Wasiache watoto wakose shule kwa sababu hela zote zimeishia kwenye malumbano juu ya Katiba,” alisisitiza Kadinali Pengo.
Kwa upande wake Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Marek Solczynski hakutofautiana na kauli ya Kadinali Pengo kwa kusema pamoja na kwamba Askofu Niwemugizi ana haki ya kutoa maoni yake lakini tatizo linakuja pale watu wakaposhindwa kung’amua kuwa ni maoni binafsi au ni ya kanisa.
Amesisitiza kwamba kanisa lina taratibu zake za kutoa maoni kwa masuala ya kijamii na kwa Serikali. “Hayo ni maoni yake binafsi na wala yasihusishwe na kanisa katoliki,” alisema Balozi Askofu Merek.
Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kipaumbeke cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza yeye binafsi ni miongini mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.
Hata hivyo, wachambuzi wa mambo walisema, pamoja na mjadala mkubwa ulioibuka na baadhi ya wanasiasa kususia mchakato wa kukamilisha Katiba mpya, wataalamu wa sheria wanasema Katiba inayopendekezwa ilikuwa ni bora kuliko ya sasa ikiwemo kuruhusu wagombea kuhoji mahakamani matokeo mbalimbali ikiwemo ya urais.
“Hata mimi ukiniuliza leo tuache kufanya mageuzi ya msingi katika jamii ili kuwa na uchumi imara au tuanze kushughulika na Katiba mpya, nitakwambia tuachane na Katiba.
“Nakumbuka ile Katiba Inayopendekezwa ilikuwa na masuala makubwa yenye maslahi kwa nchi ikiwemo kipengele cha kupinga matokeo ya urais lakini kwa kuwa kuna watu walikuwa na maslahi yao binafsi, wakatoka nje ya Bunge na kukwamisha mchakato ule sioni uharaka wa leo tuache mengine yote turejee kwenye mchakato huu,” alisema Wakili wa Mahakama Kuu, James Nandonde.
CHANZO: Mwananchi
Kwa kauli ya Niwemugizi soma zaidi hapa;
Askofu Niwemugizi asema yuko tayari kuitwa mchochezi
Mkuu katiba mpya muhimu lakini sio kipaumbele chetu.Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.
Kipande cha haki kitashindaKanisa katoliki vipande 2 kisa Magu
Hawezi kukemea kama alivyofanya kwenye utawala wa jk. Kwasababu sasa hivi wao kila kitu wanachotaka kutoka serikalini wanapata bila shida yoyote na wala hawahojiwi na mtu. Ndoomana hujasikia hata siku moja kanisa likilaani mambo yanavyokwenda kwa sasa.Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.
Hivi haya ulosema hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba?,hivi hizo Huduma mnazosema ni akina nani zinawahusu?,katiba inalinda utu wa MTU,inasimamia taratibu sahihi za kustawisha utu na maisha ya MTU,sasa ni MTU wa aina gani ambae hata akipewa Huduma bora lkn anafinyangwa utu wake atae furahia Huduma hizo,Mkuu katiba mpya muhimu lakini sio kipaumbele chetu. Elimu na Afya pamoja na huduma za jamii kama maji safi ndio vipaumbele. Hata Lowassa na UKAWA waliipa elimu kipaumbele ktk ile kauliu ya ELIMU, ELIMU, ELIMU. Pia usiwasemee watu kwamba wengi kipaumbele chetu ni katiba kabla ya kura ya maoni. Hivi sasa ukizunguka nchi nzima ukauliza tufute elimu bure na mipango ya maendeleo kisha pesa tuelekeze kwenye kupata katiba mpya utapata kuungwa mkono na angalau 51% ya watanzania wote?
Katiba wanayo Ila siyo written constitution. Hebu rudi Form 2Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Mkuu katiba mpya muhimu lakini sio kipaumbele chetu. Elimu na Afya pamoja na huduma za jamii kama maji safi ndio vipaumbele. Hata Lowassa na UKAWA waliipa elimu kipaumbele ktk ile kauliu ya ELIMU, ELIMU, ELIMU. Pia usiwasemee watu kwamba wengi kipaumbele chetu ni katiba kabla ya kura ya maoni. Hivi sasa ukizunguka nchi nzima ukauliza tufute elimu bure na mipango ya maendeleo kisha pesa tuelekeze kwenye kupata katiba mpya utapata kuungwa mkono na angalau 51% ya watanzania wote?