Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.
Pamoja na uhuru uliokuwa na wa kutoa mawazo, BAK, maneno uliyotumia kujadili mada kuhusu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, Mhadhama Kardinali Pengo, ni ya kitoto. Kama wewe ni mtu mzima ni mtu mzima hovyo.

Siyo tu umemdharirisha kama yeye, bali hata nafasi katika jamii, Kanisa Katoliki na waumini wake wote.

Sikubali kwamba kauli ya Askofu mtajwa na Kardinali Pengo inawakilisha mawazo ya Watanzania mlio wengi. Ni kauli inayowakilisha wanasiasa wenye uchu wa madaraka.

Niliwahi kuandika humu jamvini, kwamba wanaotaka Katiba mpya si wananchi ila wanasiasa tena uchwara. Katika Katiba JMT, nikikuuliza ni Ibara ipi inamnyima raia kufanya shughuli zake za kimaendeleo, au haki na uhuru wake? Utabaki kuropoka tu.

JITAMBUE KWANZA NDIO UWEZE KUMJIBU MTU KAMA MHADHAMA KARDINALI PENGO.

Kama hukufunzwa na wazazi wako, utafunzwa na dunia. Hata maandiko matakatifu yanatutaka kutii mamlaka, na kuheshimu wazazi, tupate maisha mema na bora duniani.
 
Kati ya vitu vinavyo nifanya nisiende kanisani, Pengo namba moja. Akitoka madarakani ntarudi kwa nguvu zote.
 
esitena tetena,

Pengo akitaka kujua kama ni msimamo wa Kanisa au la,Aendeshe kura ya maoni miongoni mwa Wakatoliki tupate jibu kamili siyo kupinga tu! Katiba Mpya ndo yenyewe.
 
Hata wakati wa Kikwete,Pengo haelewekieleweki au umesahau kipindi Gwajima anamuuliza maharage aliyokula ameyatoa wapi?
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi, gwajima alishawahi kumwambia hivyo hivyo lkn bado hajasikia anajiona boss wa kanisa katoliki tz kitu ambacho sio kweli, hata aliyoyasema yeye ni maoni yake binafsi na sio msimamo wa kanisa
 
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
We kwani hujamsikia vizuri, anapinga katiba mpya huyu mzee, katumwa na magufuli
 
um

Unapotosha umma wewe kardinal ni mkuu wa kanisa Katoliki nchni na hakuna askof anayeteuliwa bila mapendekezo yake na ushauri kwa papa sasa leo hii unadanganya na kumlingansha shekh mkuu wa mkoa dsm na mashekh wa mikoa mingne unakosea ukweli ulipaswa kumlingasha muft wa tanzana na shekh wa mkoa wowote Tanzana na jibu ni kwamba anayeshikilia cheo cha kitaifa ndiyo boss wa wote hayo mengine ni utendaji wa ndani ya Kanisa.
 
BAK katumia maneno yapi mabaya? Huyo Pengo ashavimbiwa vya kunyonga sasa hivi anatupumilia tu hewa chafu

Halafu huyo ni mwanadamu kama wewe kuwa Kadrinali hakumfanyi awe malaika hivyo akiongea ujinga atakosolewa tu
 
Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Ile ni nchi ya kifalme huwezi kuifananisha na tz nchi ya democracy
 
Huyu ni askofu wangu jimbo la Dar ila kwa hili hapana simuungi hata kidole.
 
esitena tetena,

Sitaacha kuwa Mkatoliki maana wewe pengo sio Yesu ila hapo babaumechemka. Hata kama nimwenzetu kama ni lazima tumpinge na tumpinge tu.Je tulipoteza hela bure kuandaa katiba mpya? Nashauri waumini wa Dar tuprotest kwa kukataa kutoa sadaka jumapili ya kesho ili tutume ujumbe kwa Pengo aache kurudi na mtawala kisa ni mmoja wetu.
 
Huyu hafai kabisa kuwa kiongozi wa kanisa ni mnafiki na haaminiki
 
Kanisa katoliki linaangalia upande wenye maslai
 
Ahadi 70 au 120 Mkuu?
Mwa 6:3
Ufafanuzi tafadhali.
Mkuu ni 70 ukiwa na nguvu basi 80 mambo ya agano la kale yamefanyiwa review na ujio wa Bwana Yesu

Huko kwenye agano la kale kuna walio ishi miaka 900 je unafikiria inawezekana kwa sasa hivi kuishi miaka 900?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…