Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Hufuati kauli ya Askofu? Basi wewe si Mkatoliki. Kama unatawaliwa na ushawishi wako unatawaliwa na ushawishi wa shetani. Endelea na hoja yako kama katiba inavyokuruhusu lakini futa kusingizio cha ukatoliki.
 
Baba Pengo Kaa kimya ! Watanzania tunataka KATIBA MPYA !! au unataka yatokee ya Rwanda ndiyo uamke...? Tunajuwa katoliki ndiyo Dola lakini jaribuni kuuma na kupuliza jamani ....!!
 
Mh. Pengo upo sahihi kabisa. Kipaumbele cha Watanzania ni maisha bora, siyo katiba.
Nayasema haya kwa sababu naamini mtu hawezi kula katiba, hawezi kuvaa katiba, hawezi kutibiwa na katiba.
Ebu tujiulize, katika familia zetu kuna katiba?

Bila shaka hakuna, na mambo yote katika familia zetu yanatekelezwa vizuri na kwa ufanisi mzuri tu pamoja na kutokuwa na katiba ya familia.
 
Wew ndiye unayetakiwa utie akili kidogo kwa sababu pamoja na hao viongozi wastaafu kuongea bado hautakuwa misimamo wa watanzani, elewa hiyo itakuwa bado ni misimamo yao. Vinginevyo tutaishia kusema ni siasa.

NB : yako mambo ambayo siyaungi mkono yanayofanywa na huyo magufuli
 
Kwanza ulisema ni msimamo wangu sasa unabadili na kusema ni misimamo yao! Hujitambui weye hata chembe unaruka ruka huku na kule bila kujua unachoandika.


 
Siyo kweli. Katiba kwenye ngazi ya familia ipo. Wajibu wa baba, mama na watoto uko wazi. Mambo haya hayaingiliani. Hata kama kuna house girl kazi na majukumu yake yana mipaka.

Uendeshaji wa nchi unafuata STK yaani sheria,taratibu na Kanuni. Hiyo ndiyo Katiba.

Maendeleo hayawezi kuja bila katiba vinginevyo kutakuwa na upendeleo. Upendeleo huzaa manunguniko,na manunguniko hukosesha Amani
 
Huyu mzee Pengo hovyo kweli. Mbona kanisa lake limeweka katiba na anayeivunja anatengwa? Kwahiyo hakuna hata haja ya katiba ya kanisa? Mbona mnawakataza watu wasile nyama ijumaa kuu? Je wale tu ili wasife na njaa? Mzee emb staafu urudi Katavi ukalime upambane na njaa na maradhi.
 
Bishop Gwajima nakusihi popote ulipo amsha dude umetulia naona watesi wetu wanainuka tena.
 
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
Na yeye ni maoni yake binafsi maana nae sio msemaji wa Kanisa
 
Huyu mzee apumzike, nikiwa mkatoliki na niliyelelewa kikatoliki haswaaa! Nasema Pengo anatumika vibaya na Serikali, ni kigeugeu sana huyu mzee, na anatuzamishia meli wakristo, sijui kwa maslahi yapi,... Simuungi mkono kabisaaaa
 
Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Kwetu katiba mpya siyo kipaumbele kwa ajli ya maendeleo bali usalama wetu na ustawi wa taifa letu. Amani ndio msingi wa furaha kwa sisi maskini.
Kwani kwa miaka yote, hiyo katiba mbovu imeleta maendeleo yapi ya kujivunia?
 
Tusizungushe akili za watu bure, Wakatoliki tumekuwa na ubinafsi sana hasa endapo mgombea anatokea katika dhehebu letu la RC, nakumbuka sana namna maaskofu walivyo kimya hata kwa ukiukaji wa katiba na namna demokrasia inavyokandamizwa. Wakati wa Jakaya ilikuwa daily matamko kutoka kwa maaskofu. Mhashama huyu anatakiwa aelewe kuwa hata upande mwingine unaweza toa raisi mwenye busara zaidi.
 
[emoji23] [emoji23] Watu wanajihami, Gwajima Sijui kama leo atamuacha salama.
 
Alifafanua zaidi kwamba kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndio msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge,Ngara lakini kimsingi kauli ile imekosa vigezo vya kuichukulia kama msimamo wa kanisa au jimbo anakotoka."


Sasa nyie mlitaka Pengo aseme huwa ni msimamo wa kanisa au vp? Hata mnacholalamika humu hakieleweki.
 
Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.
Ni hivi, hata kauli ya Pengo siyo msimamo wa Kanisa, na mimi ni mkatoliki. Pengo ni Askofu wa jimbo la Dar na si kiongozi wa wakatoliki wote.

Yeye ana bahati amechaguliwa na Papa kuwa kadinari lakini si kwamba yuko juu ya maaskofu wengine.

Papa anateuwa hata padri ambaye hajawa Askofu kuwa kadinari.

Kuna uchawi Pengo amewaloga watu wanadhani yeye ndio kiongozi wetu mkuu hapa Tanzania, hapana, Pengo ni kada wa ccm ndio sababu anapewa airtime kupotosha.
 
Hata ushuzi aliiongea Pengo siyo msimamo wa kanisa.

Msimamo wa kanisa unatolewa na Rais wa TEC.

Pengo ametowa maoni yake kama kada wa ccm.
 
pengo anatuzngua ... yan iman catholik wanaitumia vbaya sana (serikar) . Arf ni kwel mzee angestaafu tu kwan ni mgonjwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…