Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Siyo kweli! Mimi ni Mkatoliki na sifuati kauli tu kwa vile imesemwa na papa, askofu, padre, katekista au kiongozi wa jumuiya ndogondogo mpaka iwe na ushawishi kwangu kwamba haipingani na neno la Mungu na ina mchango chanya kwa imani ya Kanisa na imani yangu na pia ustawi wangu na wa familia yangu. Nje ya criteria hii, papa, askofu, padre, katekista au kiongozi wa jumuiya ndogondogo anajisumbua maana sitafuata neno lake. Hivyo, siyo kweli kwamba "Wakatoliki ni watiifu kwa viongozi wao". Labda ungesema "baadhi ya Wakatoliki ni watiifu kwa viongozi wao" (maana hata wakiambiwa mambo yasiyo ya msingi wanatii). Kwangu siyo hivyo - hata mahubiri ya padre nayachuja kama hayakidhi kiwango hata sisikilizi, natoka nje ili amalize au nakacha kabisa. Ninafuata imani yangu kwa uhuru na si kwa kumwogopa kiongozi wa kiroho maana hivi ndivyo nilivyoelelewa.
Hufuati kauli ya Askofu? Basi wewe si Mkatoliki. Kama unatawaliwa na ushawishi wako unatawaliwa na ushawishi wa shetani. Endelea na hoja yako kama katiba inavyokuruhusu lakini futa kusingizio cha ukatoliki.
 
Baba Pengo Kaa kimya ! Watanzania tunataka KATIBA MPYA !! au unataka yatokee ya Rwanda ndiyo uamke...? Tunajuwa katoliki ndiyo Dola lakini jaribuni kuuma na kupuliza jamani ....!!
 
Mh. Pengo upo sahihi kabisa. Kipaumbele cha Watanzania ni maisha bora, siyo katiba.
Nayasema haya kwa sababu naamini mtu hawezi kula katiba, hawezi kuvaa katiba, hawezi kutibiwa na katiba.
Ebu tujiulize, katika familia zetu kuna katiba?

Bila shaka hakuna, na mambo yote katika familia zetu yanatekelezwa vizuri na kwa ufanisi mzuri tu pamoja na kutokuwa na katiba ya familia.
 
Mtazamo wa Watanzania wengi hata Viongozi wastaafu ambao wamemkoromea huyo dikteta uchwara na hawa ni MACCM wala si wa upizani. Mwinyi, Butiku, Warioba, Kinana na hata Kikwete wiki chache zilizopita kabla ya shambulizi la Lissu alimkoromea kwamba wapinzani si maadui wa Serikali, lakini cha kushangaza huyo askofu uchwara yeye haoni maovu yanayotendwa na huyo dhalimu.

Tia akili kichwani badala ya kukurupuka eti ni msimamo wangu!
Wew ndiye unayetakiwa utie akili kidogo kwa sababu pamoja na hao viongozi wastaafu kuongea bado hautakuwa misimamo wa watanzani, elewa hiyo itakuwa bado ni misimamo yao. Vinginevyo tutaishia kusema ni siasa.

NB : yako mambo ambayo siyaungi mkono yanayofanywa na huyo magufuli
 
Kwanza ulisema ni msimamo wangu sasa unabadili na kusema ni misimamo yao! Hujitambui weye hata chembe unaruka ruka huku na kule bila kujua unachoandika.



Wew ndiye unayetakiwa utie akili kidogo kwa sababu pamoja na hao viongozi wastaafu kuongea bado hautakuwa misimamo wa watanzani, elewa hiyo itakuwa bado ni misimamo yao.
Vinginevyo tutaishia kusema ni siasa.
NB : yako mambo ambayo siyaungi mkono yanayofanywa na huyo magufuli
 
Mh. Pengo upo sahihi kabisa. Kipaumbele cha Watanzania ni maisha bora, siyo katiba.
Nayasema haya kwa sababu naamini mtu hawezi kula katiba, hawezi kuvaa katiba, hawezi kutibiwa na katiba.
Ebu tujiulize, katika familia zetu kuna katiba?
Bila shaka hakuna, na mambo yote katika familia zetu yanatekelezwa vizuri na kwa ufanisi mzuri tu pamoja na kutokuwa na katiba ya familia.
Siyo kweli. Katiba kwenye ngazi ya familia ipo. Wajibu wa baba, mama na watoto uko wazi. Mambo haya hayaingiliani. Hata kama kuna house girl kazi na majukumu yake yana mipaka.

Uendeshaji wa nchi unafuata STK yaani sheria,taratibu na Kanuni. Hiyo ndiyo Katiba.

Maendeleo hayawezi kuja bila katiba vinginevyo kutakuwa na upendeleo. Upendeleo huzaa manunguniko,na manunguniko hukosesha Amani
 
Huyu mzee Pengo hovyo kweli. Mbona kanisa lake limeweka katiba na anayeivunja anatengwa? Kwahiyo hakuna hata haja ya katiba ya kanisa? Mbona mnawakataza watu wasile nyama ijumaa kuu? Je wale tu ili wasife na njaa? Mzee emb staafu urudi Katavi ukalime upambane na njaa na maradhi.
 
Bishop Gwajima nakusihi popote ulipo amsha dude umetulia naona watesi wetu wanainuka tena.
 
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
Na yeye ni maoni yake binafsi maana nae sio msemaji wa Kanisa
 
Huyu mzee apumzike, nikiwa mkatoliki na niliyelelewa kikatoliki haswaaa! Nasema Pengo anatumika vibaya na Serikali, ni kigeugeu sana huyu mzee, na anatuzamishia meli wakristo, sijui kwa maslahi yapi,... Simuungi mkono kabisaaaa
 
Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Kwetu katiba mpya siyo kipaumbele kwa ajli ya maendeleo bali usalama wetu na ustawi wa taifa letu. Amani ndio msingi wa furaha kwa sisi maskini.
Kwani kwa miaka yote, hiyo katiba mbovu imeleta maendeleo yapi ya kujivunia?
 
Nathubutu kusema Askofu wangu Pengo uzee unamwingia vibaya...hata hekima ile ya kawaida ambayo angeweza kuwa nayo kijana form four failure kwake imeshaondoka{natubu kunena haya juu ya mpakwa mafuta}ila ukweli lazima usemwe!!!sijui amehongwa au ninini sijui,labda nae anautafuta ukuu wa wilaya?!au ukatibu mkuu!inasikitisha.
Tusizungushe akili za watu bure, Wakatoliki tumekuwa na ubinafsi sana hasa endapo mgombea anatokea katika dhehebu letu la RC, nakumbuka sana namna maaskofu walivyo kimya hata kwa ukiukaji wa katiba na namna demokrasia inavyokandamizwa. Wakati wa Jakaya ilikuwa daily matamko kutoka kwa maaskofu. Mhashama huyu anatakiwa aelewe kuwa hata upande mwingine unaweza toa raisi mwenye busara zaidi.
 
[emoji23] [emoji23] Watu wanajihami, Gwajima Sijui kama leo atamuacha salama.
 
Alifafanua zaidi kwamba kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndio msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge,Ngara lakini kimsingi kauli ile imekosa vigezo vya kuichukulia kama msimamo wa kanisa au jimbo anakotoka."


Sasa nyie mlitaka Pengo aseme huwa ni msimamo wa kanisa au vp? Hata mnacholalamika humu hakieleweki.
 
Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.
Ni hivi, hata kauli ya Pengo siyo msimamo wa Kanisa, na mimi ni mkatoliki. Pengo ni Askofu wa jimbo la Dar na si kiongozi wa wakatoliki wote.

Yeye ana bahati amechaguliwa na Papa kuwa kadinari lakini si kwamba yuko juu ya maaskofu wengine.

Papa anateuwa hata padri ambaye hajawa Askofu kuwa kadinari.

Kuna uchawi Pengo amewaloga watu wanadhani yeye ndio kiongozi wetu mkuu hapa Tanzania, hapana, Pengo ni kada wa ccm ndio sababu anapewa airtime kupotosha.
 
Alifafanua zaidi kwamba kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndio msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge,Ngara lakini kimsingi kauli ile imekosa vigezo vya kuichukulia kama msimamo wa kanisa au jimbo anakotoka."


Sasa nyie mlitaka Pengo aseme huwa ni msimamo wa kanisa au vp? Hata mnacholalamika humu hakieleweki.
Hata ushuzi aliiongea Pengo siyo msimamo wa kanisa.

Msimamo wa kanisa unatolewa na Rais wa TEC.

Pengo ametowa maoni yake kama kada wa ccm.
 
pengo anatuzngua ... yan iman catholik wanaitumia vbaya sana (serikar) . Arf ni kwel mzee angestaafu tu kwan ni mgonjwa sana
 
Back
Top Bottom