Siyo kweli! Mimi ni Mkatoliki na sifuati kauli tu kwa vile imesemwa na papa, askofu, padre, katekista au kiongozi wa jumuiya ndogondogo mpaka iwe na ushawishi kwangu kwamba haipingani na neno la Mungu na ina mchango chanya kwa imani ya Kanisa na imani yangu na pia ustawi wangu na wa familia yangu. Nje ya criteria hii, papa, askofu, padre, katekista au kiongozi wa jumuiya ndogondogo anajisumbua maana sitafuata neno lake. Hivyo, siyo kweli kwamba "Wakatoliki ni watiifu kwa viongozi wao". Labda ungesema "baadhi ya Wakatoliki ni watiifu kwa viongozi wao" (maana hata wakiambiwa mambo yasiyo ya msingi wanatii). Kwangu siyo hivyo - hata mahubiri ya padre nayachuja kama hayakidhi kiwango hata sisikilizi, natoka nje ili amalize au nakacha kabisa. Ninafuata imani yangu kwa uhuru na si kwa kumwogopa kiongozi wa kiroho maana hivi ndivyo nilivyoelelewa.